Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 * - 译解目录


含义的翻译 章: 麦尔彦   段:

Maryam

كٓهيعٓصٓ
Kaf Ha Ya 'Ayn Swad.[1]
[1] Herufi hizi "Kaf Ha Ya 'Ayn Swad" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
阿拉伯语经注:
ذِكۡرُ رَحۡمَتِ رَبِّكَ عَبۡدَهُۥ زَكَرِيَّآ
Huu ni ukumbusho wa rehema ya Mola wako Mlezi kwa mja wake, Zakariya.
阿拉伯语经注:
إِذۡ نَادَىٰ رَبَّهُۥ نِدَآءً خَفِيّٗا
Alipomwita Mola wake Mlezi kwa siri.
阿拉伯语经注:
قَالَ رَبِّ إِنِّي وَهَنَ ٱلۡعَظۡمُ مِنِّي وَٱشۡتَعَلَ ٱلرَّأۡسُ شَيۡبٗا وَلَمۡ أَكُنۢ بِدُعَآئِكَ رَبِّ شَقِيّٗا
Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi, mifupa yangu imedhoofika, na kichwa kinametameta kwa mvi; wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe.
阿拉伯语经注:
وَإِنِّي خِفۡتُ ٱلۡمَوَٰلِيَ مِن وَرَآءِي وَكَانَتِ ٱمۡرَأَتِي عَاقِرٗا فَهَبۡ لِي مِن لَّدُنكَ وَلِيّٗا
Na hakika mimi ninawahofia wasimamizi wa baada yangu. Na mke wangu ni tasa. Basi nitunuku mrithi kutoka kwako.
阿拉伯语经注:
يَرِثُنِي وَيَرِثُ مِنۡ ءَالِ يَعۡقُوبَۖ وَٱجۡعَلۡهُ رَبِّ رَضِيّٗا
Anirithi na awarithi ukoo wa Yaaqub. Na umjaalie ewe Mola wangu Mlezi awe mwenye kuridhisha.
阿拉伯语经注:
يَٰزَكَرِيَّآ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَٰمٍ ٱسۡمُهُۥ يَحۡيَىٰ لَمۡ نَجۡعَل لَّهُۥ مِن قَبۡلُ سَمِيّٗا
(Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi tunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya. Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake.
阿拉伯语经注:
قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَٰمٞ وَكَانَتِ ٱمۡرَأَتِي عَاقِرٗا وَقَدۡ بَلَغۡتُ مِنَ ٱلۡكِبَرِ عِتِيّٗا
Akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Vipi nitakuwa na mwana na ilhali mke wangu ni tasa, na mimi nimeshafikia ukongwe katika uzee?
阿拉伯语经注:
قَالَ كَذَٰلِكَ قَالَ رَبُّكَ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٞ وَقَدۡ خَلَقۡتُكَ مِن قَبۡلُ وَلَمۡ تَكُ شَيۡـٔٗا
Akasema: Hivyo ndivyo alivyosema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu. Na hakika Mimi nilikwishakuumba wewe zamani na wala hukuwa kitu.
阿拉伯语经注:
قَالَ رَبِّ ٱجۡعَل لِّيٓ ءَايَةٗۖ قَالَ ءَايَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ ٱلنَّاسَ ثَلَٰثَ لَيَالٖ سَوِيّٗا
Akasema: Mola wangu Mlezi nijaalie Ishara. Akasema: Ishara yako ni kuwa hutasema na watu kwa usiku tatu, na ilhali u mzima sawasawa.
阿拉伯语经注:
فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوۡمِهِۦ مِنَ ٱلۡمِحۡرَابِ فَأَوۡحَىٰٓ إِلَيۡهِمۡ أَن سَبِّحُواْ بُكۡرَةٗ وَعَشِيّٗا
Basi akawatokea kaumu yake kutoka mihirabuni. Akawaashiria kwamba: Msabihini Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni.
阿拉伯语经注:
يَٰيَحۡيَىٰ خُذِ ٱلۡكِتَٰبَ بِقُوَّةٖۖ وَءَاتَيۡنَٰهُ ٱلۡحُكۡمَ صَبِيّٗا
Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hekima angali mtoto.
阿拉伯语经注:
وَحَنَانٗا مِّن لَّدُنَّا وَزَكَوٰةٗۖ وَكَانَ تَقِيّٗا
Na tukampa huruma itokayo kwetu, na utakaso, na akawa mcha Mungu.
阿拉伯语经注:
وَبَرَّۢا بِوَٰلِدَيۡهِ وَلَمۡ يَكُن جَبَّارًا عَصِيّٗا
Na akawa mwema kwa wazazi wake, wala hakuwa jabari muasi.
阿拉伯语经注:
وَسَلَٰمٌ عَلَيۡهِ يَوۡمَ وُلِدَ وَيَوۡمَ يَمُوتُ وَيَوۡمَ يُبۡعَثُ حَيّٗا
Na salama iwe juu yake siku ya kuzaliwa, na siku ya kufa, na siku ya kufufuliwa.
阿拉伯语经注:
وَٱذۡكُرۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ مَرۡيَمَ إِذِ ٱنتَبَذَتۡ مِنۡ أَهۡلِهَا مَكَانٗا شَرۡقِيّٗا
Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipojitenga mbali na jamaa zake mahali upande wa mashariki.
阿拉伯语经注:
فَٱتَّخَذَتۡ مِن دُونِهِمۡ حِجَابٗا فَأَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرٗا سَوِيّٗا
Na akaweka pazia kujikinga nao. Basi tukamtumia Roho wetu, naye akajifananisha kwake sawa sawa na mtu.
阿拉伯语经注:
قَالَتۡ إِنِّيٓ أَعُوذُ بِٱلرَّحۡمَٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيّٗا
(Maryamu) akasema: Hakika mimi ninajikinga kwa Mwingi wa rehema aniepushe nawe, ikiwa wewe ni mcha Mungu.
阿拉伯语经注:
قَالَ إِنَّمَآ أَنَا۠ رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَٰمٗا زَكِيّٗا
(Malaika huyo) akasema: Hakika mimi ni mtume tu kutoka kwa Mola wako Mlezi ili nikutunuku mwana aliyetakasika.
阿拉伯语经注:
قَالَتۡ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَٰمٞ وَلَمۡ يَمۡسَسۡنِي بَشَرٞ وَلَمۡ أَكُ بَغِيّٗا
Akasema: Nitampataje mwana ilhali mtu yeyote hajawahi kunigusa, wala sikuwahi kuwa kahaba?
阿拉伯语经注:
قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٞۖ وَلِنَجۡعَلَهُۥٓ ءَايَةٗ لِّلنَّاسِ وَرَحۡمَةٗ مِّنَّاۚ وَكَانَ أَمۡرٗا مَّقۡضِيّٗا
(Malaika) akasema: Hivyo ndiyo alivyosema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na rehema kutoka kwetu, na hilo ni jambo lililokwishahukumiwa.
阿拉伯语经注:
۞ فَحَمَلَتۡهُ فَٱنتَبَذَتۡ بِهِۦ مَكَانٗا قَصِيّٗا
Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali.
阿拉伯语经注:
فَأَجَآءَهَا ٱلۡمَخَاضُ إِلَىٰ جِذۡعِ ٱلنَّخۡلَةِ قَالَتۡ يَٰلَيۡتَنِي مِتُّ قَبۡلَ هَٰذَا وَكُنتُ نَسۡيٗا مَّنسِيّٗا
Kisha uchungu wa kuzaa ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya, na nikawa niliyesahaulika kabisa!
阿拉伯语经注:
فَنَادَىٰهَا مِن تَحۡتِهَآ أَلَّا تَحۡزَنِي قَدۡ جَعَلَ رَبُّكِ تَحۡتَكِ سَرِيّٗا
Kwa hivyo, akamnadi kutokea chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi ameshafanya chini yako kijito kidogo cha maji!
阿拉伯语经注:
وَهُزِّيٓ إِلَيۡكِ بِجِذۡعِ ٱلنَّخۡلَةِ تُسَٰقِطۡ عَلَيۡكِ رُطَبٗا جَنِيّٗا
Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.
阿拉伯语经注:
فَكُلِي وَٱشۡرَبِي وَقَرِّي عَيۡنٗاۖ فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ ٱلۡبَشَرِ أَحَدٗا فَقُولِيٓ إِنِّي نَذَرۡتُ لِلرَّحۡمَٰنِ صَوۡمٗا فَلَنۡ أُكَلِّمَ ٱلۡيَوۡمَ إِنسِيّٗا
Basi kula, na kunywa, na litulize jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote, basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa rehema, ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu yeyote.
阿拉伯语经注:
فَأَتَتۡ بِهِۦ قَوۡمَهَا تَحۡمِلُهُۥۖ قَالُواْ يَٰمَرۡيَمُ لَقَدۡ جِئۡتِ شَيۡـٔٗا فَرِيّٗا
Basi akaenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu sana!
阿拉伯语经注:
يَٰٓأُخۡتَ هَٰرُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ ٱمۡرَأَ سَوۡءٖ وَمَا كَانَتۡ أُمُّكِ بَغِيّٗا
Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu mbaya, wala mama yako hakuwa kahaba.
阿拉伯语经注:
فَأَشَارَتۡ إِلَيۡهِۖ قَالُواْ كَيۡفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي ٱلۡمَهۡدِ صَبِيّٗا
Kwa hivyo, akamuashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeshe aliye bado mtoto mdogo yumo katika mlezi?
阿拉伯语经注:
قَالَ إِنِّي عَبۡدُ ٱللَّهِ ءَاتَىٰنِيَ ٱلۡكِتَٰبَ وَجَعَلَنِي نَبِيّٗا
(Mtoto huyo) akasema: Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii.
阿拉伯语经注:
وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيۡنَ مَا كُنتُ وَأَوۡصَٰنِي بِٱلصَّلَوٰةِ وَٱلزَّكَوٰةِ مَا دُمۡتُ حَيّٗا
Na amenifanya ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Swala na Zaka maadamu ni hai.
阿拉伯语经注:
وَبَرَّۢا بِوَٰلِدَتِي وَلَمۡ يَجۡعَلۡنِي جَبَّارٗا شَقِيّٗا
Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu.
阿拉伯语经注:
وَٱلسَّلَٰمُ عَلَيَّ يَوۡمَ وُلِدتُّ وَيَوۡمَ أَمُوتُ وَيَوۡمَ أُبۡعَثُ حَيّٗا
Na amani iko juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayokufa, na siku nitakayofufuliwa kuwa hai.
阿拉伯语经注:
ذَٰلِكَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَۖ قَوۡلَ ٱلۡحَقِّ ٱلَّذِي فِيهِ يَمۡتَرُونَ
Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.
阿拉伯语经注:
مَا كَانَ لِلَّهِ أَن يَتَّخِذَ مِن وَلَدٖۖ سُبۡحَٰنَهُۥٓۚ إِذَا قَضَىٰٓ أَمۡرٗا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ
Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kujifanyia mwana, Subhanahu (Yeye ametakasika)! Anapolihukumia jambo, basi hakika huliambia tu: "Kuwa!" Na linakuwa.
阿拉伯语经注:
وَإِنَّ ٱللَّهَ رَبِّي وَرَبُّكُمۡ فَٱعۡبُدُوهُۚ هَٰذَا صِرَٰطٞ مُّسۡتَقِيمٞ
Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Hii ndiyo njia iliyonyooka.
阿拉伯语经注:
فَٱخۡتَلَفَ ٱلۡأَحۡزَابُ مِنۢ بَيۡنِهِمۡۖ فَوَيۡلٞ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن مَّشۡهَدِ يَوۡمٍ عَظِيمٍ
Lakini makundi yakahitilafiana wao kwa wao. Basi ole wao hao waliokufuru kwa kuhudhuria Siku iliyo kuu!
阿拉伯语经注:
أَسۡمِعۡ بِهِمۡ وَأَبۡصِرۡ يَوۡمَ يَأۡتُونَنَا لَٰكِنِ ٱلظَّٰلِمُونَ ٱلۡيَوۡمَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ
Watasikia na wataona vizuri vilivyoje Siku watakayotujia! Lakini madhalimu sasa wamo katika upotovu ulio dhahiri.
阿拉伯语经注:
وَأَنذِرۡهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡحَسۡرَةِ إِذۡ قُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ وَهُمۡ فِي غَفۡلَةٖ وَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ
Na waonye siku ya majuto makubwa itapokatwa amri. Nao wako katika ghafla, wala hawaamini.
阿拉伯语经注:
إِنَّا نَحۡنُ نَرِثُ ٱلۡأَرۡضَ وَمَنۡ عَلَيۡهَا وَإِلَيۡنَا يُرۡجَعُونَ
Hakika Sisi ndio tutairithi ardhi na wale walio juu yake. Na kwetu watarejeshwa.
阿拉伯语经注:
وَٱذۡكُرۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ إِبۡرَٰهِيمَۚ إِنَّهُۥ كَانَ صِدِّيقٗا نَّبِيًّا
Na mtaje katika Kitabu hiki Ibrahim. Hakika yeye alikuwa mkweli mno, na Nabii.
阿拉伯语经注:
إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ يَٰٓأَبَتِ لِمَ تَعۡبُدُ مَا لَا يَسۡمَعُ وَلَا يُبۡصِرُ وَلَا يُغۡنِي عَنكَ شَيۡـٔٗا
Alipomwambia baba yake: Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu visivyosikia, na visivyoona, na visivyokufaa chochote?
阿拉伯语经注:
يَٰٓأَبَتِ إِنِّي قَدۡ جَآءَنِي مِنَ ٱلۡعِلۡمِ مَا لَمۡ يَأۡتِكَ فَٱتَّبِعۡنِيٓ أَهۡدِكَ صِرَٰطٗا سَوِيّٗا
Ewe baba yangu! Kwa yakini imenifikia elimu ambayo haikukujia wewe. Basi nifuate mimi, nami nitakuongoza njia iliyo sawa.
阿拉伯语经注:
يَٰٓأَبَتِ لَا تَعۡبُدِ ٱلشَّيۡطَٰنَۖ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ كَانَ لِلرَّحۡمَٰنِ عَصِيّٗا
Ewe baba yangu! Usimuabudu Shetani. Hakika Shetani ni mwenye kumuasi sana Mwingi wa rehema.
阿拉伯语经注:
يَٰٓأَبَتِ إِنِّيٓ أَخَافُ أَن يَمَسَّكَ عَذَابٞ مِّنَ ٱلرَّحۡمَٰنِ فَتَكُونَ لِلشَّيۡطَٰنِ وَلِيّٗا
Ewe baba yangu! Hakika mimi ninahofu ije kukupata adhabu inayotoka kwa Mwingi wa rehema, ukaja kuwa mwenziwe Shetani.
阿拉伯语经注:
قَالَ أَرَاغِبٌ أَنتَ عَنۡ ءَالِهَتِي يَٰٓإِبۡرَٰهِيمُۖ لَئِن لَّمۡ تَنتَهِ لَأَرۡجُمَنَّكَۖ وَٱهۡجُرۡنِي مَلِيّٗا
(Baba) akasema: Je huitaki miungu yangu, ewe Ibrahim? Kama huachi, basi lazima nitakupiga mawe. Na niondokee mbali kwa muda!
阿拉伯语经注:
قَالَ سَلَٰمٌ عَلَيۡكَۖ سَأَسۡتَغۡفِرُ لَكَ رَبِّيٓۖ إِنَّهُۥ كَانَ بِي حَفِيّٗا
(Ibrahim) akasema: Salamun 'alaika (Amani iwe juu yako)! Mimi nitakuombea msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ananihurumia sana.
阿拉伯语经注:
وَأَعۡتَزِلُكُمۡ وَمَا تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَأَدۡعُواْ رَبِّي عَسَىٰٓ أَلَّآ أَكُونَ بِدُعَآءِ رَبِّي شَقِيّٗا
Nami ninajitenga mbali nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na ninamwomba Mola wangu Mlezi; asaa nisiwe mwenye kukosa bahati kwa kumwomba Mola wangu Mlezi.
阿拉伯语经注:
فَلَمَّا ٱعۡتَزَلَهُمۡ وَمَا يَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَهَبۡنَا لَهُۥٓ إِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَۖ وَكُلّٗا جَعَلۡنَا نَبِيّٗا
Basi alipojitenga mbali nao na yale waliyokuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, tukamtunuku Is-haq na Yaaqub, na kila mmoja wao tukamfanya Nabii.
阿拉伯语经注:
وَوَهَبۡنَا لَهُم مِّن رَّحۡمَتِنَا وَجَعَلۡنَا لَهُمۡ لِسَانَ صِدۡقٍ عَلِيّٗا
Na tukawatunuku katika rehema zetu na tukawafanya kupewa sifa za kweli tukufu.
阿拉伯语经注:
وَٱذۡكُرۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ مُوسَىٰٓۚ إِنَّهُۥ كَانَ مُخۡلَصٗا وَكَانَ رَسُولٗا نَّبِيّٗا
Na mtaje Musa katika Kitabu. Hakika yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa, na alikuwa Mtume, Nabii.
阿拉伯语经注:
وَنَٰدَيۡنَٰهُ مِن جَانِبِ ٱلطُّورِ ٱلۡأَيۡمَنِ وَقَرَّبۡنَٰهُ نَجِيّٗا
Na tulimwitia upande wa kulia wa mlima na tukamsogeza kunong'ona naye.
阿拉伯语经注:
وَوَهَبۡنَا لَهُۥ مِن رَّحۡمَتِنَآ أَخَاهُ هَٰرُونَ نَبِيّٗا
Nasi kwa rehema zetu tukamtunuku kakaye, Harun, awe Nabii.
阿拉伯语经注:
وَٱذۡكُرۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ إِسۡمَٰعِيلَۚ إِنَّهُۥ كَانَ صَادِقَ ٱلۡوَعۡدِ وَكَانَ رَسُولٗا نَّبِيّٗا
Na mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii.
阿拉伯语经注:
وَكَانَ يَأۡمُرُ أَهۡلَهُۥ بِٱلصَّلَوٰةِ وَٱلزَّكَوٰةِ وَكَانَ عِندَ رَبِّهِۦ مَرۡضِيّٗا
Na alikuwa akiwaamrisha ahali zake Swala na Zaka, na alikuwa mbele ya Mola wake Mlezi mwenye kuridhiwa.
阿拉伯语经注:
وَٱذۡكُرۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ إِدۡرِيسَۚ إِنَّهُۥ كَانَ صِدِّيقٗا نَّبِيّٗا
Na mtaje katika Kitabu Idris. Hakika yeye alikuwa ni mkweli mno, Nabii.
阿拉伯语经注:
وَرَفَعۡنَٰهُ مَكَانًا عَلِيًّا
Na tulimuinua mahali pa juu.
阿拉伯语经注:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ مِن ذُرِّيَّةِ ءَادَمَ وَمِمَّنۡ حَمَلۡنَا مَعَ نُوحٖ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡرَٰٓءِيلَ وَمِمَّنۡ هَدَيۡنَا وَٱجۡتَبَيۡنَآۚ إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُ ٱلرَّحۡمَٰنِ خَرُّواْۤ سُجَّدٗاۤ وَبُكِيّٗا۩
Hao ndio aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii katika uzao wa Adam, na katika uzao wa wale tuliowabeba pamoja na Nuhu, na katika uzao wa Ibrahim na Israili, na katika wale tuliowaongoa na tukawateua. Wanaposomewa Aya za Mwingi wa rehema, huanguka kusujudu na kulia.
阿拉伯语经注:
۞ فَخَلَفَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ خَلۡفٌ أَضَاعُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَٱتَّبَعُواْ ٱلشَّهَوَٰتِۖ فَسَوۡفَ يَلۡقَوۡنَ غَيًّا
Lakini wakaja baada yao wafuatizi walioipoteza Swala, na wakafuata matamanio. Basi watakujakuta malipo ya ubaya.
阿拉伯语经注:
إِلَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَأُوْلَٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ وَلَا يُظۡلَمُونَ شَيۡـٔٗا
Isipokuwa mwenye kutubu, akaamini, na akatenda mema. Hao basi, wataingia Bustanini wala hawatadhulumiwa chochote.
阿拉伯语经注:
جَنَّٰتِ عَدۡنٍ ٱلَّتِي وَعَدَ ٱلرَّحۡمَٰنُ عِبَادَهُۥ بِٱلۡغَيۡبِۚ إِنَّهُۥ كَانَ وَعۡدُهُۥ مَأۡتِيّٗا
Bustani za milele ambazo aliwaahidi Rahmani (Mwingi wa rehema) waja wake katika ghaibu. Hakika Yeye ahadi yake hakuna shaka itafika.
阿拉伯语经注:
لَّا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوًا إِلَّا سَلَٰمٗاۖ وَلَهُمۡ رِزۡقُهُمۡ فِيهَا بُكۡرَةٗ وَعَشِيّٗا
Humo hawatasikia upuuzi wowote, isipokuwa Salama tu. Na watapata humo riziki zao asubuhi na jioni.
阿拉伯语经注:
تِلۡكَ ٱلۡجَنَّةُ ٱلَّتِي نُورِثُ مِنۡ عِبَادِنَا مَن كَانَ تَقِيّٗا
Hiyo ndiyo Bustani tutakayowarithisha katika waja wetu wale waliokuwa wacha Mungu.
阿拉伯语经注:
وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمۡرِ رَبِّكَۖ لَهُۥ مَا بَيۡنَ أَيۡدِينَا وَمَا خَلۡفَنَا وَمَا بَيۡنَ ذَٰلِكَۚ وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيّٗا
Wala hatuteremki isipokuwa kwa amri ya Mola wako Mlezi. Ni yake Yeye yaliyoko mbele yetu na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyomo katikati ya hayo. Na Mola wako Mlezi si mwenye kusahau.
阿拉伯语经注:
رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا فَٱعۡبُدۡهُ وَٱصۡطَبِرۡ لِعِبَٰدَتِهِۦۚ هَلۡ تَعۡلَمُ لَهُۥ سَمِيّٗا
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi muabudu Yeye tu, na usubiri katika kumuabudu. Je, unajua chochote kilicho sawa naye?
阿拉伯语经注:
وَيَقُولُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَءِذَا مَا مِتُّ لَسَوۡفَ أُخۡرَجُ حَيًّا
Na mwanadamu husema: Hivyo, nitakapokufa, ni kweli nitafufuliwa niwe hai tena?
阿拉伯语经注:
أَوَلَا يَذۡكُرُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَنَّا خَلَقۡنَٰهُ مِن قَبۡلُ وَلَمۡ يَكُ شَيۡـٔٗا
Je, hakumbuki mwanadamu ya kwamba hakika tulimuumba kabla, na wala hakuwa chochote?
阿拉伯语经注:
فَوَرَبِّكَ لَنَحۡشُرَنَّهُمۡ وَٱلشَّيَٰطِينَ ثُمَّ لَنُحۡضِرَنَّهُمۡ حَوۡلَ جَهَنَّمَ جِثِيّٗا
Basi ninaapa kwa Mola wako Mlezi! Kwa yakini tutawakusanya wao pamoja na mashetani. Kisha tutawahudhurisha kuizunguka Jahannamu huku wamepiga magoti!
阿拉伯语经注:
ثُمَّ لَنَنزِعَنَّ مِن كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمۡ أَشَدُّ عَلَى ٱلرَّحۡمَٰنِ عِتِيّٗا
Kisha kwa yakini tutaondoa katika kila kundi wale miongoni mwao waliozidi kumuasi Arrahmani (Mwingi wa rehema).
阿拉伯语经注:
ثُمَّ لَنَحۡنُ أَعۡلَمُ بِٱلَّذِينَ هُمۡ أَوۡلَىٰ بِهَا صِلِيّٗا
Tena hakika Sisi tunawajua vyema zaidi wanaostahiki kuunguzwa humo.
阿拉伯语经注:
وَإِن مِّنكُمۡ إِلَّا وَارِدُهَاۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتۡمٗا مَّقۡضِيّٗا
Wala hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa ataifikia. Hiyo ni hukumu ya Mola wako Mlezi ambayo lazima itimizwe.
阿拉伯语经注:
ثُمَّ نُنَجِّي ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْ وَّنَذَرُ ٱلظَّٰلِمِينَ فِيهَا جِثِيّٗا
Kisha tutawaokoa sawasawa wale waliomcha Mungu; na tutawaacha madhalimu humo huku wamepiga magoti.
阿拉伯语经注:
وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُنَا بَيِّنَٰتٖ قَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَيُّ ٱلۡفَرِيقَيۡنِ خَيۡرٞ مَّقَامٗا وَأَحۡسَنُ نَدِيّٗا
Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale waliokufuru huwaambia wale walioamini: Ni lipi katika makundi mawili haya lenye cheo kizuri na lililo zuri zaidi barazani?
阿拉伯语经注:
وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّن قَرۡنٍ هُمۡ أَحۡسَنُ أَثَٰثٗا وَرِءۡيٗا
Na kaumu ngapi tuliziangamiza zilizokuwa na mapambo mazuri zaidi na wazuri zaidi katika muonekano!
阿拉伯语经注:
قُلۡ مَن كَانَ فِي ٱلضَّلَٰلَةِ فَلۡيَمۡدُدۡ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ مَدًّاۚ حَتَّىٰٓ إِذَا رَأَوۡاْ مَا يُوعَدُونَ إِمَّا ٱلۡعَذَابَ وَإِمَّا ٱلسَّاعَةَ فَسَيَعۡلَمُونَ مَنۡ هُوَ شَرّٞ مَّكَانٗا وَأَضۡعَفُ جُندٗا
Sema: Yule aliye katika upotofu, basi Arrahmani (Mwingi wa rehema) na amuongezee (muda, mali na mengineyo) mpaka atakapoona yale waliyoahidiwa - ima ni adhabu au ni Saa, hapo ndipo watakapojua ni nani mwenye makao maovu zaidi na mwenye jeshi dhaifu zaidi.
阿拉伯语经注:
وَيَزِيدُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ٱهۡتَدَوۡاْ هُدٗىۗ وَٱلۡبَٰقِيَٰتُ ٱلصَّٰلِحَٰتُ خَيۡرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابٗا وَخَيۡرٞ مَّرَدًّا
Na Mwenyezi Mungu huwazidishia wale walioongoka uongofu. Na mema yenye kubakia ni bora katika malipo mbele ya Mola wako Mlezi na yana marejeo mema.
阿拉伯语经注:
أَفَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي كَفَرَ بِـَٔايَٰتِنَا وَقَالَ لَأُوتَيَنَّ مَالٗا وَوَلَدًا
Je, umemwona aliyezikufuru Ishara zetu na akasema: Kwa hakika mimi nitapewa mali na wana!
阿拉伯语经注:
أَطَّلَعَ ٱلۡغَيۡبَ أَمِ ٱتَّخَذَ عِندَ ٱلرَّحۡمَٰنِ عَهۡدٗا
Kwani yeye amepata habari za ghaibu, au amechukua agano kwa Arrahmani (Mwingi wa rehema)?
阿拉伯语经注:
كَلَّاۚ سَنَكۡتُبُ مَا يَقُولُ وَنَمُدُّ لَهُۥ مِنَ ٱلۡعَذَابِ مَدّٗا
Hasha! Tutaandika anayoyasema, na tutamuongezea sawasawa katika adhabu.
阿拉伯语经注:
وَنَرِثُهُۥ مَا يَقُولُ وَيَأۡتِينَا فَرۡدٗا
Na tutamrithi hayo anayoyasema, na atatujia mtupu peke yake!
阿拉伯语经注:
وَٱتَّخَذُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ ءَالِهَةٗ لِّيَكُونُواْ لَهُمۡ عِزّٗا
Na walichukua miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati iwape nguvu.
阿拉伯语经注:
كَلَّاۚ سَيَكۡفُرُونَ بِعِبَادَتِهِمۡ وَيَكُونُونَ عَلَيۡهِمۡ ضِدًّا
Sivyo hivyo! Wataikataa hiyo ibada yao, na watakuwa ndio dhidi yao.
阿拉伯语经注:
أَلَمۡ تَرَ أَنَّآ أَرۡسَلۡنَا ٱلشَّيَٰطِينَ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ تَؤُزُّهُمۡ أَزّٗا
Kwani huoni ya kwamba tuliwatuma mashetani kwa makafiri wawachochee sawasawa?
阿拉伯语经注:
فَلَا تَعۡجَلۡ عَلَيۡهِمۡۖ إِنَّمَا نَعُدُّ لَهُمۡ عَدّٗا
Basi usiwafanyie haraka. Sisi tunawahesabia idadi ya siku zao.
阿拉伯语经注:
يَوۡمَ نَحۡشُرُ ٱلۡمُتَّقِينَ إِلَى ٱلرَّحۡمَٰنِ وَفۡدٗا
Siku tutakayowakusanya wacha Mungu kuwapeleka kwa Arrahmani (Mwingi wa rehema) kuwa ni wageni wake.
阿拉伯语经注:
وَنَسُوقُ ٱلۡمُجۡرِمِينَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وِرۡدٗا
Na tukawaswaga wahalifu kwenda katika Jahannamu hali ya kuwa wana kiu.
阿拉伯语经注:
لَّا يَمۡلِكُونَ ٱلشَّفَٰعَةَ إِلَّا مَنِ ٱتَّخَذَ عِندَ ٱلرَّحۡمَٰنِ عَهۡدٗا
Hawatakuwa na mamlaka ya uombezi isipokuwa yule aliyechukua ahadi kwa Arrahmani (Mwingi wa rehema).
阿拉伯语经注:
وَقَالُواْ ٱتَّخَذَ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَلَدٗا
Na wao ati walisema kuwa Arrahmani (Mwingi wa rehema) alijifanyia mwana!
阿拉伯语经注:
لَّقَدۡ جِئۡتُمۡ شَيۡـًٔا إِدّٗا
Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno!
阿拉伯语经注:
تَكَادُ ٱلسَّمَٰوَٰتُ يَتَفَطَّرۡنَ مِنۡهُ وَتَنشَقُّ ٱلۡأَرۡضُ وَتَخِرُّ ٱلۡجِبَالُ هَدًّا
Zinakaribia mbingu kulipuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande.
阿拉伯语经注:
أَن دَعَوۡاْ لِلرَّحۡمَٰنِ وَلَدٗا
Kwa kudai kwao kuwa Arrahmani (Mwingi wa rehema) ana mwana.
阿拉伯语经注:
وَمَا يَنۢبَغِي لِلرَّحۡمَٰنِ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا
Wala Arrahmani (Mwingi wa rehema) hafailii kujichukulia mwana.
阿拉伯语经注:
إِن كُلُّ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ إِلَّآ ءَاتِي ٱلرَّحۡمَٰنِ عَبۡدٗا
Hakuna yeyote aliyemo mbinguni na ardhini isipokuwa atamjia Arrahmani (Mwingi wa rehema) kuwa ni mja wake.
阿拉伯语经注:
لَّقَدۡ أَحۡصَىٰهُمۡ وَعَدَّهُمۡ عَدّٗا
Yeye hakika amewadhibiti na amewahesabu sawasawa.
阿拉伯语经注:
وَكُلُّهُمۡ ءَاتِيهِ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فَرۡدًا
Na kila mmoja wao atamjia Siku ya Kiyama peke yake.
阿拉伯语经注:
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ سَيَجۡعَلُ لَهُمُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وُدّٗا
Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Arrahmani (Mwingi wa rehema) atawafanyia mapenzi.
阿拉伯语经注:
فَإِنَّمَا يَسَّرۡنَٰهُ بِلِسَانِكَ لِتُبَشِّرَ بِهِ ٱلۡمُتَّقِينَ وَتُنذِرَ بِهِۦ قَوۡمٗا لُّدّٗا
Na hakika tumeifanya nyepesi (Qur'ani) kwa ulimi wako, ili uwabashirie kwayo wacha Mungu, na uwaonye kwayo kaumu wagumu mno.
阿拉伯语经注:
وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّن قَرۡنٍ هَلۡ تُحِسُّ مِنۡهُم مِّنۡ أَحَدٍ أَوۡ تَسۡمَعُ لَهُمۡ رِكۡزَۢا
Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao. Je, unamuona hata mmoja katika wao au unasikia hata mnong'ono wao?
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 麦尔彦
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 - 译解目录

由拉瓦德翻译中心团队与拉布瓦 الدعوة协会和伊斯兰内容服务协会合作翻译。

关闭