قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - عبد اللہ محمد اور ناصر خمیس

48 : 68

فَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ ٱلۡحُوتِ إِذۡ نَادَىٰ وَهُوَ مَكۡظُومٞ

Basi vumilia, (ewe Mtume), kwa kile Alichokiamua Mola wako na kukipitisha. Na miongoni mwa hivyo ni kuwapa muhula na kuchelewesha ushindi wako kwao. Na usiwe ni kama yule mtu wa chewa, naye ni Yūnus, (amani imshukie), alipokasirika na kutokuwa na uvumilivu na watu wake, pindi alipomuita Mola Wake, na huku amezongwa na maudhi, akimuomba Awaharakishie adhabu. info
التفاسير: |
next

Al-Qalam

prev
:
0:00 0:00