Mwenyezi Mungu anaapa kwa Qur'ani yenye kuweka wazi Dini ya Haki, yenye kuwabainishia watu yaliyo na maslaha ya dunia yao na Akhera yao, ili kujuulisha utukufu wa cheo chake.
Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji.
Hakika Sisi tumeanza kuiteremsha Qur'ani katika usiku ulio jaa kheri, wenye baraka nyingi, kwani ni mwendo wetu kuonya kwa kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu.
Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima!
Katika usiku huu wenye baraka hupambanuliwa baina ya mambo yote yenye hikima, na Qur'ani ndio kilele cha hikima, na ndio pambanuo baina ya kweli na uwongo. Na kwa hivyo ndio ikateremshwa katika usiku huo.
Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma.
Nakusudia kwa jambo hili, yaani jambo kuu lenye kutoka kwetu kama ilivyo kwisha pita hukumu ya mpango wetu. Kwani ni shani yetu kutuma Mitume kwa Vitabu ili kuwafikishia waja wetu.
Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.
Kwa ajili ya rehema ya Mola wako Mlezi kwa waja wake, amewatuma Mitume kwa watu wawafikishie uwongofu wake, kwani hakika Yeye peke yake, ndiye Mwenye kusikia kila cha kusikiwa, Mwenye kujua kila cha kujuulikana.
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini.
Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini na haki, na mnaifuata, na mnaamini kuwa hakika ndio Yeye Mwenye kuteremsha Qur'ani kuwa ni rehema na uwongofu.
Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo.
Hapana Mungu isipo kuwa Yeye anaye stahiki kuabudiwa, Yeye peke yake, Mwenye kuhuisha na kufisha. Na Yeye peke yake, ndiye aliye kuumbeni nyinyi na kawaumba baba zenu wa mwanzo.
Lakini makafiri wana shaka na ukweli huu, wamo wakifuata pumbao lao. Na huo ndio mtindo wa watu wa pumbao na michezo, sio mwendo wa watu wa ilimu na yakini.
Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri,
Basi ewe Mtume! Ngojea ukame utapo wateremkia, wakasibiwa na kukonda na udhaifu wa kuona, ikawa mtu huwa anaona baina ya mbingu na ardhi moshi dhaahiri shaahiri, akawa anasikia mvumo wake wala hauoni.
Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha.
Watu hawa watawaidhika vipi, hata watimize hiyo Imani wanayo iahidi wakiondolewa adhabu, na hali Mtume mwenye ujumbe ulio wazi kesha wajia na miujiza yenye kuonyesha ukweli wake, na hayo ndiyo mawaidha makubwa kabisa?
Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu.
Kisha wakaacha kumsadiki Mtume aliye tiliwa nguvu na miujiza iliyo wazi, na wakamwambia: Huo uwongo na uzushi! Mara nyengine wakimsingizia kuwa amefunzwa hayo na mtu, na mara nyengine kuwa akili yake imekorogeka.
Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile!
Mwenyezi Mungu anawarudi: Sisi hakika tutakuondoleeni adhabu wakati wa duniani, nao ni wakati mchache, lakini nyinyi mtarejea tu, bila ya shaka, yale yale mliyo kuwa mkiyatenda.
Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu.
Na bila ya shaka tulikwisha wafanyia mtihani, kabla ya makafiri wa Makka, kaumu ya Firauni kwa kuwaitia kwenye Imani, na akawajia Musa, Mtume Mtukufu kwa Mwenyezi Mungu. Wakamkataa kwa inda tu. Na huo ndio mtindo wa hawa washirikina.
Akasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu.
Mtume Mtukufu aliwaambia: Nipeni enyi waja wa Mwenyezi Mungu lilio waajibu juu yenu, nalo ni kuitikia wito wangu, kwani mimi ni Mtume nimetumwa makhsusi kwenu, na ni muaminifu katika ujumbe wangu.
Wala msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu kwa kumkadhibisha Mtume wake, kwani mimi nakuleteeni muujiza ulio wazi wa kubainisha ukweli wa Unabii wangu na Utume wangu.
Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu.
Musa akamwambia Mola wake Mlezi kwa kumshitakia watu wake alipo kata tamaa nao kuwa hawaamini: Hakika watu hawa shauri yao imekwisha fika ukomo katika ukafiri; basi Wewe wafanyie wanalo stahiki.
Mwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa.
(Naye Musa akaambiwa:) Toka na Waumini usiku usiku kwa kificho, wasije kukupateni, kwani Firauni na askari wake watakufuateni pindi wakijua, wakukamateni.
Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe.
Mfano wa adhabu hiyo Mwenyezi Mungu humuadhibu mwenye kwenda kinyume na amri yake, na akatoka katika ut'iifu wake, na humwondolea neema yule mwenye nayo akawapa watu wenginewe wasio kuwa na makhusiano nao yoyote, la ya ujamaa wala dini.
La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula.
Basi la mbingu wala ardhi hazikuwahuzunukia ilipo wanyakua adhabu, jinsi ilivyo haribika hali yao; wala hawakungojewa watubu, wala hawakupewa muhula wapate kudiriki taksiri yao, kwa jinsi walivyo dharauliwa!
Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe.
Ninaapa: Tuliwakhiari Wana wa Israili kwa kuwa tuliwajua kwamba wao wana stahiki kuteuliwa kuliko watu wengine wote wa zama zao. Kwa hivyo tukawatuma miongoni mwao Manabii wengi kwa kuwa tulijua hali zao.
Hakika hawa wanao kadhibisha kufufuliwa bila ya shaka wanasema: Hapana kufa ila kwa haya haya mauti yetu ya kwanza ya duniani, wala sisi hatutafufuliwa tena.
Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi.
Hakika hawa wanao kadhibisha kufufuliwa bila ya shaka wanasema: Hapana kufa ila kwa haya haya mauti yetu ya kwanza ya duniani, wala sisi hatutafufuliwa tena.
Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.
Na wao humwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu na Waumini: Ikiwa nyinyi mnasema kweli katika madai yenu kwamba Mola wenu Mlezi anahuisha wafu kwa ajili ya hisabu katika Akhera, basi upesi upesi tufufulieni baba zetu walio kwisha kufa, kwa kumwomba huyo Mola wenu Mlezi!
Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu.
Je! Makafiri wa Makka wanawashinda kaumu ya Tubbaa' na walio watangulia kwa nguvu, na ulinzi, na utawala, na mambo yote ya kidunia? Ewe Muhammad! Hao washirikina wa kaumu yako hawawashindi hao kwa nguvu, na hao Sisi tuliwateketeza katika dunia kwa ukafiri wao na madhambi yao. Basi nawawazingatie!
Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui.
Hatukuziumba hizo ila kwa umbo lilio ambatana na hikima, kwa nidhamu iliyo thibiti yenye kuonyesha ushahidi wa kuwepo Mwenyezi Mungu wa pekee, Mwenye uwezo. Lakini wengi wa hawa wameghafilika, wamo katika upofu, hawazioni dalili hizi.
Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.
Siku ambayo jamaa hawezi kumtetea jamaa yake, wala rafiki kumtetea rafiki yake kwa lolote, hata kwa uchache wa adhabu. Wala wao hawatanusuriwa nafsi zao mbele ya Mwenyezi Mungu.
Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
Lakini wale ambao Mwenyezi Mungu amewarehemu, miongoni mwa Waumini, Mwenyezi Mungu atawasamehe, na atawapa ruhusa ya uombezi waweze kuwaombea wenginewe. Hakika Yeye ndiye Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye kuwarehemu waja wake Waumini.
Ataambiwa kwa kejeli na maskhara: Onja hii adhabu kali, kwani ati wewe si ndiye mtukufu mwenye nguvu katika kaumu yako, ndiye mheshimiwa unavyo jiona mwenyewe!
Hakika hao ambao wamejikinga nafsi zao na maasi kwa kufuata ut'iifu wa Mwenyezi Mungu wapo pahala patukufu ambapo ndani yake wao wanajipatia amani kwa nafsi zao.
Katika mabustani watapo kuwa ndani yake wanastarehe, na chemchem za maji yanayo pita chini yao, kwa sababu ya kuwakirimu wao kwa kutukuza hizo neema zao.
Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu,
Huko Peponi hawataonja mauti baada ya mauti ya kwanza waliyo kwisha yaonja duniani ulipo kwisha muda wao wa kuishi, na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni.
Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
Kuhifadhiwa kwao na adhabu ni fadhila na hisani ya Muumba wako. Kuhifadhiwa huko na adhabu na kuingizwa kwao Peponi ndio hadi ya mwisho ya kufuzu kulio kukubwa.
Basi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka.
Basi hakika Sisi tumekufanyia wepesi kuisoma Qur'ani na kuifikisha kama ilivyo teremka kwa lugha yako, na lugha yao, ili wapate kuwaidhika, na waiamini, na watende kwa mujibu yaliomo ndani yake.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
ผลการค้นหา:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".