Check out the new design

แปล​ความหมาย​อัลกุรอาน​ - คำแปลภาษาสวาฮิลี - ศูนย์การแปลรุว๊าด * - สารบัญ​คำแปล


แปลความหมาย​ สูเราะฮ์: Al-‘Ankabūt   อายะฮ์:

Al-Ankabut

الٓمٓ
Alif Lam Mim.[1]
[1] Herufi hizi "Alif, Laam, Miim" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
أَحَسِبَ ٱلنَّاسُ أَن يُتۡرَكُوٓاْ أَن يَقُولُوٓاْ ءَامَنَّا وَهُمۡ لَا يُفۡتَنُونَ
Je, watu wanadhani kwamba wataachwa kwa kuwa wanasema, "Tumeamini." Nao wasijaribiwe?
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَلَقَدۡ فَتَنَّا ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ فَلَيَعۡلَمَنَّ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ صَدَقُواْ وَلَيَعۡلَمَنَّ ٱلۡكَٰذِبِينَ
Hakika tuliwajaribu waliokuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawajua wale walio wakweli na atawajua waongo.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
أَمۡ حَسِبَ ٱلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ أَن يَسۡبِقُونَاۚ سَآءَ مَا يَحۡكُمُونَ
Au wale wanaotenda maovu wanadhani kwamba watatushinda? Ni hukumu mbaya mno hiyo wanayohukumu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
مَن كَانَ يَرۡجُواْ لِقَآءَ ٱللَّهِ فَإِنَّ أَجَلَ ٱللَّهِ لَأٓتٖۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ
Mwenye kutaraji kukutana na Mwenyezi Mungu, basi hakika miadi ya Mwenyezi Mungu itafika bila ya shaka. Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua zaidi.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَمَن جَٰهَدَ فَإِنَّمَا يُجَٰهِدُ لِنَفۡسِهِۦٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَغَنِيٌّ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na anayefanya juhudi, basi bila ya shaka anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake. Hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa walimwengu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَنُكَفِّرَنَّ عَنۡهُمۡ سَيِّـَٔاتِهِمۡ وَلَنَجۡزِيَنَّهُمۡ أَحۡسَنَ ٱلَّذِي كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Na wale walioamini na wakatenda mema, kwa yakini tutawafutia makosa yao, na bila shaka tutawalipa bora ya waliyokuwa wakiyatenda.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَوَصَّيۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ بِوَٰلِدَيۡهِ حُسۡنٗاۖ وَإِن جَٰهَدَاكَ لِتُشۡرِكَ بِي مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٞ فَلَا تُطِعۡهُمَآۚ إِلَيَّ مَرۡجِعُكُمۡ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Na tumemuusia mwanadamu kuwafanyia wema wazazi wake. Na ikiwa watapambana nawe ili unishirikishe Mimi na yale usiyokuwa na elimu nayo, basi usiwatii. Kwangu Mimi ndiyo marejeo yenu, na nitawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَنُدۡخِلَنَّهُمۡ فِي ٱلصَّٰلِحِينَ
Na wale walioamini na wakatenda mema, bila ya shaka tutawatia miongoni mwa watu wema.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ فَإِذَآ أُوذِيَ فِي ٱللَّهِ جَعَلَ فِتۡنَةَ ٱلنَّاسِ كَعَذَابِ ٱللَّهِۖ وَلَئِن جَآءَ نَصۡرٞ مِّن رَّبِّكَ لَيَقُولُنَّ إِنَّا كُنَّا مَعَكُمۡۚ أَوَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِأَعۡلَمَ بِمَا فِي صُدُورِ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na katika watu yupo yule anayesema, "Tumemuamini Mwenyezi Mungu." Lakini anapopewa maudhi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, anayafanya mateso ya watu kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na inapokuja nusura kutoka kwa Mola wako Mlezi, kwa yakini husema, "Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi." Kwani Mwenyezi Mungu hayajui zaidi yaliyomo vifuani mwa walimwengu?
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَلَيَعۡلَمَنَّ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَلَيَعۡلَمَنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ
Na hapana shaka Mwenyezi Mungu atawajua wale walioamini, na atawajua wanafiki.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّبِعُواْ سَبِيلَنَا وَلۡنَحۡمِلۡ خَطَٰيَٰكُمۡ وَمَا هُم بِحَٰمِلِينَ مِنۡ خَطَٰيَٰهُم مِّن شَيۡءٍۖ إِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ
Na wale waliokufuru waliwaambia wale walioamini, "Fuateni njia yetu, nasi tutayabeba makosa yenu." Wala wao hawatabeba katika makosa yao chochote kile. Hakika hao ni waongo.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَلَيَحۡمِلُنَّ أَثۡقَالَهُمۡ وَأَثۡقَالٗا مَّعَ أَثۡقَالِهِمۡۖ وَلَيُسۡـَٔلُنَّ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ عَمَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ
Na hapana shaka wataibeba mizigo yao na mizigo mingine pamoja na mizigo yao. Na kwa yakini wataulizwa Siku ya Qiyama juu ya yale waliyokuwa wakiyazua.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ فَلَبِثَ فِيهِمۡ أَلۡفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمۡسِينَ عَامٗا فَأَخَذَهُمُ ٱلطُّوفَانُ وَهُمۡ ظَٰلِمُونَ
Na hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, na akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini. Basi tufani ikawachukua, nao ni madhalimu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
فَأَنجَيۡنَٰهُ وَأَصۡحَٰبَ ٱلسَّفِينَةِ وَجَعَلۡنَٰهَآ ءَايَةٗ لِّلۡعَٰلَمِينَ
Nasi tukamwokoa yeye na wenziwe wa katika safina, na tukaifanya kuwa ni Ishara kwa walimwengu wote.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَإِبۡرَٰهِيمَ إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱتَّقُوهُۖ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Na Ibrahim pale alipowaambia watu wake, "Muabuduni Mwenyezi Mungu, na mcheni Yeye. Hiyo ndiyo heri yenu, ikiwa nyinyi mnajua."
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
إِنَّمَا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَوۡثَٰنٗا وَتَخۡلُقُونَ إِفۡكًاۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَا يَمۡلِكُونَ لَكُمۡ رِزۡقٗا فَٱبۡتَغُواْ عِندَ ٱللَّهِ ٱلرِّزۡقَ وَٱعۡبُدُوهُ وَٱشۡكُرُواْ لَهُۥٓۖ إِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
Hakika nyinyi mnaabudu tu masanamu badala ya Mwenyezi Mungu, na mnazua uzushi. Hakika hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawawamilikii riziki yoyote. Basi tafuteni riziki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mumuabudu Yeye, na mumshukuru Yeye. Kwake Yeye ndiko mtarudishwa.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَإِن تُكَذِّبُواْ فَقَدۡ كَذَّبَ أُمَمٞ مِّن قَبۡلِكُمۡۖ وَمَا عَلَى ٱلرَّسُولِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ
Na mkikadhibisha, basi kaumu kadhaa wa kadhaa za kabla yenu zilikwisha kadhibisha. Na si juu ya Mtume isipokuwa kufikisha Ujumbe waziwazi."
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ كَيۡفَ يُبۡدِئُ ٱللَّهُ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥٓۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ
Je, wao hawaoni jinsi Mwenyezi Mungu anavyoanzisha uumbaji, na kisha akaurudisha tena. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قُلۡ سِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَٱنظُرُواْ كَيۡفَ بَدَأَ ٱلۡخَلۡقَۚ ثُمَّ ٱللَّهُ يُنشِئُ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأٓخِرَةَۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ
Sema, "Tembeeni katika ardhi na tazameni jinsi alivyoanzisha uumbaji; kisha Mwenyezi Mungu ndiye anayeumba umbo la baadaye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
يُعَذِّبُ مَن يَشَآءُ وَيَرۡحَمُ مَن يَشَآءُۖ وَإِلَيۡهِ تُقۡلَبُونَ
Humuadhibu amtakaye, na humrehemu amtakaye. Na kwake Yeye mtapelekwa.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِي ٱلسَّمَآءِۖ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٖ
Na nyinyi si wenye kushinda katika ardhi wala katika mbingu. Wala nyinyi hamna mlinzi wala msaidizi isipokuwa Mwenyezi Mungu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَلِقَآئِهِۦٓ أُوْلَٰٓئِكَ يَئِسُواْ مِن رَّحۡمَتِي وَأُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Na wale waliozikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu na kukutana naye, hao ndio waliokata tamaa na rehema yangu, na hao ndio wana adhabu chungu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوۡمِهِۦٓ إِلَّآ أَن قَالُواْ ٱقۡتُلُوهُ أَوۡ حَرِّقُوهُ فَأَنجَىٰهُ ٱللَّهُ مِنَ ٱلنَّارِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Basi haikuwa jawabu ya watu wake isipokuwa walisema, "Muueni au mchomeni moto!" Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamwokoa kutokana na moto huo. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanaoamini.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَقَالَ إِنَّمَا ٱتَّخَذۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ أَوۡثَٰنٗا مَّوَدَّةَ بَيۡنِكُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ ثُمَّ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يَكۡفُرُ بَعۡضُكُم بِبَعۡضٖ وَيَلۡعَنُ بَعۡضُكُم بَعۡضٗا وَمَأۡوَىٰكُمُ ٱلنَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّٰصِرِينَ
Na alisema, "Hakika nyinyi mmeyashika masanamu badala ya Mwenyezi Mungu kwa mapenzi yaliyo baina yenu katika uhai wa duniani. Kisha Siku ya Qiyama mtakataana nyinyi kwa nyinyi, na mtalaaniana nyinyi kwa nyinyi. Na makazi yenu ni Motoni. Wala hamtapata wa kukunusuru wowote."
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
۞ فَـَٔامَنَ لَهُۥ لُوطٞۘ وَقَالَ إِنِّي مُهَاجِرٌ إِلَىٰ رَبِّيٓۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Luti akamuamini, na akasema, "Hakika mimi nahamia kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima."
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَوَهَبۡنَا لَهُۥٓ إِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَجَعَلۡنَا فِي ذُرِّيَّتِهِ ٱلنُّبُوَّةَ وَٱلۡكِتَٰبَ وَءَاتَيۡنَٰهُ أَجۡرَهُۥ فِي ٱلدُّنۡيَاۖ وَإِنَّهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ لَمِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ
Na tulimtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaa'qub. Na tukajaalia katika dhuria zake Unabii na Kitabu, na tukampa ujira wake katika dunia; naye hakika katika Akhera bila ya shaka ni katika watu wema.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَلُوطًا إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦٓ إِنَّكُمۡ لَتَأۡتُونَ ٱلۡفَٰحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنۡ أَحَدٖ مِّنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na pale Luti alipowaambia watu wake, "Hakika nyinyi mnafanya uchafu, ambao hapana mmoja katika walimwengu aliyewatangulia kwa hayo.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
أَئِنَّكُمۡ لَتَأۡتُونَ ٱلرِّجَالَ وَتَقۡطَعُونَ ٱلسَّبِيلَ وَتَأۡتُونَ فِي نَادِيكُمُ ٱلۡمُنكَرَۖ فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوۡمِهِۦٓ إِلَّآ أَن قَالُواْ ٱئۡتِنَا بِعَذَابِ ٱللَّهِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Je, nyinyi mnawaingilia wanaume, na mnaikata njia? Na katika mikutano yenu mnafanya maovu?" Basi haikuwa jawabu ya watu wake isipokuwa walisema, "Tuletee hiyo adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwa wewe ni katika wakweli."
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قَالَ رَبِّ ٱنصُرۡنِي عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Akasema, "Ewe Mola wangu Mlezi, ninusuru kutokana na watu waharibifu hawa!"
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَلَمَّا جَآءَتۡ رُسُلُنَآ إِبۡرَٰهِيمَ بِٱلۡبُشۡرَىٰ قَالُوٓاْ إِنَّا مُهۡلِكُوٓاْ أَهۡلِ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةِۖ إِنَّ أَهۡلَهَا كَانُواْ ظَٰلِمِينَ
Na wajumbe wetu walipomjia Ibrahim na bishara, walisema, "Hakika sisi hapana shaka tutawaangamiza watu wa mji huu, kwani watu wake hakika wamekuwa madhalimu."
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قَالَ إِنَّ فِيهَا لُوطٗاۚ قَالُواْ نَحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَن فِيهَاۖ لَنُنَجِّيَنَّهُۥ وَأَهۡلَهُۥٓ إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ كَانَتۡ مِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ
Akasema, "Hakika humo yumo Luti." Wao wakasema, "Sisi tunajua zaidi ni nani yumo humo. Hapana shaka tutamwokoa yeye na ahali zake, isipokuwa mkewe aliye miongoni mwa watakaokaa nyuma."
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَلَمَّآ أَن جَآءَتۡ رُسُلُنَا لُوطٗا سِيٓءَ بِهِمۡ وَضَاقَ بِهِمۡ ذَرۡعٗاۖ وَقَالُواْ لَا تَخَفۡ وَلَا تَحۡزَنۡ إِنَّا مُنَجُّوكَ وَأَهۡلَكَ إِلَّا ٱمۡرَأَتَكَ كَانَتۡ مِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ
Na wajumbe wetu walipomfikia Luti, alihuzunika kwa sababu yao, na moyo ukaona dhiki kubwa kwa sababu yao. Wakasema, "Usihofu, wala usihuzunike. Hakika sisi tutakuokoa wewe na ahali zako, isipokuwa mkeo aliye miongoni mwa watakaokaa nyuma.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
إِنَّا مُنزِلُونَ عَلَىٰٓ أَهۡلِ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةِ رِجۡزٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ
Kwa yakini sisi tutawateremshia watu wa mji huu adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya uchafu wanaoufanya.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَلَقَد تَّرَكۡنَا مِنۡهَآ ءَايَةَۢ بَيِّنَةٗ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ
Na hakika tumeacha katika mji huo Ishara iliyo wazi kwa watu wanaotumia akili zao.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَإِلَىٰ مَدۡيَنَ أَخَاهُمۡ شُعَيۡبٗا فَقَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱرۡجُواْ ٱلۡيَوۡمَ ٱلۡأٓخِرَ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ
Na kwa Madyana tulimtuma ndugu yao Shuaibu, naye akasema, "Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu na iogopeni Siku ya Akhera, wala msiende katika ardhi mkifanya uharibifu."
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلرَّجۡفَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دَارِهِمۡ جَٰثِمِينَ
Lakini walimkadhibisha, basi ukawatwaa mtikiso wa ardhi, wakapambazukiwa ndani ya nyumba zao nao wameanguka kifudifudi.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَعَادٗا وَثَمُودَاْ وَقَد تَّبَيَّنَ لَكُم مِّن مَّسَٰكِنِهِمۡۖ وَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَعۡمَٰلَهُمۡ فَصَدَّهُمۡ عَنِ ٱلسَّبِيلِ وَكَانُواْ مُسۡتَبۡصِرِينَ
Na pia kina A'di na Thamud. Nanyi yamekwisha wabainikia kutokana na maskani zao. Na Shetani aliwapambia vitendo vyao, na akawazuilia Njia, na hali walikuwa wenye kuona.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَقَٰرُونَ وَفِرۡعَوۡنَ وَهَٰمَٰنَۖ وَلَقَدۡ جَآءَهُم مُّوسَىٰ بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَٱسۡتَكۡبَرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا كَانُواْ سَٰبِقِينَ
Na pia Qaruni na Firauni na Hamana! Na Musa aliwajia kwa Ishara waziwazi, lakini walijivuna katika nchi, wala hawakuweza kushinda.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
فَكُلًّا أَخَذۡنَا بِذَنۢبِهِۦۖ فَمِنۡهُم مَّنۡ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِ حَاصِبٗا وَمِنۡهُم مَّنۡ أَخَذَتۡهُ ٱلصَّيۡحَةُ وَمِنۡهُم مَّنۡ خَسَفۡنَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ وَمِنۡهُم مَّنۡ أَغۡرَقۡنَاۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيَظۡلِمَهُمۡ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ
Basi kila mmoja tulimtesa kwa mujibu wa makosa yake. Kati yao wapo tuliowapelekea kimbunga cha changarawe; na kati yao wapo walionyakuliwa na ukelele; na kati yao wapo ambao tuliwadidimiza katika ardhi; na kati yao wapo tuliowazamisha. Wala Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wenyewe wakijidhulumu nafsi zao.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
مَثَلُ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَوۡلِيَآءَ كَمَثَلِ ٱلۡعَنكَبُوتِ ٱتَّخَذَتۡ بَيۡتٗاۖ وَإِنَّ أَوۡهَنَ ٱلۡبُيُوتِ لَبَيۡتُ ٱلۡعَنكَبُوتِۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ
Mfano wa wale waliowafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyojitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
إِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Kwa hakika Mwenyezi Mungu anajua kila kitu wanachokiomba badala yake Yeye. Na Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَتِلۡكَ ٱلۡأَمۡثَٰلُ نَضۡرِبُهَا لِلنَّاسِۖ وَمَا يَعۡقِلُهَآ إِلَّا ٱلۡعَٰلِمُونَ
Na hiyo ni mifano tunawapigia watu, na hawaifahamu isipokuwa wenye elimu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
خَلَقَ ٱللَّهُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ
Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Kwa hakika katika hayo ipo Ishara kwa Waumini.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
ٱتۡلُ مَآ أُوحِيَ إِلَيۡكَ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَۖ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ تَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِۗ وَلَذِكۡرُ ٱللَّهِ أَكۡبَرُۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تَصۡنَعُونَ
Soma yale uliyofunuliwa katika Kitabu, na ushike Swala. Hakika Swala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
۞ وَلَا تُجَٰدِلُوٓاْ أَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ إِلَّا بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ إِلَّا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡهُمۡۖ وَقُولُوٓاْ ءَامَنَّا بِٱلَّذِيٓ أُنزِلَ إِلَيۡنَا وَأُنزِلَ إِلَيۡكُمۡ وَإِلَٰهُنَا وَإِلَٰهُكُمۡ وَٰحِدٞ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ
Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu isipokuwa kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni, "Tumeyaamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu. Na mungu wetu na mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake."
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَكَذَٰلِكَ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَۚ فَٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۖ وَمِنۡ هَٰٓؤُلَآءِ مَن يُؤۡمِنُ بِهِۦۚ وَمَا يَجۡحَدُ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَّا ٱلۡكَٰفِرُونَ
Na namna hivyo tumekuteremshia Kitabu hiki (Qur-ani). Basi wale tuliowapa Kitabu (cha Biblia) wataiamini (Qur-ani), na miongoni mwa hawa (washirikina) wapo watakaoiamini. Na hawazikatai Ishara zetu isipokuwa makafiri.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَمَا كُنتَ تَتۡلُواْ مِن قَبۡلِهِۦ مِن كِتَٰبٖ وَلَا تَخُطُّهُۥ بِيَمِينِكَۖ إِذٗا لَّٱرۡتَابَ ٱلۡمُبۡطِلُونَ
Na wewe hukuwa kabla yake unasoma kitabu chochote, wala hukukiandika kwa mkono wako wa kulia. Ingelikuwa hivyo, wana batili wangelifanya shaka.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
بَلۡ هُوَ ءَايَٰتُۢ بَيِّنَٰتٞ فِي صُدُورِ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَۚ وَمَا يَجۡحَدُ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَّا ٱلظَّٰلِمُونَ
Bali hii (Qur-ani) ni Ishara zilizo wazi katika vifua vya wale waliopewa elimu. Na hawazikatai Ishara zetu isipokuwa madhalimu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَقَالُواْ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ ءَايَٰتٞ مِّن رَّبِّهِۦۚ قُلۡ إِنَّمَا ٱلۡأٓيَٰتُ عِندَ ٱللَّهِ وَإِنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٞ مُّبِينٌ
Na walisema, "Mbona hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?" Sema, "Hakika Ishara ziko tu kwake Mwenyezi Mungu; ama mimi kwa hakika ni mwonyaji mwenye kubainisha tu."
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
أَوَلَمۡ يَكۡفِهِمۡ أَنَّآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ يُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَرَحۡمَةٗ وَذِكۡرَىٰ لِقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Je, kwani hayakuwatosha ya kwamba tumekuteremshia Kitabu hiki wanachosomewa? Hakika katika hayo, zipo rehema na mawaidha kwa watu wanaoamini.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قُلۡ كَفَىٰ بِٱللَّهِ بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡ شَهِيدٗاۖ يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱلۡبَٰطِلِ وَكَفَرُواْ بِٱللَّهِ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Sema, "Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni Shahidi kati yangu na nyinyi. Anayajua yaliyomo katika mbingu na ardhi. Na wale wanaoiamini batili na wakamkufuru Mwenyezi Mungu, hao ndio waliohasiri."
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَيَسۡتَعۡجِلُونَكَ بِٱلۡعَذَابِ وَلَوۡلَآ أَجَلٞ مُّسَمّٗى لَّجَآءَهُمُ ٱلۡعَذَابُۚ وَلَيَأۡتِيَنَّهُم بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ
Na wanakuhimiza waletewe adhabu kwa haraka. Na lau kuwa hapana wakati maalumu uliowekwa, basi adhabu ingeliwajia, na ingeliwatokea kwa ghafla ilhali wao hawana habari.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
يَسۡتَعۡجِلُونَكَ بِٱلۡعَذَابِ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةُۢ بِٱلۡكَٰفِرِينَ
Wanakuhimiza waletewe adhabu kwa haraka, na hali Jahannamu kwa hakika imewazunguka makafiri!
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
يَوۡمَ يَغۡشَىٰهُمُ ٱلۡعَذَابُ مِن فَوۡقِهِمۡ وَمِن تَحۡتِ أَرۡجُلِهِمۡ وَيَقُولُ ذُوقُواْ مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Siku itakapowafunika adhabu hiyo kutoka juu yao na chini ya miguu yao, na atasema, "Onjeni hayo mliyokuwa mkiyatenda!"
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
يَٰعِبَادِيَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّ أَرۡضِي وَٰسِعَةٞ فَإِيَّٰيَ فَٱعۡبُدُونِ
Enyi waja wangu mlioamini! Kwa hakika ardhi yangu ina wasaa. Basi niabuduni Mimi peke yangu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
كُلُّ نَفۡسٖ ذَآئِقَةُ ٱلۡمَوۡتِۖ ثُمَّ إِلَيۡنَا تُرۡجَعُونَ
Kila nafsi itaonja mauti. Kisha mtarudishwa kwetu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَنُبَوِّئَنَّهُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ غُرَفٗا تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ نِعۡمَ أَجۡرُ ٱلۡعَٰمِلِينَ
Na ambao wameamini na wakatenda mema, bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Bustani ya mbinguni yenye kupitiwa chini yake mito, wakidumu humo. Ni mzuri ulioje huo ujira wa watendao.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
ٱلَّذِينَ صَبَرُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ
Ambao walisubiri, na wakamtegemea Mola wao Mlezi.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَكَأَيِّن مِّن دَآبَّةٖ لَّا تَحۡمِلُ رِزۡقَهَا ٱللَّهُ يَرۡزُقُهَا وَإِيَّاكُمۡۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ
Na ni wanyama wangapi hawawezi kujimilikia riziki zao! Mwenyezi Mungu anawaruzuku hao na nyinyi pia. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua zaidi.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَلَئِن سَأَلۡتَهُم مَّنۡ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَسَخَّرَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُۖ فَأَنَّىٰ يُؤۡفَكُونَ
Na ukiwauliza; ni nani aliyeumba mbingu na ardhi na akafanya jua na mwezi kutiii amri yake? Bila ya shaka, watasema: Mwenyezi Mungu. Wapi basi wanakogeuzwa?
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
ٱللَّهُ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦ وَيَقۡدِرُ لَهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ
Mwenyezi Mungu humkunjulia, na humkunjia riziki amtakaye katika waja wake. Kwa hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi kila kitu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَلَئِن سَأَلۡتَهُم مَّن نَّزَّلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ مِنۢ بَعۡدِ مَوۡتِهَا لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُۚ قُلِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡقِلُونَ
Na ukiwauliza: Ni nani anayeteremsha maji kutoka mbinguni, na akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake? Bila ya shaka watasema: Ni Mwenyezi Mungu. Sema: Alhamdu Lillahi (Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu). Bali wengi katika wao hawatumii akili.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَمَا هَٰذِهِ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَآ إِلَّا لَهۡوٞ وَلَعِبٞۚ وَإِنَّ ٱلدَّارَ ٱلۡأٓخِرَةَ لَهِيَ ٱلۡحَيَوَانُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ
Na haya maisha ya dunia si chochote isipokuwa ni pumbao na mchezo. Na hakika nyumba ya Akhera ndiyo maisha hasa; laiti wangelikuwa wanajua!
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
فَإِذَا رَكِبُواْ فِي ٱلۡفُلۡكِ دَعَوُاْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ فَلَمَّا نَجَّىٰهُمۡ إِلَى ٱلۡبَرِّ إِذَا هُمۡ يُشۡرِكُونَ
Na wanapopanda katika marikebu, humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumkusudia yeye tu dini yake. Lakini anapowavua wakafika nchi kavu, mara wanamshirikisha.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
لِيَكۡفُرُواْ بِمَآ ءَاتَيۡنَٰهُمۡ وَلِيَتَمَتَّعُواْۚ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ
Wapate kuyakufuru yale tuliyowapa, na wajistareheshe. Lakini watakuja jua!
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّا جَعَلۡنَا حَرَمًا ءَامِنٗا وَيُتَخَطَّفُ ٱلنَّاسُ مِنۡ حَوۡلِهِمۡۚ أَفَبِٱلۡبَٰطِلِ يُؤۡمِنُونَ وَبِنِعۡمَةِ ٱللَّهِ يَكۡفُرُونَ
Je, hawaoni ya kwamba tumeifanya nchi takatifu ina amani, na hali watu wengine wananyakuliwa kote kwa majirani zao? Je, wanaamini batili, na neema za Mwenyezi Mungu wanazikufuru?
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِٱلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَهُۥٓۚ أَلَيۡسَ فِي جَهَنَّمَ مَثۡوٗى لِّلۡكَٰفِرِينَ
Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu au anayekadhibisha Haki inapomjia? Je, si katika Jahannamu ndiyo yatakuwa makazi ya makafiri?
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَٱلَّذِينَ جَٰهَدُواْ فِينَا لَنَهۡدِيَنَّهُمۡ سُبُلَنَاۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَمَعَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na wale wanaofanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi hakika tutawaongoa kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na watu wema.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
 
แปลความหมาย​ สูเราะฮ์: Al-‘Ankabūt
สารบัญสูเราะฮ์ หมายเลข​หน้า​
 
แปล​ความหมาย​อัลกุรอาน​ - คำแปลภาษาสวาฮิลี - ศูนย์การแปลรุว๊าด - สารบัญ​คำแปล

แปลโดยทีมงานศูนย์แปลรุว๊าด ร่วมกับสมาคมการเผยแพร่ศาสนาอิสลามที่รอบวะฮ์ และสมาคมบริการเนื้อหาอิสลามด้วยภาษาต่าง ๆ

ปิด