Check out the new design

Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili ng Sentro ng Rowad sa Pagsasalin * - Indise ng mga Salin


Salin ng mga Kahulugan Surah: Al-A‘rāf   Ayah:
وَجَٰوَزۡنَا بِبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱلۡبَحۡرَ فَأَتَوۡاْ عَلَىٰ قَوۡمٖ يَعۡكُفُونَ عَلَىٰٓ أَصۡنَامٖ لَّهُمۡۚ قَالُواْ يَٰمُوسَى ٱجۡعَل لَّنَآ إِلَٰهٗا كَمَا لَهُمۡ ءَالِهَةٞۚ قَالَ إِنَّكُمۡ قَوۡمٞ تَجۡهَلُونَ
Na tukawavusha bahari Wana wa Israili, kisha wakajia kaumu waliokuwa wanayaabudu masanamu yao. Wakasema, "Ewe Musa! Tufanyie mungu kama hawa walivyo na miungu." Musa akasema: Hakika nyinyi ni kaumu msiojua kitu.
Ang mga Tafsir na Arabe:
إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ مُتَبَّرٞ مَّا هُمۡ فِيهِ وَبَٰطِلٞ مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Hakika hawa, haya waliyomo yatakuja angamia, na ni batili hayo waliyokuwa wakiyafanya.
Ang mga Tafsir na Arabe:
قَالَ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَبۡغِيكُمۡ إِلَٰهٗا وَهُوَ فَضَّلَكُمۡ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ
Akasema, "Je, niwatafutie mungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ilhali Yeye ndiye aliyewafadhilisha juu ya walimwengu wote?"
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَإِذۡ أَنجَيۡنَٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ يُقَتِّلُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ
Na pale tulipowaokoa kutoka kwa watu wa Firauni waliowatia adhabu mbaya zaidi. Wakiwaua wavulana wenu, na wakawaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo yalikuwa majaribio makubwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi.
Ang mga Tafsir na Arabe:
۞ وَوَٰعَدۡنَا مُوسَىٰ ثَلَٰثِينَ لَيۡلَةٗ وَأَتۡمَمۡنَٰهَا بِعَشۡرٖ فَتَمَّ مِيقَٰتُ رَبِّهِۦٓ أَرۡبَعِينَ لَيۡلَةٗۚ وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَٰرُونَ ٱخۡلُفۡنِي فِي قَوۡمِي وَأَصۡلِحۡ وَلَا تَتَّبِعۡ سَبِيلَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Na tulimuahidi Musa masiku thelathini na tukayatimiza kwa kumi; basi ikatimia miadi ya Mola wake Mlezi masiku arabaini. Na Musa akamwambia kaka yake, Haarun: Shika pahali pangu katika kaumu yangu na utengeneze, wala usifuate njia ya waharibifu.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَلَمَّا جَآءَ مُوسَىٰ لِمِيقَٰتِنَا وَكَلَّمَهُۥ رَبُّهُۥ قَالَ رَبِّ أَرِنِيٓ أَنظُرۡ إِلَيۡكَۚ قَالَ لَن تَرَىٰنِي وَلَٰكِنِ ٱنظُرۡ إِلَى ٱلۡجَبَلِ فَإِنِ ٱسۡتَقَرَّ مَكَانَهُۥ فَسَوۡفَ تَرَىٰنِيۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُۥ لِلۡجَبَلِ جَعَلَهُۥ دَكّٗا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقٗاۚ فَلَمَّآ أَفَاقَ قَالَ سُبۡحَٰنَكَ تُبۡتُ إِلَيۡكَ وَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Na alipokuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamuongelesha, alisema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe nikutazame. Mwenyezi Mungu akasema: Hutaniona. Lakini utazame huo mlima. Ikiwa utabaki mahali pake, basi utaniona. Basi alipojionyesha Mola wake Mlezi kwa mlima huo, akaufanya upasukepasuke, na Musa akaanguka chini akazimia. Basi alipozindukana, akasema: Subhanaka (Umetakasika)! Nimetubia kwako, na mimi ni wa kwanza wa Waumini.
Ang mga Tafsir na Arabe:
 
Salin ng mga Kahulugan Surah: Al-A‘rāf
Indise ng mga Surah Numero ng Pahina
 
Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili ng Sentro ng Rowad sa Pagsasalin - Indise ng mga Salin

Isinalin ito ng isang pangkat ng Sentro ng Rowad sa Pagsasalin sa pakikipagtulungan ng Samahan ng Da‘wah sa Rabwah at Samahan ng Paglilingkod sa Nilalamang Islāmiko sa mga Wika.

Isara