Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 * - 译解目录


含义的翻译 章: 优努斯   段:
وَلَوۡ أَنَّ لِكُلِّ نَفۡسٖ ظَلَمَتۡ مَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لَٱفۡتَدَتۡ بِهِۦۗ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَۖ وَقُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ
Na lau kuwa kila nafsi iliyodhulumu inamiliki kila kilichomo katika ardhi, basi bila ya shaka ingejikomboa kwavyo. Na watakapoiona adhabu, wataficha majuto. Na itahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa.
阿拉伯语经注:
أَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ أَلَآ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Jueni kuwa hakika ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Jueni kuwa hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Lakini wengi wao hawajui.
阿拉伯语经注:
هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
Yeye ndiye anayehuisha na anayefisha. Na kwake mtarejeshwa.
阿拉伯语经注:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَتۡكُم مَّوۡعِظَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَشِفَآءٞ لِّمَا فِي ٱلصُّدُورِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ
Enyi watu! Yamekwisha wajia mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na poza ya yale yaliyo katika vifua, na uwongofu, na rehema kwa Waumini.
阿拉伯语经注:
قُلۡ بِفَضۡلِ ٱللَّهِ وَبِرَحۡمَتِهِۦ فَبِذَٰلِكَ فَلۡيَفۡرَحُواْ هُوَ خَيۡرٞ مِّمَّا يَجۡمَعُونَ
Sema, "Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi na wafurahi kwa hayo. Hayo ndiyo bora kuliko hayo wanayoyakusanya.
阿拉伯语经注:
قُلۡ أَرَءَيۡتُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ لَكُم مِّن رِّزۡقٖ فَجَعَلۡتُم مِّنۡهُ حَرَامٗا وَحَلَٰلٗا قُلۡ ءَآللَّهُ أَذِنَ لَكُمۡۖ أَمۡ عَلَى ٱللَّهِ تَفۡتَرُونَ
Sema: Je, munaonaje yale aliyowateremshia Mwenyezi Mungu katika zile riziki, basi mkafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali. Sema, "Je, Mwenyezi Mungu aliwaruhusu, au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu?"
阿拉伯语经注:
وَمَا ظَنُّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَشۡكُرُونَ
Na ni nini dhana ya wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu uongo Siku ya Qiyama? Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru.
阿拉伯语经注:
وَمَا تَكُونُ فِي شَأۡنٖ وَمَا تَتۡلُواْ مِنۡهُ مِن قُرۡءَانٖ وَلَا تَعۡمَلُونَ مِنۡ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيۡكُمۡ شُهُودًا إِذۡ تُفِيضُونَ فِيهِۚ وَمَا يَعۡزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثۡقَالِ ذَرَّةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِي ٱلسَّمَآءِ وَلَآ أَصۡغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡبَرَ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٍ
Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur-ani, wala hamtendi kitendo chochote isipokuwa Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa isipokuwa kimo katika Kitabu kilicho wazi.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 优努斯
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 - 译解目录

由拉瓦德翻译中心团队与拉布瓦 الدعوة协会和伊斯兰内容服务协会合作翻译。

关闭