Check out the new design

แปล​ความหมาย​อัลกุรอาน​ - คำแปลภาษาสวาฮิลี - อับดุลลอฮ์ มุฮัมมัด และ นาศิร เคาะมีส * - สารบัญ​คำแปล


แปลความหมาย​ สูเราะฮ์: Hūd   อายะฮ์:
وَيَٰقَوۡمِ لَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مَالًاۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِۚ وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْۚ إِنَّهُم مُّلَٰقُواْ رَبِّهِمۡ وَلَٰكِنِّيٓ أَرَىٰكُمۡ قَوۡمٗا تَجۡهَلُونَ
Nūḥ, amani imshukiye, akaendelea kuwaambia watu wake, «Enyi watu wangu, siwaombi kwa kuwaita nyinyi kumpwekesha Mwenyezi Mungu, munipatie mali baada ya kuamini kwenu, kwani malipo ya ushauri wangu kwenu yako kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na si shughuli yangu mimi kuwafukuza Waumini, kwani wao ni wenye kukutana na Mola wao Siku ya Kiyama. Lakini mimi nawaona nyinyi kuwa ni watu msiojua, kwa kuwa mnaniamrisha niwafukuze vipenzi vya Mwenyezi Mungu na niwaepushe na mimi.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَيَٰقَوۡمِ مَن يَنصُرُنِي مِنَ ٱللَّهِ إِن طَرَدتُّهُمۡۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
«Na enyi watu wangu, ni nani mwenye kunizuia mimi na Mwenyezi Mungu Akinitesa kwa kuwafukuza kwangu Waumini? Kwani hamyazingatii mambo mkayajua yenye nafuu zaidi kwenu na yenye kufaa zaidi?
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَلَآ أَقُولُ لَكُمۡ عِندِي خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ وَلَآ أَقُولُ إِنِّي مَلَكٞ وَلَآ أَقُولُ لِلَّذِينَ تَزۡدَرِيٓ أَعۡيُنُكُمۡ لَن يُؤۡتِيَهُمُ ٱللَّهُ خَيۡرًاۖ ٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا فِيٓ أَنفُسِهِمۡ إِنِّيٓ إِذٗا لَّمِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ
«Na wala siwaambii nyinyi kuwa mimi nina mahazina ya Mwenyezi Mungu, wala mimi siyajui yasiyoonekana, na mimi si mmoja kati ya Malaika, wala siwaambii hawa mnaowadharau miongoni mwa madhaifu wa Waumini kwamba Mwenyezi Mungu hatawapa malipo mema ya matendo yao. Mwenyezi Mungu, Peke Yake, ni Mjuzi kabisa kwa yaliyomo ndani ya vifua vyao na nyoyo zao. Na nikifanya hivyo, basi mimi wakati huo nitakuwa ni miongoni mwa wale wenye kujidhulumu wao wenyewe na kuwadhulumu wengineo»
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قَالُواْ يَٰنُوحُ قَدۡ جَٰدَلۡتَنَا فَأَكۡثَرۡتَ جِدَٰلَنَا فَأۡتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Wakasema, «Ewe Nūḥ„ umelumbana na sisi na umezidisha katika malumbano yako kwetu, basi tuletee hiyo adhabu unayotuahidi, iwapo wewe ni miongoni mwa wakweli katika madai yako.»
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قَالَ إِنَّمَا يَأۡتِيكُم بِهِ ٱللَّهُ إِن شَآءَ وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ
Nūḥ, akasema kuwaambia watu wake, «Mwenyezi Mungu , Peke Yake, Ndiye Atakayewaletea nyinyi adhabu atakapo, na nyinyi si wenye kuiponyoka Akitaka kuwaadhibu, kwani Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, hakuna chochote chenye kumlemea katika ardhi wala katika mbingu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَلَا يَنفَعُكُمۡ نُصۡحِيٓ إِنۡ أَرَدتُّ أَنۡ أَنصَحَ لَكُمۡ إِن كَانَ ٱللَّهُ يُرِيدُ أَن يُغۡوِيَكُمۡۚ هُوَ رَبُّكُمۡ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
«Na hautawanufaisha nyinyi ushauri wangu na bidii yangu katika kuwalingania kwenye Imani, iwapo Mwenyezi Mungu Anataka kuwpoteza na kuwaangamiza. Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye mwenye kuwamiliki, na Kwake Yeye mtarejeshwa kesho Akhera kwa kuhesabiwa na kulipwa.»
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ إِنِ ٱفۡتَرَيۡتُهُۥ فَعَلَيَّ إِجۡرَامِي وَأَنَا۠ بَرِيٓءٞ مِّمَّا تُجۡرِمُونَ
Au je, wanasema hawa washirikina miongoni mwa watu wa Nūḥ, kwamba Nūḥ, amezua neno hili? Waambie, «Nikiwa nimemzulia urongo Mwenyezi Mungu hilo, basi ni juu yangu mimi, peke yangu, dhambi ya hilo; na nikiwa ni mkweli, basi nyinyi ndio wahalifu wenye dhambi, na mimi niko mbali na ukfiri wenu, ukanushaji wenu uhalifu wenu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَأُوحِيَ إِلَىٰ نُوحٍ أَنَّهُۥ لَن يُؤۡمِنَ مِن قَوۡمِكَ إِلَّا مَن قَدۡ ءَامَنَ فَلَا تَبۡتَئِسۡ بِمَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ
Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na sifa za upungufu na kutukuka, Alimletea wahyi Nūḥ„ amani imshukiye, ilipolazimika adhabu juu ya watu wake kwamba hawatamuamini Mwenyezi Mungu isipokuwa walioamini kabla ya hapo, «basi usisikitike, ewe Nūḥ„ juu ya yale waliokuwa wakiyafanaya.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَٱصۡنَعِ ٱلۡفُلۡكَ بِأَعۡيُنِنَا وَوَحۡيِنَا وَلَا تُخَٰطِبۡنِي فِي ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ إِنَّهُم مُّغۡرَقُونَ
«Na utengeneze jahazi kwa maangalizi yetu na kwa amri yetu na msaada wetu, hali ya kuwa wewe uko kwenye utunzi wetu na hifadhi yetu, na usitake kwangu kuwapa muhula hawa waliojidhulumu nafsi zao, miongoni mwa watu wako, kwa ukafiri wao, kwani wao ni wenye kuzamishwa kwa mafuriko.» Katika hii aya pana kuthibitisha sifa ya 'ayn (jicho ) kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa namna inavyonasibiana na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
 
แปลความหมาย​ สูเราะฮ์: Hūd
สารบัญสูเราะฮ์ หมายเลข​หน้า​
 
แปล​ความหมาย​อัลกุรอาน​ - คำแปลภาษาสวาฮิลี - อับดุลลอฮ์ มุฮัมมัด และ นาศิร เคาะมีส - สารบัญ​คำแปล

แปลโดย ดร.อับดุลลอฮ์ มุฮัมมัด อบูบักร์ และ ชัยค์ นาศิร เคาะมีส

ปิด