Check out the new design

அல்குர்ஆன் மொழிபெயர்ப்பு - சுவாஹிலி மொழிபெயர்ப்பு- அலி முஃசின் bபிர்வானி * - மொழிபெயர்ப்பு அட்டவணை

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

மொழிபெயர்ப்பு அத்தியாயம்: அல்முஸ்ஸம்மில்   வசனம்:

Al-Muzzammil

يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمُزَّمِّلُ
Ewe uliye jifunika!
Ewe uliye jigubika kwa nguo zako!
அரபு விரிவுரைகள்:
قُمِ ٱلَّيۡلَ إِلَّا قَلِيلٗا
Kesha usiku kucha, ila kidogo tu!
Inuka kwa ajili ya Swala usiku kucha, ila kidogo tu!
அரபு விரிவுரைகள்:
نِّصۡفَهُۥٓ أَوِ ٱنقُصۡ مِنۡهُ قَلِيلًا
Nusu yake, au ipunguze kidogo.
Simama nusu ya usiku, au punguza kidogo katika hiyo nusu mpaka ifikie thuluthi,
அரபு விரிவுரைகள்:
أَوۡ زِدۡ عَلَيۡهِ وَرَتِّلِ ٱلۡقُرۡءَانَ تَرۡتِيلًا
Au izidishe - na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo.
Au zidisha kwenye nusu mpaka ifikie thuluthi mbili. Na soma Qur'ani kwa pole pole ukibainisha harufi, na pa kusita usite, pasiwe na nuksani yoyote.
அரபு விரிவுரைகள்:
إِنَّا سَنُلۡقِي عَلَيۡكَ قَوۡلٗا ثَقِيلًا
ka Hakika Sisi tutakuteremshia uli nzito.
Ewe Mtume! Hakika Sisi tutakuteremshia Qur'ani yenye kukusanya amri, na makatazo, na takalifu nzito nzito.
அரபு விரிவுரைகள்:
إِنَّ نَاشِئَةَ ٱلَّيۡلِ هِيَ أَشَدُّ وَطۡـٔٗا وَأَقۡوَمُ قِيلًا
Hakika kuamka usiku kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno yake yanatua zaidi.
Hakika ibada zinazo fanywa usiku zinaganda zaidi katika moyo wa mtu, na zinabainika zaidi ulimini, na zinasibu vyema zaidi, kuliko visomo vya ibada za mchana.
அரபு விரிவுரைகள்:
إِنَّ لَكَ فِي ٱلنَّهَارِ سَبۡحٗا طَوِيلٗا
Kwani hakika mchana una shughuli nyingi.
Hakika mchana unakuwa na mambo mengi ya kukuhangaisha kutafuta maslaha ya maisha yako, na kushughulika na mambo ya kufikisha Ujumbe. Basi jiwekee nafsi yako faragha ya usiku kwa ajili ya kumuabudu Mola wako Mlezi.
அரபு விரிவுரைகள்:
وَٱذۡكُرِ ٱسۡمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلۡ إِلَيۡهِ تَبۡتِيلٗا
Na lidhukuru jina la Mola wako Mlezi, na ujitolee kwake kwa ukamilifu.
Na pitisha ulimini mwako kudhukuru jina la Mola aliye kuumba na kukulea, na mkhusishe Yeye tu kwa ibada kwa ukamilifu.
அரபு விரிவுரைகள்:
رَّبُّ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَٱتَّخِذۡهُ وَكِيلٗا
Mola Mlezi wa mashariki na magharibi, hapana mungu isipo kuwa Yeye, basi mfanye kuwa Mtegemewa wako.
Yeye ndiye Mwenye kumiliki mashariki na magharibi, hapana wa kuabudiwa kwa haki isipo kuwa Yeye. Basi mfanye Yeye tu ndiye wa kukutosha katika mambo yako yote, ndiye wa kutegemewa peke yake kama alivyo ahidi.
அரபு விரிவுரைகள்:
وَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱهۡجُرۡهُمۡ هَجۡرٗا جَمِيلٗا
Na vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kwa vizuri.
Na vumilia upuuzi wanao usema, na jitenge nao kwa moyo wako, na nenda kinyume na vitendo vyao, pamoja na kuwapuuza, na kuacha kujilipizia.
அரபு விரிவுரைகள்:
وَذَرۡنِي وَٱلۡمُكَذِّبِينَ أُوْلِي ٱلنَّعۡمَةِ وَمَهِّلۡهُمۡ قَلِيلًا
Na niache Mimi na hao wanao kanusha, walio neemeka; na wape muhula kidogo!
Niachilie Mimi hao wanao kadhibisha, wenye kuneemeshwa, na uwape muhula muda mfupi.
அரபு விரிவுரைகள்:
إِنَّ لَدَيۡنَآ أَنكَالٗا وَجَحِيمٗا
Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unao waka kwa ukali kabisa!
Huko Akhera tumewawekea wanao kadhibisha pingu nzito, na Moto wa kuunguza,
அரபு விரிவுரைகள்:
وَطَعَامٗا ذَا غُصَّةٖ وَعَذَابًا أَلِيمٗا
Na chakula kinacho kwama kooni, na adhabu inayo umiza.
Na chakula kinacho sakama kooni, hakimezeki, na adhabu yenye uchungu mkali usio stahamilika.
அரபு விரிவுரைகள்:
يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ وَكَانَتِ ٱلۡجِبَالُ كَثِيبٗا مَّهِيلًا
Siku ambayo ardhi itatikiswa na milima pia, na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga.
Siku itakapo tikisika ardhi na milima kwa mtikiso mkubwa mno, na milima ikawa mirundu ya mchanga ulio tapanyika, baada ya kuwa mawe magumu yaliyo shikamana.
அரபு விரிவுரைகள்:
إِنَّآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡكُمۡ رَسُولٗا شَٰهِدًا عَلَيۡكُمۡ كَمَآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ رَسُولٗا
Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu, kama tulivyo mtuma Mtume kwa Firauni.
Enyi watu wa Makka! Hakika Sisi tumekutumieni Muhammad kuwa ni Mtume wa kukushuhudilieni Siku ya Kiyama kwa kukubali na kukataa, kama tulivyo mtuma Musa kwa Firauni awe ni Mtume.
அரபு விரிவுரைகள்:
فَعَصَىٰ فِرۡعَوۡنُ ٱلرَّسُولَ فَأَخَذۡنَٰهُ أَخۡذٗا وَبِيلٗا
Lakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamshika mshiko wa mateso.
Firauni akamkataa huyo Mtume, basi tukamshika kwa mshiko wa nguvu!
அரபு விரிவுரைகள்:
فَكَيۡفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرۡتُمۡ يَوۡمٗا يَجۡعَلُ ٱلۡوِلۡدَٰنَ شِيبًا
Basi nyinyi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo itawafanya watoto wadogo waote mvi?
Basi mkikufuru mtajikinga vipi na adhabu ya Siku ambayo kwa kitisho chake itawafanya vijana wawe vikongwe wasio na nguvu?
அரபு விரிவுரைகள்:
ٱلسَّمَآءُ مُنفَطِرُۢ بِهِۦۚ كَانَ وَعۡدُهُۥ مَفۡعُولًا
Hapo mbingu zitapasuka! Ahadi yake itakuwa imetekelezwa.
Mbingu juu ya nguvu zake na ukubwa wake, Siku hiyo zitapasukilia mbali kwa shida zake na vitisho vyake. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni lazima itokee, hapana hivi wala hivi.
அரபு விரிவுரைகள்:
إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذۡكِرَةٞۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا
Kwa hakika hili ni kumbusho. Mwenye kutaka atashika njia ya kwendea kwa Mola wake Mlezi.
Hakika Aya hizi zinazo taja ahadi ya Mwenyezi Mungu ni mawaidha. Kwa hivyo mwenye kutaka kunafiika kwazo ataishika njia ya kumwendea Mola wake Mlezi kwa kuchamngu na kunyenyekea.
அரபு விரிவுரைகள்:
 
மொழிபெயர்ப்பு அத்தியாயம்: அல்முஸ்ஸம்மில்
அத்தியாயங்களின் அட்டவணை பக்க எண்
 
அல்குர்ஆன் மொழிபெயர்ப்பு - சுவாஹிலி மொழிபெயர்ப்பு- அலி முஃசின் bபிர்வானி - மொழிபெயர்ப்பு அட்டவணை

அலீ முஹ்ஸின் அல் பர்வானி மூலம் மொழிபெயர்க்கப்பட்டது.

மூடுக