《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 * - 译解目录

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

含义的翻译 段: (22) 章: 优努斯
هُوَ ٱلَّذِي يُسَيِّرُكُمۡ فِي ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا كُنتُمۡ فِي ٱلۡفُلۡكِ وَجَرَيۡنَ بِهِم بِرِيحٖ طَيِّبَةٖ وَفَرِحُواْ بِهَا جَآءَتۡهَا رِيحٌ عَاصِفٞ وَجَآءَهُمُ ٱلۡمَوۡجُ مِن كُلِّ مَكَانٖ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُمۡ أُحِيطَ بِهِمۡ دَعَوُاْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ لَئِنۡ أَنجَيۡتَنَا مِنۡ هَٰذِهِۦ لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّٰكِرِينَ
Yeye ndiye anaye kuendesheni bara na baharini. Hata mnapo kuwa majahazini na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakaufurahia, upepo mkali ukawazukia, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakaona wameshazongwa, basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia niya: Ukituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru.
Mwenyezi Mungu mnaye ikufuru neema yake, na mnakanusha Ishara zake, ndiye Yeye anaye kuezesheni kwenda na kutembea nchi kavu kwa miguu au kwa vipando, na baharini kwa vyombo alivyo fanya vikutumikieni, vinavyo kwenda juu ya maji, kama anavyo visahilishia Mwenyezi Mungu kwa upepo mzuri unao puliza kwa amani mpaka kufikilia huko vyendako. Hata mkisha tumaini na mkafurahia huvuma tena upepo mkali ukatibua mawimbi kutoka kila upande, na mkayakinika kuwa hapana ila kuhiliki tu! Katika shida kama hii hamna tegemeo ila Mwenyezi Mungu. Hapo basi mnamwomba madua kwa usafi wa niya, kwa kuyakinika kuwa hapana mwokozi isipo kuwa Yeye, na mnampa ahadi kuwa pindi akikuvueni na balaa hiyo mtamuamini, na mtakuwa wenye kushukuru.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 段: (22) 章: 优努斯
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 - 译解目录

古兰经斯瓦希里语译解,阿里·穆哈森·伯瓦尼翻译

关闭