Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 * - 译解目录

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

含义的翻译 章: 哈吉拉   段:
ٱلَّذِينَ جَعَلُواْ ٱلۡقُرۡءَانَ عِضِينَ
Ambao wakaifanya Qur'ani vipande vipande. [91]
[91] Hao waliifanya Qur'ani vipande mbali mbali, nayo hali kuwa haikubali kugawika kwa umuujiza wake na ukweli wake.
阿拉伯语经注:
فَوَرَبِّكَ لَنَسۡـَٔلَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Basi Naapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawahoji wote. [92]
[92] Ikiwa hiyo hali yao, basi Wallahi kwa Aliye kuumba akakulinda na akakulea, hapana shaka tutawahisabu wote Siku ya Kiyama,
阿拉伯语经注:
عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Kwa waliyo kuwa wakiyatenda. [93]
[93] Kwa vitendo vyao vya kuudhi, na kufuru, na kejeli.
阿拉伯语经注:
فَٱصۡدَعۡ بِمَا تُؤۡمَرُ وَأَعۡرِضۡ عَنِ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Basi wewe yatangaze uliyo amrishwa, na jitenge na washirikina. [94]
[94] Basi wewe tangaza wito wa Haki, wala usishughulike na wayatendao washirikina na maneno yao.
阿拉伯语经注:
إِنَّا كَفَيۡنَٰكَ ٱلۡمُسۡتَهۡزِءِينَ
Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanao kejeli. [95]
[95] Na hao washirikina wanao ukejeli wito wako hawatokushinda, wala hawatoweza kukuingilia kati baina yako na wito wako.
阿拉伯语经注:
ٱلَّذِينَ يَجۡعَلُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۚ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ
Hao wanao fanya kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu yupo mungu mwingine.Basi, watakuja jua! [96]
[96] Hao washirikina mawazo yao yamedhoofika, ndio wakafanya kuwa Mwenyezi Mungu anao miungu mingine ya masanamu. Na watakuja jua matokeo ya ushirikina wao itapo wateremkia adhabu chungu.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ نَعۡلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدۡرُكَ بِمَا يَقُولُونَ
Na Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo. [97]
[97] Nasi tunajua dhiki ya moyo inayo kupata kwa wanayo yasema ya ushirikina na kejeli na dharau.
阿拉伯语经注:
فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ ٱلسَّٰجِدِينَ
Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni wanaomsujudia. [98]
[98] Ikikupata dhiki hiyo mkimbilie Mwenyezi Mungu Mtukufu umwelekee, na umt'ii na umnyenyekee, na utake msaada kwa Sala, kwani humo ndio imo poza.
阿拉伯语经注:
وَٱعۡبُدۡ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأۡتِيَكَ ٱلۡيَقِينُ
Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini. (nao ni Mauti) [99]
[99] Na shikilia ibada ya Mwenyezi Mungu aliye kuumba, akakulinda, mpaka ifike amri ya yakini, nayo ni Mauti.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 哈吉拉
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 - 译解目录

阿里·穆哈森·伯瓦尼翻译。

关闭