Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 * - 译解目录

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

含义的翻译 章: 穆扎底拉   段:
أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ مَا يَكُونُ مِن نَّجۡوَىٰ ثَلَٰثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمۡ وَلَا خَمۡسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمۡ وَلَآ أَدۡنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمۡ أَيۡنَ مَا كَانُواْۖ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُواْ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٌ
Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi? Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wane wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawaambia waliyo yatenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Kwani hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo mbinguni na yaliomo katika ardhi, na wala hapana siri ya watu watatu ila Yeye Mwenyezi Mungu ndiye wane wao kwa kuyajua kwake wanayo fanyia siri, wala hawawi watano ila na Yeye ndiye wa sita wao. Wala duni kuliko hivyo, wala kuzidi hivyo, ila Yeye yuko pamoja nao, anayajua hayo wanayo yanong'ona, popote walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawapa khabari kwa kila walilo litenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutimia ujuzi wake.
阿拉伯语经注:
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ نُهُواْ عَنِ ٱلنَّجۡوَىٰ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا نُهُواْ عَنۡهُ وَيَتَنَٰجَوۡنَ بِٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِ وَمَعۡصِيَتِ ٱلرَّسُولِۖ وَإِذَا جَآءُوكَ حَيَّوۡكَ بِمَا لَمۡ يُحَيِّكَ بِهِ ٱللَّهُ وَيَقُولُونَ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ لَوۡلَا يُعَذِّبُنَا ٱللَّهُ بِمَا نَقُولُۚ حَسۡبُهُمۡ جَهَنَّمُ يَصۡلَوۡنَهَاۖ فَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ
Kwani huwaoni wale walio katazwa kunong'onezana kisha wakayarudia yale yale waliyo katazwa, na wakanong'ona juu ya mambo ya dhambi, na ya uadui, na ya kumuasi Mtume? Na wakikujia hukuamkia sivyo anavyo kuamkia Mwenyezi Mungu. Na husema katika nafsi zao: Mbona Mwenyezi hatuadhibu kwa haya tuyasemayo? Basi Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Na hayo ndiyo marejeo maovu yaliyoje!
Ewe Mtume! Huwaoni hao walio katazwa kufanya njama za siri wao kwa wao kwa mambo ya kutia shaka katika nyoyo za Waumini, kisha wakayarejea yale yale waliyo katazwa? Na wanafanya njama kwa madhambi wanayo yatenda, na uadui wanao uazimia, na uasi dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na wanapo kuja kwako wanakuamkia kwa kauli ya kupotoa, sivyo anavyo kuamkia Mwenyezi Mungu. Na wao husema katika nafsi zao: Mbona Mwenyezi Mungu hatuadhibu kwa haya tunayo yasema ikiwa huyu ni Mtume kweli? Inawatosha hao Jahannamu. Wataingia humo waungue kwa moto wake. Na marejeo maovu yalioje marejeo yao. Ilikuwako sulhu baina ya Waislamu na Mayahudi katika mji wa Madina. Na ikawa akipita mtu katika Waislamu kwao Mayahudi hunong'ona wao kwa wao ili adhani yule Muislamu kuwa wao wanapanga njama za kutaka kumuuwa, au lolote la kumdhuru apate kugeuza njia asiwapitie tena. Mtume s.a.w. akawakataza hayo, lakini hawakuacha mtindo wao, wakayarejea yale yale waliyo katazwa. Na wakawa akija Mtume s.a.w. wakimwamkia kwa maamkio ya kumuapiza. Ndiyo ikashuka Aya hii.
阿拉伯语经注:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا تَنَٰجَيۡتُمۡ فَلَا تَتَنَٰجَوۡاْ بِٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِ وَمَعۡصِيَتِ ٱلرَّسُولِ وَتَنَٰجَوۡاْ بِٱلۡبِرِّ وَٱلتَّقۡوَىٰۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِيٓ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ
Enyi mlio amini! Mnapo nong'ona msinong'one kwa sababu ya mambo ya madhambi, na uadui, na kumuasi Mtume. Bali nong'onezane kwa kutenda mema na kuacha maovu. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwake mtakusanywa nyote.
Enyi mlio msadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake! Mnapo sema siri, basi msiwe mkisema siri katika mambo ya madhambi, na kufanya uadui, na kwenda kinyume na Mtume. Semeni siri katika mambo ya kheri, na kuepukana na madhambi. Na mwogopeni Mwenyezi Mungu ambaye kwake Yeye tu, si kwengineko, ndio mtakusanywa baada ya kufufuliwa.
阿拉伯语经注:
إِنَّمَا ٱلنَّجۡوَىٰ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ لِيَحۡزُنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَلَيۡسَ بِضَآرِّهِمۡ شَيۡـًٔا إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ
Kwa hakika minong'ono hiyo inatokana na Shetani ili awahuzunishe walio amini, na wala haitawadhuru chochote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na juu ya Mwenyezi Mungu tu ndio wategemee Waumini.
Hakika kusema siri kwa kuchochea shaka shaka ni katika kuzainishwa na Shetani, ili apate kuingiza huzuni katika nyoyo za Waumini. Wala hayo hayawezi kuwaletea madhara yoyote wao ila kwa kupenda Mwenyezi Mungu. Basi Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu peke yake.
阿拉伯语经注:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا قِيلَ لَكُمۡ تَفَسَّحُواْ فِي ٱلۡمَجَٰلِسِ فَٱفۡسَحُواْ يَفۡسَحِ ٱللَّهُ لَكُمۡۖ وَإِذَا قِيلَ ٱنشُزُواْ فَٱنشُزُواْ يَرۡفَعِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنكُمۡ وَٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ دَرَجَٰتٖۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ
Enyi mlio amini! Mkiambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atakufanyieni nyinyi nafasi. Na mkiambiwa: Ondokeni, basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua walio amini miongoni mwenu, na walio pewa ilimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.
Enyi mlio msadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake! Mkitakiwa baadhi yenu kuwafanyia nafasi wenzenu mnapo kaa katika majlisi zenu, basi wafanyieni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atakufanyieni nyinyi nafasi. Na mkitakiwa kuondoka pale mlipo kaa basi ondokeni. Mwenyezi Mungu hutukuza vyeo vya Waumini, na wale walio pewa ilimu kwa daraja nyingi. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 穆扎底拉
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 - 译解目录

阿里·穆哈森·伯瓦尼翻译。

关闭