Check out the new design

Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dili Tercüme - Rowad Tercüme Merkezi * - Mealler fihristi


Anlam tercümesi Sure: Sûratu'l-Bakarah   Ayet:
مَثَلُهُمۡ كَمَثَلِ ٱلَّذِي ٱسۡتَوۡقَدَ نَارٗا فَلَمَّآ أَضَآءَتۡ مَا حَوۡلَهُۥ ذَهَبَ ٱللَّهُ بِنُورِهِمۡ وَتَرَكَهُمۡ فِي ظُلُمَٰتٖ لَّا يُبۡصِرُونَ
Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto, na ulipoangaza vile vilivyoko kandokando yake, Mwenyezi Mungu aliiondoa nuru yao na akawaacha katika viza mbalimbali, hawaoni.[1]
[1] Huu ni mfano wa yule aliyekuwa katika giza kubwa, kwa hivyo akauwasha moto kutoka kwa mtu mwingine. (Tafsir Assa'dii) Na nuru ya moto huo ilitoka kwa Waislamu ambao wao (wanafiki) wanaishi pamoja nao. Na hakusema: Mwenyezi Mungu aliuondoa 'mwangaza wao'. Kwa sababu mwangaza ni ziada juu ya nuru. Kwa hivyo, aliondoa asili (nuru) na ziada yake (mwangaza). (Tafsir Ibn Al-Qayyim)
Arapça tefsirler:
صُمُّۢ بُكۡمٌ عُمۡيٞ فَهُمۡ لَا يَرۡجِعُونَ
Ni viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea.[1]
[1] Ni viziwi kwa sababu hawaisikii heri. Ni mabubu kwa sababu hawaitamki heri. Na ni vipofu kwa sababu hawaioni haki. Kwa hivyo, hawatarejea kwa haki kwa kuwa waliiacha baada ya kuijua. Tofauti na mwenye kuiacha haki kwa ujinga na upotovu, yeye yuko karibu zaidi na kurudi katika haki. (Tafsir Assa'dii)
Arapça tefsirler:
أَوۡ كَصَيِّبٖ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فِيهِ ظُلُمَٰتٞ وَرَعۡدٞ وَبَرۡقٞ يَجۡعَلُونَ أَصَٰبِعَهُمۡ فِيٓ ءَاذَانِهِم مِّنَ ٱلصَّوَٰعِقِ حَذَرَ ٱلۡمَوۡتِۚ وَٱللَّهُ مُحِيطُۢ بِٱلۡكَٰفِرِينَ
Au ni kama mvua kubwa itokayo mbinguni, ina viza mbalimbali, na radi, na umeme; wakawa wanatia vidole vyao katika masikio yao kwa sababu ya mapigo ya radi, kwa kuogopa kufa. Na Mwenyezi Mungu amewazunguka makafiri.[1]
[1] Hapa Mwenyezi Mugnu aliufananisha uwongofu aliowaongoza kwao waja wake, na mvua. Kwa sababu, nyoyo huhuishwa kwa uwongofu, kama vile ardhi huhuishwa na mvua. Na fungu la wanafiki katika uwongofu huo ni kama fungu la yule ambaye hakupata katika mvua isipokuwa giza, radi na umeme, wala hana fungu zaidi ya hayo katika yale yaliyokusudiwa kutoka kwa mvua hiyo kama vile uhai wa nchi, watu, miti na wanyama. (Tafsir Ibn Al-Qayyim)
Arapça tefsirler:
يَكَادُ ٱلۡبَرۡقُ يَخۡطَفُ أَبۡصَٰرَهُمۡۖ كُلَّمَآ أَضَآءَ لَهُم مَّشَوۡاْ فِيهِ وَإِذَآ أَظۡلَمَ عَلَيۡهِمۡ قَامُواْۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَذَهَبَ بِسَمۡعِهِمۡ وَأَبۡصَٰرِهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ
Unakaribia umeme kunyakua macho yao. Kila ukiwatolea mwangaza, wanatembea ndani yake. Na linapowawia giza, wanasimama. Na angelitaka Mwenyezi Mungu angeliondoa kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.[1]
[1] Aya imemalizika kwa kusema: "Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu." Kwa sababu aliwaonya wanafiki juu ya adhabu yake na uwezo wake, na akawaambia kwamba amewazunguka, na kwamba ana uwezo wa kuondoa kusikia na kuona kwao. (Tafsir Ibn Kathir)
Arapça tefsirler:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱعۡبُدُواْ رَبَّكُمُ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ
Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliyekuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu, ili mpate Kumcha Mwenyezi Mungu.[1]
[1] "Enyi watu" inawaamrisha wanadamu wote. (Tafsir Ibn Al-Qayyim)
Arapça tefsirler:
ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ فِرَٰشٗا وَٱلسَّمَآءَ بِنَآءٗ وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجَ بِهِۦ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ رِزۡقٗا لَّكُمۡۖ فَلَا تَجۡعَلُواْ لِلَّهِ أَندَادٗا وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
(Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni ardhi hii kuwa kama tandiko, na mbingu kama paa. Na akateremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo akatoa mazao yawe riziki zenu.[1] Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika, na hali nyinyi mnajua.[2]
[1] Unaonaje mtu ambaye atazinduka kutoka usingizini au katika hali ya kughafilika, (yani kuumbwa) na akakuta ametandikiwa zulia zuri (yani ardhi) na ameekewa hema (yani mbingu) hapo; na kuwekewa chakula na kinywaji. Je hapaswi kumshukuru aliyetenda haya? Basi hii ndiyo maana ya aya hii. (Tafsir Al-Baqqaa'ii)
[2] "Na hali nyinyi mnajua" kwamba, Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliyefanya vitendo hivyo vyote. Basi ni vipi mnamfanyia washirika? (Tafsir Ibn Al-Qayyim)
Arapça tefsirler:
وَإِن كُنتُمۡ فِي رَيۡبٖ مِّمَّا نَزَّلۡنَا عَلَىٰ عَبۡدِنَا فَأۡتُواْ بِسُورَةٖ مِّن مِّثۡلِهِۦ وَٱدۡعُواْ شُهَدَآءَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyomteremshia mja wetu, basi leteni sura moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli.
Arapça tefsirler:
فَإِن لَّمۡ تَفۡعَلُواْ وَلَن تَفۡعَلُواْ فَٱتَّقُواْ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلۡحِجَارَةُۖ أُعِدَّتۡ لِلۡكَٰفِرِينَ
Na ikiwa hamtofanya - na wala hamtofanya kamwe - basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa makafiri.
Arapça tefsirler:
 
Anlam tercümesi Sure: Sûratu'l-Bakarah
Surelerin fihristi Sayfa numarası
 
Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dili Tercüme - Rowad Tercüme Merkezi - Mealler fihristi

Rowad Tercüme Merkezi Ekibi tarafından Rabvede'ki Tebliğ, İrşat ve Toplum Bilinçlendirme Derneği ve Dünya dillerinde İslami içerik ve hizmet cemiyeti işbirliğiyle tercüme edilmiştir.

Kapat