Check out the new design

Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - Bản dịch tiếng Swahili - Trung tâm Dịch thuật Rowad * - Mục lục các bản dịch


Ý nghĩa nội dung Chương: Al-'Araf   Câu:
۞ وَإِذۡ نَتَقۡنَا ٱلۡجَبَلَ فَوۡقَهُمۡ كَأَنَّهُۥ ظُلَّةٞ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُۥ وَاقِعُۢ بِهِمۡ خُذُواْ مَآ ءَاتَيۡنَٰكُم بِقُوَّةٖ وَٱذۡكُرُواْ مَا فِيهِ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ
Na pale tulipounyanyua mlima juu yao ukawa kama kwamba ni kiwingu kilichowafunika, na wakadhani kuwa utawaangukia, (tukawaambia): Chukueni yale tuliyowapa kwa nguvu, na yakumbukeni yaliyomo ndani yake ili mche.
Các Tafsir tiếng Ả-rập:
وَإِذۡ أَخَذَ رَبُّكَ مِنۢ بَنِيٓ ءَادَمَ مِن ظُهُورِهِمۡ ذُرِّيَّتَهُمۡ وَأَشۡهَدَهُمۡ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَلَسۡتُ بِرَبِّكُمۡۖ قَالُواْ بَلَىٰ شَهِدۡنَآۚ أَن تَقُولُواْ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ إِنَّا كُنَّا عَنۡ هَٰذَا غَٰفِلِينَ
Na pale Mola wako Mlezi alipochukua kutoka kwa wanadamu kutoka katika migongo yao dhuria zao na akawashuhudisha juu ya nafsi zao (na kuwaambia), "Je, mimi si Mola wenu Mlezi?" Wakasema, "Ndiyo, tumeshuhudia." Mje mkasema Siku ya Qiyama, "Hakika sisi tulikuwa tumeghafilika na haya."
Các Tafsir tiếng Ả-rập:
أَوۡ تَقُولُوٓاْ إِنَّمَآ أَشۡرَكَ ءَابَآؤُنَا مِن قَبۡلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةٗ مِّنۢ بَعۡدِهِمۡۖ أَفَتُهۡلِكُنَا بِمَا فَعَلَ ٱلۡمُبۡطِلُونَ
Au mkasema: Hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla yetu, na sisi ni dhuriya zao tu baada yao. Basi utatuangamiza kwa sababu ya waliyoyafanya wapotovu?
Các Tafsir tiếng Ả-rập:
وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ وَلَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ
Na ndiyo kama hivyo tunavyozieleza Ishara kwa kina, ili huenda wakarejea.
Các Tafsir tiếng Ả-rập:
وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ ٱلَّذِيٓ ءَاتَيۡنَٰهُ ءَايَٰتِنَا فَٱنسَلَخَ مِنۡهَا فَأَتۡبَعَهُ ٱلشَّيۡطَٰنُ فَكَانَ مِنَ ٱلۡغَاوِينَ
Na wasomee habari za yule ambaye tulimpa Ishara zetu, naye akajivua kutoka kwazo, basi Shetani akamfuata. Kwa hivyo, akawa miongoni mwa waliopotea.
Các Tafsir tiếng Ả-rập:
وَلَوۡ شِئۡنَا لَرَفَعۡنَٰهُ بِهَا وَلَٰكِنَّهُۥٓ أَخۡلَدَ إِلَى ٱلۡأَرۡضِ وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُۚ فَمَثَلُهُۥ كَمَثَلِ ٱلۡكَلۡبِ إِن تَحۡمِلۡ عَلَيۡهِ يَلۡهَثۡ أَوۡ تَتۡرُكۡهُ يَلۡهَثۚ ذَّٰلِكَ مَثَلُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۚ فَٱقۡصُصِ ٱلۡقَصَصَ لَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ
Na lau kuwa tungelitaka, tungelimwinua kwazo, lakini yeye alizama katika ulimwengu na akafuata matamanio yake. Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa. Ukimhujumu hupumua na kutoa ulimi nje, na ukimwacha, pia hupumua na kutoa ulimi nje. Huo ni mfano wa kaumu ambao walizikadhibisha Ishara zetu. Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari.
Các Tafsir tiếng Ả-rập:
سَآءَ مَثَلًا ٱلۡقَوۡمُ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَأَنفُسَهُمۡ كَانُواْ يَظۡلِمُونَ
Mfano mbaya zaidi ni wa kaumu waliozikadhibisha Ishara zetu na walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.
Các Tafsir tiếng Ả-rập:
مَن يَهۡدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلۡمُهۡتَدِيۖ وَمَن يُضۡلِلۡ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, basi huyo ndiye mwongofu. Na yule aliyempoteza, basi hao ndio waliohasiri.
Các Tafsir tiếng Ả-rập:
 
Ý nghĩa nội dung Chương: Al-'Araf
Mục lục các chương Kinh Số trang
 
Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - Bản dịch tiếng Swahili - Trung tâm Dịch thuật Rowad - Mục lục các bản dịch

Người dịch: Nhóm thuộc Trung tâm Dịch thuật Rowad hợp tác với Hiệp hội Tuyên truyền Ar-Rabwah và Hiệp hội Dịch vụ Nội dung về Islam bằng đa ngôn ngữ.

Đóng lại