prev

At-Tahrim

next

1 : 66

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَآ أَحَلَّ ٱللَّهُ لَكَۖ تَبۡتَغِي مَرۡضَاتَ أَزۡوَٰجِكَۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Ewe Mtume! kwanini unaizuia nafsi yako na halali Aliyokuhalalishia Allah Mtukufu kwa kutaka kuwaridhisha wake zako? Na Allah Mtukufu ni Mwenye kukusamehe, ni Mwenye huruma kwako. info
التفاسير: |

2 : 66

قَدۡ فَرَضَ ٱللَّهُ لَكُمۡ تَحِلَّةَ أَيۡمَٰنِكُمۡۚ وَٱللَّهُ مَوۡلَىٰكُمۡۖ وَهُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ

Kwa hakika Amepasisha Allah Mtukufu kwenu, (enyi Waumini), kuvihalalisha viapo vyenu kwa kuvitolea kafara. Kafara yenyewe ni kuwalisha masikini kumi au kuwavisha au kuacha mtumwa huru. Na asiyepata cha kutoa, basi afunge siku tatu. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuwanusuru nyinyi na kuyasimamia mambo yenu. Na Yeye Ndiye Mjuzi wa mambo yanayowafaa Akayapitisha kwenu, Ndiye Mwingi wa hekima kwenye maneno Yake na matendo Yake. info
التفاسير: |

3 : 66

وَإِذۡ أَسَرَّ ٱلنَّبِيُّ إِلَىٰ بَعۡضِ أَزۡوَٰجِهِۦ حَدِيثٗا فَلَمَّا نَبَّأَتۡ بِهِۦ وَأَظۡهَرَهُ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ عَرَّفَ بَعۡضَهُۥ وَأَعۡرَضَ عَنۢ بَعۡضٖۖ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِۦ قَالَتۡ مَنۡ أَنۢبَأَكَ هَٰذَاۖ قَالَ نَبَّأَنِيَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡخَبِيرُ

Na pindi Mtume alipompa siri mke wake Hafṣah, (radhi za Allah Mtukufu zimshukie), ya mazungumzo fulani, na yeye alipomwambia maneno hayo mke mwenzake ‛Ᾱishah, radhi za Allah Mtukufu zimshukie, na Allah Mtukufu Akamjulisha Mtume Wake kuwa mkewe ameitoa siri yake, alimjulisha Hafṣah sehemu ya maneno aliyoyatoa na akayanyamazia mengine asimwambie kwa kuchunga heshima. Basi Mtume alipomwambia Hafṣah yale mazungumzo aliyoyatangaza, alisema hafsah, «Ni nani aliyekwambia maneno hayo?» Akasema Mtume, «Aliyeniambia hayo ni Allah Mtukufu, Aliye Mwingi wa ujuzi na utambuzi, Ambaye hakifichiki Kwake chenye kujificha chochote». info
التفاسير: |

4 : 66

إِن تَتُوبَآ إِلَى ٱللَّهِ فَقَدۡ صَغَتۡ قُلُوبُكُمَاۖ وَإِن تَظَٰهَرَا عَلَيۡهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ مَوۡلَىٰهُ وَجِبۡرِيلُ وَصَٰلِحُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۖ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ بَعۡدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ

Iwapo mtarudi kwa Allah Mtukufu (ewe Ḥafṣah na ‛Ᾱishah) basi yatakuwa yamepatikana kwenu yanayopelekea kukubaliwa toba yenu, kwa kuwa nyoyo zenu zilielekea kwenye kuyapenda yale aliyoyachukia Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ya kutoa siri yake. Na mtakaposaidiana kuwa dhidi yake kwa kufanya yanayomuudhi, basi Allah Mtukufu Ndiye Msimamizi wake na Mtetezi wake na Jibrili na Waumini wema. Na Malaika, baada ya usaidizi wa Allah Mtukufu, ni wasaidizi wake na watetezi wake dhidi ya yoyote anayemuudhi na kumfanyia uadui. info
التفاسير: |

5 : 66

عَسَىٰ رَبُّهُۥٓ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبۡدِلَهُۥٓ أَزۡوَٰجًا خَيۡرٗا مِّنكُنَّ مُسۡلِمَٰتٖ مُّؤۡمِنَٰتٖ قَٰنِتَٰتٖ تَٰٓئِبَٰتٍ عَٰبِدَٰتٖ سَٰٓئِحَٰتٖ ثَيِّبَٰتٖ وَأَبۡكَارٗا

Linalotarajiwa kwa Mola wake iwapo atawaacha nyinyi, (enyi wake zake), ni amuoze, badala yenu, wake wanyenyekevu kwa Allah Mtukufu, wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, wenye kumtii Allah Mtukufu, wenye kurudi kwenye yale anayoyapenda Allah Mtukufu ya kumtii, wenye kumuabudu kwa wingi, wenye kufunga sana, wakiwa wake wakuu miongoni mwao na wanawali. info
التفاسير: |

6 : 66

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ قُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ وَأَهۡلِيكُمۡ نَارٗا وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلۡحِجَارَةُ عَلَيۡهَا مَلَٰٓئِكَةٌ غِلَاظٞ شِدَادٞ لَّا يَعۡصُونَ ٱللَّهَ مَآ أَمَرَهُمۡ وَيَفۡعَلُونَ مَا يُؤۡمَرُونَ

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Zilindeni nafsi zenu kwa kuyatenda yale ambayo Amewaamrisha kwayo Allah Mtukufu na kuyaepuka yale ambayo Amewakataza nayo, na walindeni watu wenu kwa kile mnachotumia kujilinda nyinyi wenyewe na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Watasimamia kuadhibiwa watu wa Motoni Malaika wenye nguvu walio thabiti katika usimamizi wao, wasioenda kinyume na Allah Mtukufu katika maamrisho Yake, na wanaotekeleza yale wanayoamrishwa nayo. info
التفاسير: |

7 : 66

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَا تَعۡتَذِرُواْ ٱلۡيَوۡمَۖ إِنَّمَا تُجۡزَوۡنَ مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Na wataambiwa wale waliokanusha kwamba Allah Mtukufu Ndiye Mola wa haki na wakamkufuru, watakapoingizwa Motoni, «Msitafute nyudhuru Siku ya Leo, ukweli ni kwamba nyinyi mnapewa malipo ya yale ambayo mlikuwa mkiyafanya duniani». info
التفاسير: |
prev

At-Tahrim

next
:
0:00 0:00