prev

Al-Fath

next

1 : 48

إِنَّا فَتَحۡنَا لَكَ فَتۡحٗا مُّبِينٗا

Sisi tumekufungulia wewe (tumekupa ushindi), ewe Mtume, ushindi ulio wa dhahiri, ambao ndani yake Allah Mtukufu Ataipa nguvu Dini yake na Atakupa ushindi juu ya maadui wako, na ushindi huo ni mapatano ya (Ḥudaybiyah), ambayo kwayo watu waliingia katika amani, na zikapanuka juhudi za ulinganizi wa Dini ya Allah Mtukufu, na watu wakaingia kwenye Dini ya Allah Mtukufu makundi kwa makundi. Kwa sababu hiyo, Allah Mtukufu Aliyaita mapatano hayo “ushindi ulio wa wazi” yaani uliokuwa wazi wenye kujitokeza. info
التفاسير: |

2 : 48

لِّيَغۡفِرَ لَكَ ٱللَّهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنۢبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكَ وَيَهۡدِيَكَ صِرَٰطٗا مُّسۡتَقِيمٗا

Tumekufungulia ufunguzi huo wa ushindi na tukakufanyia sahali, ili Allah Mtukufu Akusamehe dhambi zako zilizotangulia na za baadae, kwa sababu ya utiifu mwingi ulioufanya unaotokana na ushindi huu, na kwa tabu uliyoivumilia, na ili Akutimizie neema Zake kwako, kwa kuipa ushindi Dini yake. info
التفاسير: |

3 : 48

وَيَنصُرَكَ ٱللَّهُ نَصۡرًا عَزِيزًا

Akunusuru juu ya maadui wako na Akuongoze njia ya Dini iliyonyooka na Allah Mtukufu Akunusuru nusra yenye nguvu kwa namna ambayo Uislamu hautakuwa mnyonge. info
التفاسير: |

4 : 48

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ ٱلسَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ لِيَزۡدَادُوٓاْ إِيمَٰنٗا مَّعَ إِيمَٰنِهِمۡۗ وَلِلَّهِ جُنُودُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Yeye Ndiye Allah Mtukufu Aliyeteremsha utulivu ndani ya nyoyo za wenye kuamini katika siku ya (Ḥudaybiyah), zikatulia, na yakini ikajikita ndani ya hizo nyoyo, ili wazidi kumuamini Allah Mtukufu na kumfuata Mtume Wake. Na Allah Mtukufu, (Aliyetakasika na kutukuka), Ana askari wa mbinguni na ardhini, Anawanusuru kwa askari hao waja Wake Waumini. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi sana wa maslahi ya viumbe Vyake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo Wake na utengenezaji Wake. info
التفاسير: |

5 : 48

لِّيُدۡخِلَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنۡهُمۡ سَيِّـَٔاتِهِمۡۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِندَ ٱللَّهِ فَوۡزًا عَظِيمٗا

Apate kuwaingiza Waumini wa kiume na Waumini wa kike kwenye mabustani ya Peponi ambayo mito inapita chini ya miti yake na majumba yake ya fahari, hali ya kukaa humo milele, na Awafutie kila baya walilolifanya asiwaadhibu kwalo. Malipo hayo kwa Allah Mtukufu ndio kuokoka na kila kero na ndio kupata kila linalotafutwa. info
التفاسير: |

6 : 48

وَيُعَذِّبَ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ وَٱلۡمُشۡرِكَٰتِ ٱلظَّآنِّينَ بِٱللَّهِ ظَنَّ ٱلسَّوۡءِۚ عَلَيۡهِمۡ دَآئِرَةُ ٱلسَّوۡءِۖ وَغَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ وَلَعَنَهُمۡ وَأَعَدَّ لَهُمۡ جَهَنَّمَۖ وَسَآءَتۡ مَصِيرٗا

Na Apate kuwaadhibu wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike, na washirikina wa kiume na washirikina wa kike wanaomdhania Allah Mtukufu dhana mbaya, ya kuwa yeye Hatamnusuru Mtume na waliokuwa pamoja naye dhidi ya maadui wao, na kuwa Yeye Hataipa ushindi Dini Yake. Basi juu ya hao utazunguka mzunguko wa adhabu na kila kilicho kibaya kwao, na Amewaandalia moto wa Jahanamu; na mashukio mabaya ya mtu kuishia ni hayo. info
التفاسير: |

7 : 48

وَلِلَّهِ جُنُودُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمًا

Na Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Ana askari wa mbinguni na ardhini. Anawanusuru kwa askari hao waja Wake Waumini. Na Allah Mtukufu ni Mshindi Mwenye uwezo juu viumbe Vyake, ni Mwingi wa hekima katika kuendesha mambo yao. info
التفاسير: |

8 : 48

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ شَٰهِدٗا وَمُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا

Hakika sisi tumekutuma, ewe Mtume, uwe shahidi kwa umati wako juu ya ufikishaji ujumbe, uwabainishie kile ulichotumwa kwao, uwabashirie Pepo wanaokutii, na uwaonye na adhabu ya sasa na ya baadaye. info
التفاسير: |

9 : 48

لِّتُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَتُعَزِّرُوهُ وَتُوَقِّرُوهُۚ وَتُسَبِّحُوهُ بُكۡرَةٗ وَأَصِيلًا

Mpate kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, mumnusuru Allah Mtukufu kwa kuinusuru Dini Yake, mumtukuze na mumtakase mwanzo wa mchana na mwisho wake. info
التفاسير: |
prev

Al-Fath

next
:
0:00 0:00