Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - Indise ng mga Salin

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Salin ng mga Kahulugan Ayah: (13) Surah: Fātir
يُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِي ٱلنَّهَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِي ٱلَّيۡلِ وَسَخَّرَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلّٞ يَجۡرِي لِأَجَلٖ مُّسَمّٗىۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡ لَهُ ٱلۡمُلۡكُۚ وَٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ مَا يَمۡلِكُونَ مِن قِطۡمِيرٍ
Anauingiza usiku katika mchana, na anauingiza mchana katika usiku. Na amelifanya jua na mwezi kutumikia. Kila kimojapo kinakwenda kwa muda maalumu. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Na hao mnao waomba badala yake hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende.
Yeye huuingiza usiku katika mchana, na mchana katika usiku. Matokeo yake ni kuwa saa zao hurefuka na hufupika kwa mujibu wa mipango ya hikima miaka nenda miaka rudi. Na Yeye amelifanya jua na mwezi kutumika kwa manufaa yenu. Kila kimojapo kinakwenda kwa muda maalumu utao ishia kwake. Huyo mwenye shani kuu ndiye Mwenyezi Mungu Mwenye kuyapanga mambo yenu. Ufalme ni wake Yeye peke yake. Na hao wengineo mnao waomba kuwa ni miungu mnao waabudu hawawezi kumiliki hata ugozi mwembamba ule wa kokwa ya tende. Basi inakuwaje wastahili kuabudiwa? Aya hii tukufu inaonyesha kuwa jua lina muda utakao kwisha baadae. Na huenda kuwa huo ndio utao kuwa Mwisho kwa mujibu wasemavyo wataalamu wa ilimu ya Falaki (Astronomy) kwamba jua linaunguza kuni zake za Dharra (Nuclear fuel) nayo ni Hydrogen inayo geuka kuwa Helium. Huenda kuwa ukisha muda wa jua ndio Msiba Mkuu wa Ulimwengu wote.
Ang mga Tafsir na Arabe:
 
Salin ng mga Kahulugan Ayah: (13) Surah: Fātir
Indise ng mga Surah Numero ng Pahina
 
Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - Indise ng mga Salin

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

Isara