Check out the new design

クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - ルゥワード翻訳事業センター * - 対訳の目次


対訳 章: 高壁章   節:
۞ قَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ لَنُخۡرِجَنَّكَ يَٰشُعَيۡبُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَكَ مِن قَرۡيَتِنَآ أَوۡ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَاۚ قَالَ أَوَلَوۡ كُنَّا كَٰرِهِينَ
Wakasema waheshimiwa waliotakabari katika kaumu yake, "Lazima tutakutoa ewe Shu'aib na wale walioamini pamoja nawe katika mji wetu, au lazima mtarejea katika mila yetu." Akasema, "Je, hata kama tunachukia?"
アラビア語 クルアーン注釈:
قَدِ ٱفۡتَرَيۡنَا عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا إِنۡ عُدۡنَا فِي مِلَّتِكُم بَعۡدَ إِذۡ نَجَّىٰنَا ٱللَّهُ مِنۡهَاۚ وَمَا يَكُونُ لَنَآ أَن نَّعُودَ فِيهَآ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّنَاۚ وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَيۡءٍ عِلۡمًاۚ عَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡنَاۚ رَبَّنَا ٱفۡتَحۡ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَ قَوۡمِنَا بِٱلۡحَقِّ وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلۡفَٰتِحِينَ
"Bila ya shaka tutakuwa tumemzulia uwongo Mwenyezi Mungu ikiwa tutarudi katika mila yenu baada ya Mwenyezi Mungu kwishatuokoa kutokana nayo. Wala haiwi kwetu sisi kuirejea mila hiyo, isipokuwa akitaka Mwenyezi Mungu, Mola wetu Mlezi. Mola wetu Mlezi umekienea kila kitu kwa elimu. Kwa Mwenyezi Mungu tumetegemea. Mola wetu Mlezi, hukumu baina yetu na kaumu yetu kwa haki, nawe ndiwe Mbora zaidi wa wanaohukumu."
アラビア語 クルアーン注釈:
وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ لَئِنِ ٱتَّبَعۡتُمۡ شُعَيۡبًا إِنَّكُمۡ إِذٗا لَّخَٰسِرُونَ
Na wakasema waheshimiwa waliokufuru katika kaumu yake, "Mkimfuata Shu'aib, basi hakika nyinyi mtahasiri."
アラビア語 クルアーン注釈:
فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلرَّجۡفَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دَارِهِمۡ جَٰثِمِينَ
Basi tetemeko la ardhi likawachukua, kwa hivyo wakawa katika makazi yao wameanguka kifudifudi.
アラビア語 クルアーン注釈:
ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ شُعَيۡبٗا كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَاۚ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ شُعَيۡبٗا كَانُواْ هُمُ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Wale waliomkadhibisha Shu'aib ni kama kwamba hawakuishi humo. Wale waliomkadhibisha Shu'aib walikuwa ndio waliohasiri.
アラビア語 クルアーン注釈:
فَتَوَلَّىٰ عَنۡهُمۡ وَقَالَ يَٰقَوۡمِ لَقَدۡ أَبۡلَغۡتُكُمۡ رِسَٰلَٰتِ رَبِّي وَنَصَحۡتُ لَكُمۡۖ فَكَيۡفَ ءَاسَىٰ عَلَىٰ قَوۡمٖ كَٰفِرِينَ
Basi akawaachilia mbali na akasema, "Enyi kaumu yangu! Hakika nimewafikishia jumbe za Mola wangu Mlezi, na nimewanasihi. Basi vipi niwahuzunikie kaumu makafiri?"
アラビア語 クルアーン注釈:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا فِي قَرۡيَةٖ مِّن نَّبِيٍّ إِلَّآ أَخَذۡنَآ أَهۡلَهَا بِٱلۡبَأۡسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ لَعَلَّهُمۡ يَضَّرَّعُونَ
Na hatukumtuma katika mji wowote Nabii yeyote isipokuwa tuliwachukua wakazi wake kwa umaskini na maradhi ili wanyenyekee.
アラビア語 クルアーン注釈:
ثُمَّ بَدَّلۡنَا مَكَانَ ٱلسَّيِّئَةِ ٱلۡحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَواْ وَّقَالُواْ قَدۡ مَسَّ ءَابَآءَنَا ٱلضَّرَّآءُ وَٱلسَّرَّآءُ فَأَخَذۡنَٰهُم بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ
Kisha tukabadilisha pahali pa ubaya kwa wema, mpaka wakazidi, na wakasema, "Hakika ziliwafikia baba zetu taabu na raha." Basi tukawachukua kwa ghafla hali ya kuwa hawatambui.
アラビア語 クルアーン注釈:
 
対訳 章: 高壁章
章名の目次 ページ番号
 
クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - ルゥワード翻訳事業センター - 対訳の目次

ルゥワード翻訳事業センターとラブワ招待協会およびイスラームコンテンツサービス協会の共訳

閉じる