Check out the new design

แปล​ความหมาย​อัลกุรอาน​ - คำแปลภาษาสวาฮิลี - อับดุลลอฮ์ มุฮัมมัด และ นาศิร เคาะมีส * - สารบัญ​คำแปล


แปลความหมาย​ สูเราะฮ์: Al-A‘rāf   อายะฮ์:
حَقِيقٌ عَلَىٰٓ أَن لَّآ أَقُولَ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ قَدۡ جِئۡتُكُم بِبَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ فَأَرۡسِلۡ مَعِيَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ
«Nastahili nisiseme kuhusu Mwenyezi Mungu isipokuwa ukweli na inapasa kwangu nijilazimishe nayo. Nimewajia na dalili na hoja zenye ushindi kutoka kwa Mola wenu juu ya ukweli wa yale ninayowatajia. Basi waachilie, ewe Fir'awn, Wana wa Isrāīl pamoja na mimi kutoka kwenye kifungo chako na ukandamizaji wako, na wape uhuru wa kumuabudu Mwenyezi Mungu.»
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قَالَ إِن كُنتَ جِئۡتَ بِـَٔايَةٖ فَأۡتِ بِهَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Fir'awn alisema kumwambia Mūsā, «Ukiwa umekuja na alama, kama unavyodai, basi niletee na uihudhurishe mbele yangu, ili madai yako yawe ya sawa na ukweli wako uthibiti, iwapo wewe ni mkweli katika madai yako kuwa wewe ni mjumbe wa Mola wa viumbe.»
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعۡبَانٞ مُّبِينٞ
Hapo Mūsā aliitupa fimbo yake na ikageuka nyoka mkubwa anayeonekana waziwazi.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِيَ بَيۡضَآءُ لِلنَّٰظِرِينَ
Na akauvuta mkono wake kutoka kwenye uwazi wa kanzu iliyofunguliwa kifuani au chini ya kapwa lake, na papo hapo ukawa mweupe kama maziwa usio na mbalanga, ukiwa ni alama kwa Fir'awn; akiurejesha unarudi rangi yake ya mwanzo, kama ulivyo mwili wake.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٌ عَلِيمٞ
Watukufu wa watu wa Fir'awn walisema, «Hakika Mūsā ni mchawi, anayatawala macho ya watu kwa kuwadanganya mpaka ikawaingia kwenye fikira zao kuwa fimbo ni nyoka, na kukiona kitu kinyume na vile kilivyo, na yeye ana ujuzi mwingi wa uchawi na ana uhodari nao.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
يُرِيدُ أَن يُخۡرِجَكُم مِّنۡ أَرۡضِكُمۡۖ فَمَاذَا تَأۡمُرُونَ
«Yuwataka kuwatoa nyinyi nyote kwenye nchi yenu.» Fir'awn akasema, «Mnanipa shauri gani, enyi watu watukufu, juu ya mambo ya Mūsā?»
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قَالُوٓاْ أَرۡجِهۡ وَأَخَاهُ وَأَرۡسِلۡ فِي ٱلۡمَدَآئِنِ حَٰشِرِينَ
Wakasema waliohudhuria mjadala wa Mūsā miongoni mwa mabwana wa watu wa Fir’awn na wakubwa wao, «Mfanye Mūsā na Hārūn wangojee, na upeleke askari kwenye miji ya Misri na majimbo yake.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
يَأۡتُوكَ بِكُلِّ سَٰحِرٍ عَلِيمٖ
«Ili wakukusanyie kila mchawi mwenye ujuzi mwingi wa uchawi.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَجَآءَ ٱلسَّحَرَةُ فِرۡعَوۡنَ قَالُوٓاْ إِنَّ لَنَا لَأَجۡرًا إِن كُنَّا نَحۡنُ ٱلۡغَٰلِبِينَ
Wachawi wakamjia Fir'awn wakasema, «Je, tutakuwa na zawadi na mali tukimshinda Mūsā?»
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قَالَ نَعَمۡ وَإِنَّكُمۡ لَمِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ
Fir'awn akasema, «Ndio, mtakuwa na malipo na ukaribu na mimi mkimshinda.»
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِمَّآ أَن تُلۡقِيَ وَإِمَّآ أَن نَّكُونَ نَحۡنُ ٱلۡمُلۡقِينَ
Wakasema wachawi wa Fir'awn kumwambia Mūsā, kwa njia ya kujiona na kutojali. «Ewe Mūsā, chaguwa uwe ni wa mwanzo kutupa fimbo yako au tuwe sisi ni wa mwanzo kutupa.»
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قَالَ أَلۡقُواْۖ فَلَمَّآ أَلۡقَوۡاْ سَحَرُوٓاْ أَعۡيُنَ ٱلنَّاسِ وَٱسۡتَرۡهَبُوهُمۡ وَجَآءُو بِسِحۡرٍ عَظِيمٖ
Akasema Mūsā kuwaambia wachawi, «Tupeni nyinyi.» Walipotupa kamba na fimbo, waliyaroga macho ya watu yakaona kwamba yale waliyoyafanya ni ya kweli, na hali yalikuwa ni kiinimacho na vitu vya kudhania, na waliwatisha watu vitisho vikali na walikuja na uchawi wa nguvu ulio mwingi.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
۞ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَلۡقِ عَصَاكَۖ فَإِذَا هِيَ تَلۡقَفُ مَا يَأۡفِكُونَ
Hapo Mwenyezi Mungu Alimletea wahyi mja Wake na Mtume Wake Mūsā, amani imshukiye, katika kisimamo hicho kikubwa ambacho hapo Mwenyezi Mungu Alipambanua baina ya ukweli na urongo, akimuamuru akitupe kilichoko kwenye mkono wake wa kulia, nacho ni fimbo yake. Akaitupa na papo hapo ikawa inavimeza vile wanavyovitupa na kuwafanya watu wadhanie kuwa ni vya kweli na ilhali ni vya urongo.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
فَوَقَعَ ٱلۡحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Hapo haki ikajitokeza na ikafunuka kwa aliyehudhuria na kuiona kuhusu mambo ya Mūsā, amani imshukie, na kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, analingania haki, na ukabatilika urongo waliokuwa wakiufanya.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
فَغُلِبُواْ هُنَالِكَ وَٱنقَلَبُواْ صَٰغِرِينَ
Wakashindwa wachawi wote katika mahala walipokusanyika, na akaondoka Fir'awn na watu wake wakiwa wanyonge, waliozidiwa nguvu na kushindwa.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَأُلۡقِيَ ٱلسَّحَرَةُ سَٰجِدِينَ
Wakapomoka wachawi kwa nyuso zao kwa kumsujudia Mola wa viumbe wote, kwa uwezo mkubwa wa Mwenyezi Mungu waliouona.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
 
แปลความหมาย​ สูเราะฮ์: Al-A‘rāf
สารบัญสูเราะฮ์ หมายเลข​หน้า​
 
แปล​ความหมาย​อัลกุรอาน​ - คำแปลภาษาสวาฮิลี - อับดุลลอฮ์ มุฮัมมัด และ นาศิร เคาะมีส - สารบัญ​คำแปล

แปลโดย ดร.อับดุลลอฮ์ มุฮัมมัด อบูบักร์ และ ชัยค์ นาศิร เคาะมีส

ปิด