Check out the new design

Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili ni Ali Mohsin Al-Barwani * - Indise ng mga Salin

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Salin ng mga Kahulugan Surah: Al-An‘ām   Ayah:
فَقُطِعَ دَابِرُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْۚ وَٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Ikakatwa mizizi ya watu walio dhulumu - na wa kuhimidiwa ni Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Ikateketezwa kabisa kaumu hii, yenye kudhulumu, asibakie hata mmoja. Alhamdulillahi, wa kuhimidiwa kwa sifa zote njema ni Mwenyezi Mungu, mwenye kuwalea viumbe kwa neema na nakama, na mwenye kuisafisha ardhi na ufisadi wa wenye kudhulumu.
Ang mga Tafsir na Arabe:
قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِنۡ أَخَذَ ٱللَّهُ سَمۡعَكُمۡ وَأَبۡصَٰرَكُمۡ وَخَتَمَ عَلَىٰ قُلُوبِكُم مَّنۡ إِلَٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِ يَأۡتِيكُم بِهِۗ ٱنظُرۡ كَيۡفَ نُصَرِّفُ ٱلۡأٓيَٰتِ ثُمَّ هُمۡ يَصۡدِفُونَ
Sema: Mwaonaje Mwenyezi Mungu akanyakua kusikia kwenu, na kuona kwenu, na akaziziba nyoyo zenu, ni mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu ataye kuleteeni hayo tena? Angalia vipi tunavyo zieleza Ishara, kisha wao wanapuuza.
Waambie, ewe Nabii: Hebu nambieni--Mwenyezi Mungu akinyakua kusikia kwenu, na akazifunika nyoyo zenu zisiweze kutambua kitu, akakufanyeni viziwi, vipofu hamfahamu kitu - mtamuabudu mungu gani isipo kuwa Mwenyezi Mungu atakae weza kukurejesheeni aliyo kunyang'anyeni Mwenyezi Mungu? Ewe Nabii! Tazama vipi tunavyo ziweka wazi hoja na kuzipanga mbali mbali. Kisha pamoja na haya wao wanakataa kuzizingatia na kunafiika kwazo.
Ang mga Tafsir na Arabe:
قُلۡ أَرَءَيۡتَكُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُ ٱللَّهِ بَغۡتَةً أَوۡ جَهۡرَةً هَلۡ يُهۡلَكُ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلظَّٰلِمُونَ
Sema: Mwaonaje, ikikufikieni adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa ghafla, au kwa dhaahiri, jee wataangamizwa isipo kuwa walio dhulumu?
Sema: Hebu nambieni--Ikikufikieni adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa ghafla bila ya kuitarajia, au ikakujieni kwa dhaahiri nanyi mnaitaraji, kwa kuwa mmeonywa kuwa itakuja - hivyo adhabu hiyo itamsibu yeyote ila wale watu walio jidhulumu nafsi zao kwa kushikilia ukafiri na upotovu? Hakika haitamsibu mwenginewe.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَمَا نُرۡسِلُ ٱلۡمُرۡسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَۖ فَمَنۡ ءَامَنَ وَأَصۡلَحَ فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ
Na hatuwatumi Mitume ila huwa ni wabashiri na waonyaji. Na wenye kuamini na wakatenda mema haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.
Na Sisi hatuwatumi Manabii ila ni kwa ajili ya kuwabashiria wenye kuamini mambo ya kheri na thawabu, na kuwahadharisha na adhabu wale wanao kufuru. Basi wenye kuuamini wito wao, na wakatenda mema, hawatakuwa na khofu ya kuwapata shari, wala hawatahuzunika kwa kuikosa kheri.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يَمَسُّهُمُ ٱلۡعَذَابُ بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ
Na walio kanusha Ishara zetu itawagusa adhabu kwa walivyo kuwa wakipotoka.
Na wale wanao zikanusha dalili zilio wazi za ukweli wa waliyo kuja nayo Mitume, watapata adhabu kwa kutoka kwao kwenye ut'iifu na Imani.
Ang mga Tafsir na Arabe:
قُل لَّآ أَقُولُ لَكُمۡ عِندِي خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ وَلَآ أَقُولُ لَكُمۡ إِنِّي مَلَكٌۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّۚ قُلۡ هَلۡ يَسۡتَوِي ٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡبَصِيرُۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ
Sema: Mimi sikwambiini kuwa ninazo khazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyo fichikana. Wala sikwambiini kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati ila yanayo funuliwa kwangu. Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikiri?
Ewe Mtume! Waambie hawa makafiri: Mimi sikwambiini kuwa mimi nina madaraka aliyo nayo Mwenyezi Mungu hata nikuitikieni kwa mnayo yataka. Wala sidai kuwa mimi nina ilimu ya mambo ya ghaibu, ambayo Mwenyezi Mungu hakunijuvya. Wala sisemi kuwa mimi ni Malaika ninaweza kupanda mbinguni! Mimi si chochote ila ni mwanaadamu tu. Sifuati ila Mwenyezi Mungu anacho nifunulia. Sema ewe Nabii: Je, wanakuwa sawa, aliye potoka na aliye ongoka katika kuzijua kweli hizi? Hivyo, inakuelekeeni nyinyi mkautupa uwongofu ninao kuleteeni, msiuzingatie kwa akili zenu hata ikakubainikieni Haki?
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَأَنذِرۡ بِهِ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحۡشَرُوٓاْ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ لَيۡسَ لَهُم مِّن دُونِهِۦ وَلِيّٞ وَلَا شَفِيعٞ لَّعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ
Na waonye kwayo wanao ogopa kuwa watakusanywa kwa Mola wao Mlezi, hali kuwa hawana mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye, ili wapate kuchamngu.
Na wahadharishe kwa yaliyomo katika hii Qur'ani wale wanayo khofu vitisho vya Siku watapo wachunga Malaika kwa ajili ya hisabu na malipo, Siku ambayo itayo kuwa haina wa kunusuru wala kuombea ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, wahadharishe wajitenge mbali na vinavyo mkasirisha Mwenyezi Mungu.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَلَا تَطۡرُدِ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ رَبَّهُم بِٱلۡغَدَوٰةِ وَٱلۡعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجۡهَهُۥۖ مَا عَلَيۡكَ مِنۡ حِسَابِهِم مِّن شَيۡءٖ وَمَا مِنۡ حِسَابِكَ عَلَيۡهِم مِّن شَيۡءٖ فَتَطۡرُدَهُمۡ فَتَكُونَ مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ
Wala usiwafukuze wanao mwomba Mola Mlezi wao asubuhi na jioni kwa kutaka radhi yake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata uwafukuze na uwe miongoni mwa wenye kudhulumu.
Na ewe Nabii! Usiitikie wito wa makafiri walio panda vichwa, ukawatenga Waumini wanyonge, wanao muabudu Mwenyezi Mungu daima, wala hawatafuti ila radhi zake. Wala usivishughulikie vitimbi vya washirikina juu ya hawa Waumini. Kwani wewe mbele ya Mwenyezi Mungu huna jukumu juu ya vitendo vyao, kama wao wasivyo kuwa na jukumu juu ya chochote katika vitendo vyako. Na ukiwakubalia hawa makafiri wenye kani, na ukawatenga Waumini, utakuwa miongoni mwa walio dhulumu.
Ang mga Tafsir na Arabe:
 
Salin ng mga Kahulugan Surah: Al-An‘ām
Indise ng mga Surah Numero ng Pahina
 
Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili ni Ali Mohsin Al-Barwani - Indise ng mga Salin

Isinalin ni Ali Mohsen Al-Barwani.

Isara