Wanaume ni wasimamizi imara wa wanawake, kwa yale aliyowafadhilisha kwayo Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa yale wanayoyatoa katika mali zao. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanaojilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na wale mnaochelea kutoka kwao katika utiifu, waaidhini, na wahameni katika malazi, na wapigeni. Basi wakiwatii, msitafute njia yoyote dhidi yao. Hakika, Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu, Mkubwa.[1]
[1] Na kinachomaanishwa na kuboreshwa katika kauli yake hii ni kuboreshwa kwa jinsia juu ya jinsia, na sio kumboresha kila mmoja wao juu ya mwengine. Kwa maana, kunaweza kuwa na wanawake ambao wana akili na elimu zaidi kuliko wanaume wengine. (Tafsir Tantawii)
Na mkihofia kuwepo mfarakano baina ya wawili hao, basi mtumeni mpatanishi kutoka kwa jamaa za mume, na mpatanishi kutoka kwa jamaa za mke. Ikiwa wanataka kutengeneza mambo, Mwenyezi Mungu atawawezesha kati yao. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye habari zote.
Na mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili, na jamaa, na mayatima, na masikini, na jirani wa karibu, na jirani wa ubavuni, na mwenza wa ubavuni, na mwana njia, na wale iliowamiliki mikono yenu ya kulia. Hakika, Mwenyezi Mungu hampendi mwenye kiburi anayejifahiri.
Ambao wanafanya ubahili na wanaamrisha watu ubahili, na wanaficha yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake. Na tuliwaandalia makafiri adhabu ya kudunisha.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
تلاش کے نتائج:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".