Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - Indise ng mga Salin

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Salin ng mga Kahulugan Ayah: (128) Surah: Al-An‘ām
وَيَوۡمَ يَحۡشُرُهُمۡ جَمِيعٗا يَٰمَعۡشَرَ ٱلۡجِنِّ قَدِ ٱسۡتَكۡثَرۡتُم مِّنَ ٱلۡإِنسِۖ وَقَالَ أَوۡلِيَآؤُهُم مِّنَ ٱلۡإِنسِ رَبَّنَا ٱسۡتَمۡتَعَ بَعۡضُنَا بِبَعۡضٖ وَبَلَغۡنَآ أَجَلَنَا ٱلَّذِيٓ أَجَّلۡتَ لَنَاۚ قَالَ ٱلنَّارُ مَثۡوَىٰكُمۡ خَٰلِدِينَ فِيهَآ إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٞ
Na ile Siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu. Na marafiki zao katika wanaadamu waseme: Mola Mlezi wetu! Tulinufaishana sisi na wao. Na tumefikia ukomo wetu ulio tuwekea. Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndio makaazi yenu, mtadumu humo, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hikima, na Mwenye kujua.
Na ilivyo kuwa wale walio ifuata Njia ya Mwenyezi Mungu Iliyo Nyooka watapata amani na ulinzi wa Mwenyezi Mungu, basi wale walio ifuata njia ya Shetani watapata malipo ya maasi waliyo yafanya hapo watapo kusanywa wote Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu Aliye tukuka kwa Utukufu wake atawaambia hao majini na watu walio tenda dhambi: Enyi mlio kusanyika, katika majini hadi mmekithiri kuwapoteza watu, hata wamekufuateni wengi! Tena watasema wale watu walio wafuata: Ewe Muumba wetu na Mwenye kutusimamia! Hakika sisi kwa sisi tulipeana manufaa, na tukapeana starehe kwa matamanio; na sasa ajali yetu uliyo tuwekea imekwisha fika. Hapo Mwenyezi Mungu Aliye tukuka kwa utukufu wake atasema: Makaazi yenu ya kukaa ni Motoni. Mtadumu humo milele, isipo kuwa Mwenyezi Mungu atakao penda kuwavua katika wale wasio kanya Ujumbe wa Mwenyezi Mungu. Na hakika vitendo vya Mwenyezi Mungu daima vinakuwa kwa mujibu wa hikima na ujuzi.
Ang mga Tafsir na Arabe:
 
Salin ng mga Kahulugan Ayah: (128) Surah: Al-An‘ām
Indise ng mga Surah Numero ng Pahina
 
Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - Indise ng mga Salin

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

Isara