《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 * - 译解目录

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

含义的翻译 段: (28) 章: 嘎推勒
وَمِنَ ٱلنَّاسِ وَٱلدَّوَآبِّ وَٱلۡأَنۡعَٰمِ مُخۡتَلِفٌ أَلۡوَٰنُهُۥ كَذَٰلِكَۗ إِنَّمَا يَخۡشَى ٱللَّهَ مِنۡ عِبَادِهِ ٱلۡعُلَمَٰٓؤُاْۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ
Na katika watu, na wanyama, na mifugo, pia rangi zao zinakhitalifiana. Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe.
Na miongoni mwa watu na wanyama, na mifugo, yaani ngamia, ng'ombe, kondoo na mbuzi, kadhaalika zipo khitilafu katika sura, ukubwa na rangi. Na hawazingatii huu muumbo wa ajabu na wakamwogopa aliye umba ila wanazuoni ambao wanatambua siri ya uumbaji wake. Hakika Mwenyezi Mungu Mwenye kushinda anaogopwa na Waumini, naye ni Mwingi wa kuwafutia madhambi yao wanao rejea kwake. Baada ya kueleza kukhitalifiana matunda, na milima, na watu, na wanyama, na mifugo, inaashiriwa kuwa juu ya khitilafu hizi zinazo onekana baina ya hali hizi zote, upo umoja wa asli. Kwani hayo matunda yanatokana na maji yale yale. Na milima inatokana na Magma moja. Kadhaalika khitilafu za rangi, na watu, na wanyama, na mifugo, hazidhihiri katika tone za manii ambavyo vyote hivyo vimetoka mwanzo wake. Na lau hizo tone zingeli chunguzwa kwa darubini ya Maikroskopu kisingeli onekana kitu cha kuonyesha hizo khitilafu zitazo kuwa. Kwani hizo ni siri zilioko ndani yake katika zinazo itwa Genes (Jiinz). Na labda haya pia yanaonyesha kuwa sifa za kurithi ziliomo katika asli ya mimea, na wanyama, na binaadamu, zinalindwa katika maumbile yake, na hazigeuki kwa tabia ya pahala au chakula.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 段: (28) 章: 嘎推勒
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 - 译解目录

古兰经斯瓦希里语译解,阿里·穆哈森·伯瓦尼翻译

关闭