Check out the new design

قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - مرکز رواد الترجمہ * - ترجمے کی لسٹ


معانی کا ترجمہ سورت: اعراف   آیت:
۞ قَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ لَنُخۡرِجَنَّكَ يَٰشُعَيۡبُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَكَ مِن قَرۡيَتِنَآ أَوۡ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَاۚ قَالَ أَوَلَوۡ كُنَّا كَٰرِهِينَ
Wakasema waheshimiwa waliotakabari katika kaumu yake, "Lazima tutakutoa ewe Shu'aib na wale walioamini pamoja nawe katika mji wetu, au lazima mtarejea katika mila yetu." Akasema, "Je, hata kama tunachukia?"
عربی تفاسیر:
قَدِ ٱفۡتَرَيۡنَا عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا إِنۡ عُدۡنَا فِي مِلَّتِكُم بَعۡدَ إِذۡ نَجَّىٰنَا ٱللَّهُ مِنۡهَاۚ وَمَا يَكُونُ لَنَآ أَن نَّعُودَ فِيهَآ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّنَاۚ وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَيۡءٍ عِلۡمًاۚ عَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡنَاۚ رَبَّنَا ٱفۡتَحۡ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَ قَوۡمِنَا بِٱلۡحَقِّ وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلۡفَٰتِحِينَ
"Bila ya shaka tutakuwa tumemzulia uwongo Mwenyezi Mungu ikiwa tutarudi katika mila yenu baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuokoa kutokana nayo. Wala haiwi kwetu sisi kuirejea mila hiyo, isipokuwa akitaka Mwenyezi Mungu, Mola wetu Mlezi. Mola wetu Mlezi umekienea kila kitu kwa elimu. Kwa Mwenyezi Mungu tumetegemea. Mola wetu Mlezi, hukumu baina yetu na kaumu yetu kwa haki, nawe ndiwe Mbora zaidi wa wanaohukumu."
عربی تفاسیر:
وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ لَئِنِ ٱتَّبَعۡتُمۡ شُعَيۡبًا إِنَّكُمۡ إِذٗا لَّخَٰسِرُونَ
Na wakasema waheshimiwa waliokufuru katika kaumu yake, "Mkimfuata Shu'aib, basi hakika nyinyi mtahasiri."
عربی تفاسیر:
فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلرَّجۡفَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دَارِهِمۡ جَٰثِمِينَ
Basi tetemeko la ardhi likawachukua, kwa hivyo wakawa katika makazi yao wameanguka kifudifudi.
عربی تفاسیر:
ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ شُعَيۡبٗا كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَاۚ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ شُعَيۡبٗا كَانُواْ هُمُ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Wale waliomkadhibisha Shu'aib ni kama kwamba hawakuishi humo. Wale waliomkadhibisha Shu'aib walikuwa ndio waliohasiri.
عربی تفاسیر:
فَتَوَلَّىٰ عَنۡهُمۡ وَقَالَ يَٰقَوۡمِ لَقَدۡ أَبۡلَغۡتُكُمۡ رِسَٰلَٰتِ رَبِّي وَنَصَحۡتُ لَكُمۡۖ فَكَيۡفَ ءَاسَىٰ عَلَىٰ قَوۡمٖ كَٰفِرِينَ
Basi akawaachilia mbali na akasema, "Enyi kaumu yangu! Hakika nimewafikishia jumbe za Mola wangu Mlezi, na nimewanasihi. Basi vipi niwahuzunikie kaumu makafiri?"
عربی تفاسیر:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا فِي قَرۡيَةٖ مِّن نَّبِيٍّ إِلَّآ أَخَذۡنَآ أَهۡلَهَا بِٱلۡبَأۡسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ لَعَلَّهُمۡ يَضَّرَّعُونَ
Na hatukumtuma katika mji wowote Nabii yeyote isipokuwa tuliwachukua wakazi wake kwa umaskini na maradhi ili wanyenyekee.
عربی تفاسیر:
ثُمَّ بَدَّلۡنَا مَكَانَ ٱلسَّيِّئَةِ ٱلۡحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَواْ وَّقَالُواْ قَدۡ مَسَّ ءَابَآءَنَا ٱلضَّرَّآءُ وَٱلسَّرَّآءُ فَأَخَذۡنَٰهُم بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ
Kisha tukabadilisha pahali pa ubaya kwa wema, mpaka wakazidi, na wakasema, "Hakika ziliwafikia baba zetu taabu na raha." Basi tukawachukua kwa ghafla hali ya kuwa hawatambui.
عربی تفاسیر:
 
معانی کا ترجمہ سورت: اعراف
سورتوں کی لسٹ صفحہ نمبر
 
قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - مرکز رواد الترجمہ - ترجمے کی لسٹ

مرکز رواد الترجمہ گروپ نے جمعیۃ الدعوۃ‘ ربوہ اور جمعیۃ خدمۃ المحتوى الاسلامی باللغات کے تعاون سے ترجمہ کیا۔

بند کریں