Wakikukanusha basi wewe sema: Mola Mlezi wenu ni Mwenye rehema iliyo enea. Wala haizuiliki adhabu yake kwa watu wakhalifu.
Wakanushi wakikukanusha katika haya tuliyo kuletea wahyi, waambie kwa kuwahadharisha: Hakika Mola Mlezi wenu, ambaye anapasa mumuamini Yeye peke yake, na mfuate hukumu zake, ana rehema iliyo enea na kumfikia kila anaye mt'ii, na pia anaye muasi kwa kuwa hafanyi haraka kuwaadhibu. Na lakini haitakikani mghurike na hivyo kuwa rehema yake imeenea kote, kwa sababu adhabu yake haina budi kuwafikia hao wakhalifu.
Watasema walio shirikisha: Lau kuwa Mwenyezi Mungu ange taka tusingeli shiriki sisi, wala baba zetu; wala tusingeli harimisha kitu chochote. Vivi hivi walikanusha walio kuwa kabla yao mpaka walipo onja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo ilimu mtutolee? Nyinyi hamfuati ila dhana. Wala hamsemi ila uwongo tu.
Kwa kutaka kujitolea udhuru kwa ushiriki wao, na kule kuharimisha vyakula alivyo halalisha Mwenyezi Mungu, na kukanusha yaliyo wafikia kuwa Mwenyezi Mungu kaudhika nao kwa vitendo vyao, washirikina watasema: Ushirikina wetu na kuharimisha alicho halalisha Mwenyezi Mungu, ni kwa mujibu wa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuridhi kwake! Na lau angeli penda Yeye kinyume cha hayo, na angeli chukia tuyatendayo, basi tusingeli mshirikisha sisi wala walio tutangulia, na wala tusingeli harimisha kitu chochote alicho tuhalalishia. Na walio kabla yao waliwakadhibisha Mitume wao, kama hawa wanavyo kukadhibisha wewe. Na waliendelea katika kukanusha kwao mpaka ikawafikia adhabu yetu! Waambie hawa wanao kanusha: Jee mnao ushahidi wa kutegemea ulio sahihi ya kwamba Mwenyezi Mungu amekuridhieni nyinyi mumshirikishe na mhalalishe, mkatutolea? Katika maneno yenu hamfuati ila kudhania tu. Na hiyo haitoshelezi chochote katika Haki. Na nyinyi si chochote, si lolote, ila ni waongo tu katika hayo mnayo dai.
Sema: Basi Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye hoja ya kukata. Na kama angeli penda angeli kuhidini nyote.
Ewe Nabii! Sema: Mwenyezi Mungu ana hoja iliyo wazi kuwa nyinyi ni waongo katika madai yenu kuwa Mwenyezi Mungu ameridhia vitendo vyenu! Wala hamna hoja katika ushirikina wenu, na kuhalalisha kwenu, na kuharimisha kwenu, na mengineyo. Na Mwenyezi Mungu angeli taka mhidike angeli kuhidini nyote mkafuata Njia ya Haki. Lakini hakutaka hayo kwa kuwa nyinyi mmekhiari njia ya upotovu.
Sema: Leteni mashahidi wenu watao shuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ameharimisha hawa. Basi wakishuhudia, wewe usishuhudie pamoja nao. Wala usifuate matamanio ya walio zikanusha Ishara zetu, wala hawaiamini Akhera, na ambao wanamlinganisha Mola Mlezi wao na wengine.
Ewe Nabii! Waambie: Leteni wasaidizi wenu watakao kushuhudieni kwamba kweli Mwenyezi Mungu ameharimisha hivi mnavyo dai kuwa ni haramu. Wakihudhuria na wakashuhudia, basi wewe usiawasadiki, kwa sababu hao ni waongo. Wala usifuate matamanio ya hawa walio kanusha hoja za uumbaji na Qur'ani inayo somwa, na ambao hawaiamini Akhera nao wanamshirikisha Mwenyezi Mungu, wanamfanya Yeye sawa na hao miungu inayo abudiwa kwa uwongo.
Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini.
Ewe Nabii! Waambie: Njooni nikubainishieni yaliyo haramu ambayo inatakikana mshughulike nayo, na mjitenge nayo. Msimfanye yeyote kuwa ni mshirika na Mwenyezi Mungu, kwa shirki ya namna yoyote. Wala msiwafanye uovu wazazi wenu, bali wafanyieni wema mwisho wa wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya kukufikieni ufakiri, au mnao ogopa usikufikieni siku za usoni. Kwani nyinyi sio mnao toa riziki. Bali Sisi ndio tunakuruzukuni nyinyi na tunawaruzuku wao. Wala msikaribie uchafu wa uzinzi, kwani huo ni katika mambo mabaya yanayo katazwa, sawa sawa ikiwa jahara au kwa siri asiyo iona ila Mwenyezi Mungu. Wala msiuwe nafsi yoyote aliyo kataza Mwenyezi Mungu kuiuwa kwa kutokuwapo kupasa kwake, ila ikiwa kuuwa huko ni kwa haki ya kutekeleza hukumu ya mahkama. Mwenyezi Mungu amekuamrisheni kwa amri ya nguvu muepuke haya yaliyo katazwa ambayo akili ya maumbile inakwambieni muepukane nayo, ili nanyi myatie akilini hayo.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
搜索结果:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".