Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。 * - 译解目录


含义的翻译 章: 开海菲   段:
وَكَذَٰلِكَ أَعۡثَرۡنَا عَلَيۡهِمۡ لِيَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞ وَأَنَّ ٱلسَّاعَةَ لَا رَيۡبَ فِيهَآ إِذۡ يَتَنَٰزَعُونَ بَيۡنَهُمۡ أَمۡرَهُمۡۖ فَقَالُواْ ٱبۡنُواْ عَلَيۡهِم بُنۡيَٰنٗاۖ رَّبُّهُمۡ أَعۡلَمُ بِهِمۡۚ قَالَ ٱلَّذِينَ غَلَبُواْ عَلَىٰٓ أَمۡرِهِمۡ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيۡهِم مَّسۡجِدٗا
Na kama vile tulivyowalaza miaka mingi na tukawaamsha baada yake, tuliwafanya wajulikane na watu wa zama hizo baada ya muuzaji kuzigundua aina ya dirhamu alizozileta yule aliyetumwa na wao, ili watu wapate kujua kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ya Ufufuzi ni kweli na kwamba Kiyama hakina shaka ni chenye kuja. Kitahamaka hao waliowagundua watu wa Pango wakawa ni wenye kushindana kuhusu jambo la Kiyama: kuna waliolikubali na kuna waliolipinga. Na Mwenyezi Mungu Akajaalia kule kuwagundua watu wa Pango ni hoja kwa Waumini juu ya makafiri. Na baada ya mambo yao kugnuduliwa na wakafa, lilisema kundi moja la wale waliowagundua, «Jengeni kwenye mlango wa pango jengo la kuwasitiri kisha muwawache na mambo yao, Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa hali yao.» Na wakasema wale wenye kusikizwa maneno yao na wenye uwezo miongoni mwao, «Tutatengeneza mahali pao hapo msikiti wa kufanya ibada.» Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, alikataza kuyafanya makaburi ya Manabii na watu wema kuwa misikiti, na alimlaani mwenye kufanya hivyo katika nyasia zake za mwisho kwa umati wake. Pia alikataza kabisa kujenga juu ya makaburi na kuyajengea na kuandika juu yake, kwani yote hayo ni miongoni mwa upitaji kiasi unaopelekea kuwaabudu waliomo ndani.
阿拉伯语经注:
سَيَقُولُونَ ثَلَٰثَةٞ رَّابِعُهُمۡ كَلۡبُهُمۡ وَيَقُولُونَ خَمۡسَةٞ سَادِسُهُمۡ كَلۡبُهُمۡ رَجۡمَۢا بِٱلۡغَيۡبِۖ وَيَقُولُونَ سَبۡعَةٞ وَثَامِنُهُمۡ كَلۡبُهُمۡۚ قُل رَّبِّيٓ أَعۡلَمُ بِعِدَّتِهِم مَّا يَعۡلَمُهُمۡ إِلَّا قَلِيلٞۗ فَلَا تُمَارِ فِيهِمۡ إِلَّا مِرَآءٗ ظَٰهِرٗا وَلَا تَسۡتَفۡتِ فِيهِم مِّنۡهُمۡ أَحَدٗا
Watasema baadhi ya Watu wa Kitabu wenye kujishughulisha na mambo yao kwamba wao ni watatu na wa nne wao ni mbwa wao, na kundi lingine litasema kwamba wao ni watano na wa sita wao ni mbwa wao. Maneno ya makundi mawili haya ni maneno ya kudhania bila dalili yoyote. Na kundi la tatu litasema kwamba wao ni saba na wa nane wao ni mbwa wao. Sema, ewe Mtume, «Mola wangu Ndiye Mjuzi kabisa wa idadi yao,» hakuna anayeijua idadi yao isipokuwa ni wachache kati ya viumbe Wake. Basi usibishane na Watu wa Kitabu kuhusu idadi yao isipokuwa ubishi wa juu-juu usiokuwa na undani kwa kuwasimulia yale ambayo Mwenyezi Mungu amekuletea wahyi nayo, na usiulize kuhusu idadi yao na hali zao kwani wao hawalijui hilo.
阿拉伯语经注:
وَلَا تَقُولَنَّ لِشَاْيۡءٍ إِنِّي فَاعِلٞ ذَٰلِكَ غَدًا
Na usiseme juu ya kitu chochote unachoazimia kukifanya, «Mimi nitafanya kitu hiko kesho.»
阿拉伯语经注:
إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ وَٱذۡكُر رَّبَّكَ إِذَا نَسِيتَ وَقُلۡ عَسَىٰٓ أَن يَهۡدِيَنِ رَبِّي لِأَقۡرَبَ مِنۡ هَٰذَا رَشَدٗا
Isipokuwa ufungamanishe neno lako na matakwa ya Mwenyezi Mungu na useme, «Mwenyezi Mungu Atakapo.» Na mkumbuke Mola wako unaposahau kwa kusema, «Mwenyezi Mungu Atakapo.» Na kila unaposahau, mtaje Mwenyezi Mungu, kwani kumtaja Mwenyezi Mungu huondosha kusahau, na useme, «Matarajio ni kwamba Mola wangu Aniongoze njia ya karibu zaidi yenye kufikisha kwenye uongofu na ya sawa.
阿拉伯语经注:
وَلَبِثُواْ فِي كَهۡفِهِمۡ ثَلَٰثَ مِاْئَةٖ سِنِينَ وَٱزۡدَادُواْ تِسۡعٗا
Na vijana hao walikaa wakiwa wamelala ndani ya pango yao muda wa miaka mia tatu na siku tisa kwa hesabu ya kimwezi.
阿拉伯语经注:
قُلِ ٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا لَبِثُواْۖ لَهُۥ غَيۡبُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ أَبۡصِرۡ بِهِۦ وَأَسۡمِعۡۚ مَا لَهُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَلِيّٖ وَلَا يُشۡرِكُ فِي حُكۡمِهِۦٓ أَحَدٗا
Na ukiulizwa, ewe Mtume, kuhusu muda wa kukaa kwao kwenye pango, na wewe huna ujuzi wa hilo na hukupata wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi usisongee mbele kwa lolote kuhusu jambo hilo, isipokuwa sema,»Mwenyezi Mungu Ndiye Mjuzi zaidi wa muda wa kukaa kwao. Ni wake Yeye ujuzi wa visivyoonekana vya mbinguni na ardhini, ni kuona kulioje Kwake na kusikia kulioje!» Yaani : uonee ajabu ukamilifu wa kuona Kwake na wa kusikia Kwake na wa kukizunguka Kwake kila kitu. Viumbe hawana yoyote mwingine isipokuwa Yeye wa kusimamia mambo yao, na Hana mshirika katika uamuzi Wake, hukumu Yake na sheria Zake, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake.
阿拉伯语经注:
وَٱتۡلُ مَآ أُوحِيَ إِلَيۡكَ مِن كِتَابِ رَبِّكَۖ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَٰتِهِۦ وَلَن تَجِدَ مِن دُونِهِۦ مُلۡتَحَدٗا
Na usome Qur’ani, ewe Mtume, ambayo Mwenyezi Mungu Amekuletea wahyi nayo, kwani hiyo Qur’ani ni Kitabu ambacho hakuna mwenye kuyageuza maneno yake kwa kuwa ni ya kweli na ya uadilifu, na hutapata isipokuwa kwa Mola wako mahala pa wewe kuhamia wala pa kujilinda.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 开海菲
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。 - 译解目录

阿布杜拉·穆罕默德·艾布·拜克尔博士和谢赫纳赛尔·哈米斯翻译。

关闭