《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 * - 译解目录

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

含义的翻译 段: (141) 章: 艾奈尔姆
۞ وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَ جَنَّٰتٖ مَّعۡرُوشَٰتٖ وَغَيۡرَ مَعۡرُوشَٰتٖ وَٱلنَّخۡلَ وَٱلزَّرۡعَ مُخۡتَلِفًا أُكُلُهُۥ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُتَشَٰبِهٗا وَغَيۡرَ مُتَشَٰبِهٖۚ كُلُواْ مِن ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثۡمَرَ وَءَاتُواْ حَقَّهُۥ يَوۡمَ حَصَادِهِۦۖ وَلَا تُسۡرِفُوٓاْۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡرِفِينَ
Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.
Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye umba bustani za matunda. Ipo miti inayo pandwa na kuegemezwa juu ya chanja, na ipo isiyo hitajia chanja. Na ameumba mitende, na mimea mingine inayo toa matunda yanayo khitalifiana kwa rangi, na utamu, na sura, na harufu na mengineyo. Na ameumba mizaituni, na makomamanga (makudhumani), yenye kushabihiana katika baadhi ya sifa zake, na isiyo shabihiana, ijapo kuwa udongo huenda ukawa ule ule, na yote ikawa inanyweshwa na maji yale yale. Basi kuleni matunda yake mkipenda, na toeni sadaka yake yanapo wiva na kuyachuma. Wala msifanye fujo katika kula, mkajidhuru wenyewe, na mkawadhuru mafakiri katika kuwanyima haki yao. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi watumiao kwa fujo, katika mwendo wao na vitendo vyao.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 段: (141) 章: 艾奈尔姆
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 - 译解目录

古兰经斯瓦希里语译解,阿里·穆哈森·伯瓦尼翻译

关闭