《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。 * - 译解目录


含义的翻译 段: (54) 章: 艾尔拉夫
إِنَّ رَبَّكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ يُغۡشِي ٱلَّيۡلَ ٱلنَّهَارَ يَطۡلُبُهُۥ حَثِيثٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ وَٱلنُّجُومَ مُسَخَّرَٰتِۭ بِأَمۡرِهِۦٓۗ أَلَا لَهُ ٱلۡخَلۡقُ وَٱلۡأَمۡرُۗ تَبَارَكَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Hakika Mola wenu, enyi watu, ni Yule Aliyeanzisha mbingu na ardhi kutoka kwenye 'adam (hali ya kutokuwako) kwa Siku Sita, kisha Akalingana, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, juu ya 'Arsh, -yaani : Alikuwa juu- mlingano unaonasibiana na utukufu na ukubwa Wake. Yeye , kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Anauingiza usiku kwenye mchana ukaufinika mpaka mwangaza wake ukaondoka, na Anauingiza usiku kwenye mchana mpaka giza lake likaondoka. Na daima kila mojawapo, kati ya viwili hivyi, kinafuata kingine kwa kasi. Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyeumba jua, mwezi na nyota zikiwa zinamtii Yeye, Anazipelekesha, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, vile Anavyotaka, nazo ni miongoni mwa alama kubwa za Mwenyezi Mungu. Jua utanabahi kwamba ni wake Yeye, kutakasika na sifa za upungufu na kutukuka ni Kwake, uumbaji wote, na ni Yake Yeye amri yote. Ametukuka Mwenyezi Mungu, umeendelea ukuu Wake na Ameepukana na kila upungufu, Bwana wa viumbe wote.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 段: (54) 章: 艾尔拉夫
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。 - 译解目录

古兰经斯瓦希里文译解,阿布杜拉·穆罕默德·艾布·拜克尔博士和谢赫纳赛尔·哈米斯翻译。

关闭