Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 * - 译解目录


含义的翻译 章: 盖萨斯   段:

Al-Qasas

طسٓمٓ
Twa Sin Mim.[1]
[1] Herufi hizi "Twa, Sin, Miim" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
阿拉伯语经注:
تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ
Hizi ni Aya za Kitabu kinachobainisha.
阿拉伯语经注:
نَتۡلُواْ عَلَيۡكَ مِن نَّبَإِ مُوسَىٰ وَفِرۡعَوۡنَ بِٱلۡحَقِّ لِقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Tunakusomea katika habari za Musa na Firauni kwa Haki kwa ajili ya watu wanaoamini.
阿拉伯语经注:
إِنَّ فِرۡعَوۡنَ عَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَجَعَلَ أَهۡلَهَا شِيَعٗا يَسۡتَضۡعِفُ طَآئِفَةٗ مِّنۡهُمۡ يُذَبِّحُ أَبۡنَآءَهُمۡ وَيَسۡتَحۡيِۦ نِسَآءَهُمۡۚ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Hakika Firauni alitakabari katika ardhi, na akawagawa wananchi makundi mbali mbali. Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume na akiwaacha hai watoto wao wanawake. Hakika yeye alikuwa katika waharibifu.
阿拉伯语经注:
وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى ٱلَّذِينَ ٱسۡتُضۡعِفُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَنَجۡعَلَهُمۡ أَئِمَّةٗ وَنَجۡعَلَهُمُ ٱلۡوَٰرِثِينَ
Na tukataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika ardhi na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi.
阿拉伯语经注:
وَنُمَكِّنَ لَهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَنُرِيَ فِرۡعَوۡنَ وَهَٰمَٰنَ وَجُنُودَهُمَا مِنۡهُم مَّا كَانُواْ يَحۡذَرُونَ
Na kuwaimarisha katika ardhi, na kutokana na wao kuwaonyesha kina Firauni na Hamana na majeshi yao mambo yale waliyokuwa wakiyaogopa.
阿拉伯语经注:
وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ أُمِّ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَرۡضِعِيهِۖ فَإِذَا خِفۡتِ عَلَيۡهِ فَأَلۡقِيهِ فِي ٱلۡيَمِّ وَلَا تَخَافِي وَلَا تَحۡزَنِيٓۖ إِنَّا رَآدُّوهُ إِلَيۡكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Tulimfunulia mama yake Musa kwa kumwambia: Mnyonyeshe. Na utakapomhofia, basi mtie mtoni, na usihofu wala usihuzunike. Hakika Sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa Mitume.
阿拉伯语经注:
فَٱلۡتَقَطَهُۥٓ ءَالُ فِرۡعَوۡنَ لِيَكُونَ لَهُمۡ عَدُوّٗا وَحَزَنًاۗ إِنَّ فِرۡعَوۡنَ وَهَٰمَٰنَ وَجُنُودَهُمَا كَانُواْ خَٰطِـِٔينَ
Basi wakamwokota watu wa Firauni, aje kuwa adui kwao na huzuni. Hakika Firauni na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa.
阿拉伯语经注:
وَقَالَتِ ٱمۡرَأَتُ فِرۡعَوۡنَ قُرَّتُ عَيۡنٖ لِّي وَلَكَۖ لَا تَقۡتُلُوهُ عَسَىٰٓ أَن يَنفَعَنَآ أَوۡ نَتَّخِذَهُۥ وَلَدٗا وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ
Na mkewe Firauni alisema, "Atakuwa kiburudisho cha macho yangu na yako. Msimuuwe! Huenda akatufaa, au tumpange kuwa mwenetu." Wala wao hawakutambua.
阿拉伯语经注:
وَأَصۡبَحَ فُؤَادُ أُمِّ مُوسَىٰ فَٰرِغًاۖ إِن كَادَتۡ لَتُبۡدِي بِهِۦ لَوۡلَآ أَن رَّبَطۡنَا عَلَىٰ قَلۡبِهَا لِتَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Na moyo wa mama yake Musa ukawa mtupu. Alikuwa karibu kumdhihirisha, ingelikuwa hatukumtia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini.
阿拉伯语经注:
وَقَالَتۡ لِأُخۡتِهِۦ قُصِّيهِۖ فَبَصُرَتۡ بِهِۦ عَن جُنُبٖ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ
Naye akamwambia dada yake Musa, "Mfuatie." Basi naye akawa anamuangalia kwa mbali bila ya wao kujua.
阿拉伯语经注:
۞ وَحَرَّمۡنَا عَلَيۡهِ ٱلۡمَرَاضِعَ مِن قَبۡلُ فَقَالَتۡ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰٓ أَهۡلِ بَيۡتٖ يَكۡفُلُونَهُۥ لَكُمۡ وَهُمۡ لَهُۥ نَٰصِحُونَ
Na tukamjaalia awakatae wanyonyeshaji wote tangu mwanzo. Kwa hivyo, dada yake akasema, "Je, niwaonyesheni watu wa nyumba watakaomlelea huyu, nao pia watakuwa wema kwake?"
阿拉伯语经注:
فَرَدَدۡنَٰهُ إِلَىٰٓ أُمِّهِۦ كَيۡ تَقَرَّ عَيۡنُهَا وَلَا تَحۡزَنَ وَلِتَعۡلَمَ أَنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Basi tukamrudisha kwa mama yake ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ajue ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, lakini wengi wao hawajui.
阿拉伯语经注:
وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُۥ وَٱسۡتَوَىٰٓ ءَاتَيۡنَٰهُ حُكۡمٗا وَعِلۡمٗاۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na Musa alipofika utu uzima barabara, tulimpa akili na elimu. Na hivi ndivyo tunavyowalipa wazuri.
阿拉伯语经注:
وَدَخَلَ ٱلۡمَدِينَةَ عَلَىٰ حِينِ غَفۡلَةٖ مِّنۡ أَهۡلِهَا فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيۡنِ يَقۡتَتِلَانِ هَٰذَا مِن شِيعَتِهِۦ وَهَٰذَا مِنۡ عَدُوِّهِۦۖ فَٱسۡتَغَٰثَهُ ٱلَّذِي مِن شِيعَتِهِۦ عَلَى ٱلَّذِي مِنۡ عَدُوِّهِۦ فَوَكَزَهُۥ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيۡهِۖ قَالَ هَٰذَا مِنۡ عَمَلِ ٱلشَّيۡطَٰنِۖ إِنَّهُۥ عَدُوّٞ مُّضِلّٞ مُّبِينٞ
Na akaingia mjini wakati wa kughafilika wenyeji wake, na akakuta humo wanaume wawili wanapigana - mmoja ni katika watu wake, na mwingine katika maadui zake. Kwa hivyo, yule wa kutoka kwa watu wake akamtaka msaada kumpiga adui yake. Kwa hivyo, Musa akampiga ngumi, na akamuua. Akasema, "Hiki ni katika kitendo cha Shetani. Hakika yeye ni adui, mpotezaji dhahiri."
阿拉伯语经注:
قَالَ رَبِّ إِنِّي ظَلَمۡتُ نَفۡسِي فَٱغۡفِرۡ لِي فَغَفَرَ لَهُۥٓۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
Akasema, "Mola wangu Mlezi, hakika mimi nimejidhulumu mwenyewe. Basi nisamehe." Kwa hivyo, akamsamehe; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.
阿拉伯语经注:
قَالَ رَبِّ بِمَآ أَنۡعَمۡتَ عَلَيَّ فَلَنۡ أَكُونَ ظَهِيرٗا لِّلۡمُجۡرِمِينَ
Akasema, "Mola wangu Mlezi, kwa yale uliyonineemesha, basi mimi sitakuwa kabisa msaidizi wa wahalifu."
阿拉伯语经注:
فَأَصۡبَحَ فِي ٱلۡمَدِينَةِ خَآئِفٗا يَتَرَقَّبُ فَإِذَا ٱلَّذِي ٱسۡتَنصَرَهُۥ بِٱلۡأَمۡسِ يَسۡتَصۡرِخُهُۥۚ قَالَ لَهُۥ مُوسَىٰٓ إِنَّكَ لَغَوِيّٞ مُّبِينٞ
Akapambazukiwa mjini asubuhi naye ana hofu, akiangalia huku na huku. Mara yule yule aliyemtaka msaada jana akawa anamuita kwa sauti kubwa amsaidie. Musa akamwambia, "Hakika wewe ni mgomvi kweli kweli."
阿拉伯语经注:
فَلَمَّآ أَنۡ أَرَادَ أَن يَبۡطِشَ بِٱلَّذِي هُوَ عَدُوّٞ لَّهُمَا قَالَ يَٰمُوسَىٰٓ أَتُرِيدُ أَن تَقۡتُلَنِي كَمَا قَتَلۡتَ نَفۡسَۢا بِٱلۡأَمۡسِۖ إِن تُرِيدُ إِلَّآ أَن تَكُونَ جَبَّارٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا تُرِيدُ أَن تَكُونَ مِنَ ٱلۡمُصۡلِحِينَ
Basi alipotaka kumshika kwa nguvu yule aliye adui wao wote wawili, akasema, "Ewe Musa, unataka kuniua kama ulivyomuuwa mwanamume jana? Wewe hutaki isipokuwa kuwa jabari katika ardhi, wala hutaki kuwa miongoni mwa wale watengenezao mambo."
阿拉伯语经注:
وَجَآءَ رَجُلٞ مِّنۡ أَقۡصَا ٱلۡمَدِينَةِ يَسۡعَىٰ قَالَ يَٰمُوسَىٰٓ إِنَّ ٱلۡمَلَأَ يَأۡتَمِرُونَ بِكَ لِيَقۡتُلُوكَ فَٱخۡرُجۡ إِنِّي لَكَ مِنَ ٱلنَّٰصِحِينَ
Na akaja mbio mwanamume mmoja kutoka sehemu ya mbali muno ya mji, akasema, "Ewe Musa! Hakika, wakubwa wanashauriana juu yako kukuua. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanaokupa nasaha."
阿拉伯语经注:
فَخَرَجَ مِنۡهَا خَآئِفٗا يَتَرَقَّبُۖ قَالَ رَبِّ نَجِّنِي مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ
Basi akatoka humo, naye ana hofu, akiangalia huku na huku. Akasema, "Mola wangu Mlezi, niokoe kutokana na watu madhalimu."
阿拉伯语经注:
وَلَمَّا تَوَجَّهَ تِلۡقَآءَ مَدۡيَنَ قَالَ عَسَىٰ رَبِّيٓ أَن يَهۡدِيَنِي سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ
Na alipoelekea upande wa Madyana, alisema, "Huenda Mola wangu Mlezi akaniongoa njia iliyo sawa."
阿拉伯语经注:
وَلَمَّا وَرَدَ مَآءَ مَدۡيَنَ وَجَدَ عَلَيۡهِ أُمَّةٗ مِّنَ ٱلنَّاسِ يَسۡقُونَ وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ ٱمۡرَأَتَيۡنِ تَذُودَانِۖ قَالَ مَا خَطۡبُكُمَاۖ قَالَتَا لَا نَسۡقِي حَتَّىٰ يُصۡدِرَ ٱلرِّعَآءُۖ وَأَبُونَا شَيۡخٞ كَبِيرٞ
Na alipoyafikia maji ya Madyana, akakuta umati wa watu wananywesha (wanyama wao), na akakuta karibu yao wanawake wawili wanawazuia wanyama wao. Akasema, "Mna nini?" Wakasema, "Hatunyweshi sisi mpaka wamalize hao wachungaji. Na baba yetu ni mzee sana."
阿拉伯语经注:
فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰٓ إِلَى ٱلظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَآ أَنزَلۡتَ إِلَيَّ مِنۡ خَيۡرٖ فَقِيرٞ
Basi Musa akawanyweshea; kisha akarudi kivulini, na akasema, "Mola wangu Mlezi, hakika mimi ni mhitaji wa heri utakayoniteremshia."
阿拉伯语经注:
فَجَآءَتۡهُ إِحۡدَىٰهُمَا تَمۡشِي عَلَى ٱسۡتِحۡيَآءٖ قَالَتۡ إِنَّ أَبِي يَدۡعُوكَ لِيَجۡزِيَكَ أَجۡرَ مَا سَقَيۡتَ لَنَاۚ فَلَمَّا جَآءَهُۥ وَقَصَّ عَلَيۡهِ ٱلۡقَصَصَ قَالَ لَا تَخَفۡۖ نَجَوۡتَ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ
Basi mmoja katika wale wanawake wawili akamjia, naye anaona haya. Akasema, "Hakika baba yangu anakuita akulipe ujira wa kutunyweshea." Basi alipomjia na akamsimulia visa vyake, alisema, "Usihofu; umekwisha okoka kutokana na watu hao madhalimu."
阿拉伯语经注:
قَالَتۡ إِحۡدَىٰهُمَا يَٰٓأَبَتِ ٱسۡتَـٔۡجِرۡهُۖ إِنَّ خَيۡرَ مَنِ ٱسۡتَـٔۡجَرۡتَ ٱلۡقَوِيُّ ٱلۡأَمِينُ
Akasema mmoja katika wale wanawake, "Ewe baba yetu, muajiri huyu. Hakika mbora zaidi unayeweza kuajiri ni mwenye nguvu na muaminifu."
阿拉伯语经注:
قَالَ إِنِّيٓ أُرِيدُ أَنۡ أُنكِحَكَ إِحۡدَى ٱبۡنَتَيَّ هَٰتَيۡنِ عَلَىٰٓ أَن تَأۡجُرَنِي ثَمَٰنِيَ حِجَجٖۖ فَإِنۡ أَتۡمَمۡتَ عَشۡرٗا فَمِنۡ عِندِكَۖ وَمَآ أُرِيدُ أَنۡ أَشُقَّ عَلَيۡكَۚ سَتَجِدُنِيٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ
Akasema, "Hakika mimi ninataka kukuoza mmojawapo katika binti zangu hawa wawili kwa sharti kwamba unitumikie miaka minane. Lakini ukitimiza kumi, basi hiari ni yako. Nami sitaki kukutaabisha. Mwenyezi Mungu akipenda (Inshallah), utanikuta miongoni mwa watu wema."
阿拉伯语经注:
قَالَ ذَٰلِكَ بَيۡنِي وَبَيۡنَكَۖ أَيَّمَا ٱلۡأَجَلَيۡنِ قَضَيۡتُ فَلَا عُدۡوَٰنَ عَلَيَّۖ وَٱللَّهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٞ
Musa akasema, "Hayo yamekwisha kuwa baina yangu na wewe. Muda mmojapo nikiumaliza, sitiwi ubayani. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa juu ya haya tunayoyasema."
阿拉伯语经注:
۞ فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى ٱلۡأَجَلَ وَسَارَ بِأَهۡلِهِۦٓ ءَانَسَ مِن جَانِبِ ٱلطُّورِ نَارٗاۖ قَالَ لِأَهۡلِهِ ٱمۡكُثُوٓاْ إِنِّيٓ ءَانَسۡتُ نَارٗا لَّعَلِّيٓ ءَاتِيكُم مِّنۡهَا بِخَبَرٍ أَوۡ جَذۡوَةٖ مِّنَ ٱلنَّارِ لَعَلَّكُمۡ تَصۡطَلُونَ
Basi Musa alipotimiza muda wake na akasafiri na ahali zake, aliona moto upande wa Mlima 'Turi. Akawaambia ahali zake, "Ngojeni! Hakika mimi nimeona moto. Labda nitawaletea kutoka huko habari au kijinga cha moto ili mpate kuota moto."
阿拉伯语经注:
فَلَمَّآ أَتَىٰهَا نُودِيَ مِن شَٰطِيِٕ ٱلۡوَادِ ٱلۡأَيۡمَنِ فِي ٱلۡبُقۡعَةِ ٱلۡمُبَٰرَكَةِ مِنَ ٱلشَّجَرَةِ أَن يَٰمُوسَىٰٓ إِنِّيٓ أَنَا ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Basi alipoufikia, aliitwa kutokea ng'ambo ya bonde la kuliani katika eneo lililobarikiwa kutoka kwenye mti, "Ewe Musa! Hakika Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote."
阿拉伯语经注:
وَأَنۡ أَلۡقِ عَصَاكَۚ فَلَمَّا رَءَاهَا تَهۡتَزُّ كَأَنَّهَا جَآنّٞ وَلَّىٰ مُدۡبِرٗا وَلَمۡ يُعَقِّبۡۚ يَٰمُوسَىٰٓ أَقۡبِلۡ وَلَا تَخَفۡۖ إِنَّكَ مِنَ ٱلۡأٓمِنِينَ
Na tupa chini fimbo yako. Basi alipoiona ikitikisika kama nyoka, akarudi nyuma wala hakutazama. (Akaambiwa), "Ewe Musa, njoo mbele wala usihofu. Hakika wewe ni miongoni mwa walio katika amani."
阿拉伯语经注:
ٱسۡلُكۡ يَدَكَ فِي جَيۡبِكَ تَخۡرُجۡ بَيۡضَآءَ مِنۡ غَيۡرِ سُوٓءٖ وَٱضۡمُمۡ إِلَيۡكَ جَنَاحَكَ مِنَ ٱلرَّهۡبِۖ فَذَٰنِكَ بُرۡهَٰنَانِ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦٓۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ
Ingiza mkono wako kwenye mfuko wako, utatoka mweupe pasipo na ubaya wowote. Na jiambatishe mkono wako ukihisi hofu. Basi hizi ni hoja mbili zitokazo kwa Mola wako Mlezi umpelekee Firauni na wakuu wa umma wake. Hakika hao walikuwa watu wavukao mipaka.
阿拉伯语经注:
قَالَ رَبِّ إِنِّي قَتَلۡتُ مِنۡهُمۡ نَفۡسٗا فَأَخَافُ أَن يَقۡتُلُونِ
Akasema, "Mola wangu Mlezi, hakika mimi nilimuua mtu katika wao, kwa hivyo ninahofu wataniua.
阿拉伯语经注:
وَأَخِي هَٰرُونُ هُوَ أَفۡصَحُ مِنِّي لِسَانٗا فَأَرۡسِلۡهُ مَعِيَ رِدۡءٗا يُصَدِّقُنِيٓۖ إِنِّيٓ أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ
Na kaka yangu Harun ni fasaha zaidi ulimi wake kuliko mimi. Basi mtume pamoja nami kunisaidia, ili anisadikishe. Hakika mimi ninahofu watanikadhibisha."
阿拉伯语经注:
قَالَ سَنَشُدُّ عَضُدَكَ بِأَخِيكَ وَنَجۡعَلُ لَكُمَا سُلۡطَٰنٗا فَلَا يَصِلُونَ إِلَيۡكُمَا بِـَٔايَٰتِنَآۚ أَنتُمَا وَمَنِ ٱتَّبَعَكُمَا ٱلۡغَٰلِبُونَ
(Mwenyezi Mungu) akasema, "Tutautia nguvu mkono wako kwa kaka yako, na tutawapa mamlaka, kwa hivyo hawatawafikilia. Kwa sababu ya Ishara zetu, nyinyi na watakaowafuata ndio mtashinda."
阿拉伯语经注:
فَلَمَّا جَآءَهُم مُّوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَا بَيِّنَٰتٖ قَالُواْ مَا هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّفۡتَرٗى وَمَا سَمِعۡنَا بِهَٰذَا فِيٓ ءَابَآئِنَا ٱلۡأَوَّلِينَ
Basi Musa alipowafikia na Ishara zetu, walisema, "Haya si chochote isipokuwa ni uchawi uliozuliwa. Na hatukuyasikia haya kwa baba zetu wa zamani."
阿拉伯语经注:
وَقَالَ مُوسَىٰ رَبِّيٓ أَعۡلَمُ بِمَن جَآءَ بِٱلۡهُدَىٰ مِنۡ عِندِهِۦ وَمَن تَكُونُ لَهُۥ عَٰقِبَةُ ٱلدَّارِۚ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلظَّٰلِمُونَ
Na Musa akasema, "Mola wangu Mlezi ni Mwenye kujua kabisa ni nani anayekuja na uwongofu unaotoka kwake, na ni nani atakayekuwa na mwisho mwema wa makazi. Hakika wenye kudhulumu hawatafanikiwa."
阿拉伯语经注:
وَقَالَ فِرۡعَوۡنُ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمَلَأُ مَا عَلِمۡتُ لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرِي فَأَوۡقِدۡ لِي يَٰهَٰمَٰنُ عَلَى ٱلطِّينِ فَٱجۡعَل لِّي صَرۡحٗا لَّعَلِّيٓ أَطَّلِعُ إِلَىٰٓ إِلَٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُۥ مِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ
Na Firauni akasema, "Enyi waheshimiwa, sijawahi kujua kama mnaye mungu asiyekuwa mimi. Ewe Haman, niwashie moto unichomee udongo, unijengee mnara nipate kumchungulia mungu wa Musa. Na hakika mimi ninamwona yeye ni katika waongo."
阿拉伯语经注:
وَٱسۡتَكۡبَرَ هُوَ وَجُنُودُهُۥ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُمۡ إِلَيۡنَا لَا يُرۡجَعُونَ
Na alipanda kiburi yeye na majeshi yake katika ardhi bila ya haki, na wakadhania kuwa hawatarudishwa kwetu.
阿拉伯语经注:
فَأَخَذۡنَٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡيَمِّۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلظَّٰلِمِينَ
Basi tukamshika yeye na majeshi yake, na tukawatupa baharini. Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa wenye kudhulumu?
阿拉伯语经注:
وَجَعَلۡنَٰهُمۡ أَئِمَّةٗ يَدۡعُونَ إِلَى ٱلنَّارِۖ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ لَا يُنصَرُونَ
Na tuliwafanya ni waongozi waitao kwenye Moto. Na Siku ya Qiyama hawatanusuriwa.
阿拉伯语经注:
وَأَتۡبَعۡنَٰهُمۡ فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا لَعۡنَةٗۖ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ هُم مِّنَ ٱلۡمَقۡبُوحِينَ
Na tukawafuatishia laana katika dunia hii, na Siku ya Qiyama watakuwa miongoni mwa wanaochusha.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ مِنۢ بَعۡدِ مَآ أَهۡلَكۡنَا ٱلۡقُرُونَ ٱلۡأُولَىٰ بَصَآئِرَ لِلنَّاسِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لَّعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ
Na hakika bila ya shaka tulimpa Musa Kitabu baada ya kwisha kuziangamiza kaumu za mwanzo, ili kiwafumbue macho watu, na kiwe uongofu, na rehema, ili wapate kukumbuka.
阿拉伯语经注:
وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ ٱلۡغَرۡبِيِّ إِذۡ قَضَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَى ٱلۡأَمۡرَ وَمَا كُنتَ مِنَ ٱلشَّٰهِدِينَ
Wala wewe hukuwa upande wa magharibi tulipompa Musa amri, wala hukuwa katika waliohudhuria.
阿拉伯语经注:
وَلَٰكِنَّآ أَنشَأۡنَا قُرُونٗا فَتَطَاوَلَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡعُمُرُۚ وَمَا كُنتَ ثَاوِيٗا فِيٓ أَهۡلِ مَدۡيَنَ تَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِنَا وَلَٰكِنَّا كُنَّا مُرۡسِلِينَ
Lakini Sisi tuliziumba kaumu, na ukawa mrefu umri juu yao. Wala hukuwa mkazi na watu wa Madyana ukiwasomea Aya zetu. Lakini ni Sisi tuliokuwa tukiwatuma Mitume.
阿拉伯语经注:
وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ ٱلطُّورِ إِذۡ نَادَيۡنَا وَلَٰكِن رَّحۡمَةٗ مِّن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوۡمٗا مَّآ أَتَىٰهُم مِّن نَّذِيرٖ مِّن قَبۡلِكَ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ
Wala hukuwa kando ya mlima tuliponadi. Lakini ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi ili uwaonye watu wasiopata kufikiwa na mwonyaji kabla yako, huenda wakakumbuka.
阿拉伯语经注:
وَلَوۡلَآ أَن تُصِيبَهُم مُّصِيبَةُۢ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡ فَيَقُولُواْ رَبَّنَا لَوۡلَآ أَرۡسَلۡتَ إِلَيۡنَا رَسُولٗا فَنَتَّبِعَ ءَايَٰتِكَ وَنَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Na usije kuwasibu msiba kwa iliyoyatanguliza mikono yao, wakasema, "Ewe Mola wetu Mlezi, mbona hukututumia Mtume nasi, tukafuata Ishara zako, na tukawa miongoni mwa Waumini?"
阿拉伯语经注:
فَلَمَّا جَآءَهُمُ ٱلۡحَقُّ مِنۡ عِندِنَا قَالُواْ لَوۡلَآ أُوتِيَ مِثۡلَ مَآ أُوتِيَ مُوسَىٰٓۚ أَوَلَمۡ يَكۡفُرُواْ بِمَآ أُوتِيَ مُوسَىٰ مِن قَبۡلُۖ قَالُواْ سِحۡرَانِ تَظَٰهَرَا وَقَالُوٓاْ إِنَّا بِكُلّٖ كَٰفِرُونَ
Ilipowajia Haki kutoka kwetu, walisema, "Mbona hakupewa kama aliyopewa Musa?" Je, kwani wao hawakuyakataa aliyopewa Musa zamani? Walisema, "Ni wachawi wawili wanasaidiana." Na wakasema, "Hakika sisi tunawakataa wote."
阿拉伯语经注:
قُلۡ فَأۡتُواْ بِكِتَٰبٖ مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِ هُوَ أَهۡدَىٰ مِنۡهُمَآ أَتَّبِعۡهُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Sema, "Basi leteni Kitabu kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu kilicho kiongofu zaidi kuliko hivi viwili nikifuate, kama nyinyi ni wakweli."
阿拉伯语经注:
فَإِن لَّمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَكَ فَٱعۡلَمۡ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهۡوَآءَهُمۡۚ وَمَنۡ أَضَلُّ مِمَّنِ ٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ بِغَيۡرِ هُدٗى مِّنَ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ
Na ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata matamanio yao tu. Na ni nani aliyepotea zaidi kumshinda anayefuata matamanio yake bila ya uongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.
阿拉伯语经注:
۞ وَلَقَدۡ وَصَّلۡنَا لَهُمُ ٱلۡقَوۡلَ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ
Na sasa kwa yakini tumewafikishia Neno ili wapate kukumbuka.
阿拉伯语经注:
ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِهِۦ هُم بِهِۦ يُؤۡمِنُونَ
Wale tuliowapa Kitabu kabla yake wanakiamini hiki.
阿拉伯语经注:
وَإِذَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِهِۦٓ إِنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّنَآ إِنَّا كُنَّا مِن قَبۡلِهِۦ مُسۡلِمِينَ
Na wanaposomewa, wanasema, "Tunaiamini. Hakika hii ndiyo Haki inayotoka kwa Mola wetu Mlezi. Hakika sisi kabla yake tulikuwa ni Waislamu, tulionyenyekea."
阿拉伯语经注:
أُوْلَٰٓئِكَ يُؤۡتَوۡنَ أَجۡرَهُم مَّرَّتَيۡنِ بِمَا صَبَرُواْ وَيَدۡرَءُونَ بِٱلۡحَسَنَةِ ٱلسَّيِّئَةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ
Hao watapewa ujira wao mara mbili kwa walivyovumilia, na wakaondoa ubaya kwa wema, na wakatoa katika tulivyowaruzuku.
阿拉伯语经注:
وَإِذَا سَمِعُواْ ٱللَّغۡوَ أَعۡرَضُواْ عَنۡهُ وَقَالُواْ لَنَآ أَعۡمَٰلُنَا وَلَكُمۡ أَعۡمَٰلُكُمۡ سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمۡ لَا نَبۡتَغِي ٱلۡجَٰهِلِينَ
Na wanaposikia upuuzi, hujitenga nao na husema, "Sisi tuna vitendo vyetu, na nyinyi mna vitendo vyenu. Salamun Alaikum (Amani juu yenu)! Sisi hatutaki kujibizana na wajinga."
阿拉伯语经注:
إِنَّكَ لَا تَهۡدِي مَنۡ أَحۡبَبۡتَ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ
Kwa hakika, wewe humwongoi umpendaye. Lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao.
阿拉伯语经注:
وَقَالُوٓاْ إِن نَّتَّبِعِ ٱلۡهُدَىٰ مَعَكَ نُتَخَطَّفۡ مِنۡ أَرۡضِنَآۚ أَوَلَمۡ نُمَكِّن لَّهُمۡ حَرَمًا ءَامِنٗا يُجۡبَىٰٓ إِلَيۡهِ ثَمَرَٰتُ كُلِّ شَيۡءٖ رِّزۡقٗا مِّن لَّدُنَّا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Na wakasema, "Tukiufuata uwongofu huu pamoja nawe, tutanyakuliwa kutoka nchi yetu." Je, kwani Sisi hatukuwaweka imara katika pahala patakatifu, penye amani, ambapo huletewa matunda ya kila aina kuwa ni riziki itokayo kwetu? Lakini wengi wao hawajui.
阿拉伯语经注:
وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا مِن قَرۡيَةِۭ بَطِرَتۡ مَعِيشَتَهَاۖ فَتِلۡكَ مَسَٰكِنُهُمۡ لَمۡ تُسۡكَن مِّنۢ بَعۡدِهِمۡ إِلَّا قَلِيلٗاۖ وَكُنَّا نَحۡنُ ٱلۡوَٰرِثِينَ
Na miji mingapi iliyojifahirisha katika maisha yao tumeiangamiza! Na hayo maskani yao hayakukaliwa tena baada yao, isipokuwa kwa uchache tu. Na Sisi ndio tumekuwa warithi wao.
阿拉伯语经注:
وَمَا كَانَ رَبُّكَ مُهۡلِكَ ٱلۡقُرَىٰ حَتَّىٰ يَبۡعَثَ فِيٓ أُمِّهَا رَسُولٗا يَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِنَاۚ وَمَا كُنَّا مُهۡلِكِي ٱلۡقُرَىٰٓ إِلَّا وَأَهۡلُهَا ظَٰلِمُونَ
Na Mola wako Mlezi haangamizi miji mpaka ampeleke Mtume katika miji yake mikuu awasomee Ishara zetu. Wala hatuiangamizi miji mpaka watu wake wawe madhalimu.
阿拉伯语经注:
وَمَآ أُوتِيتُم مِّن شَيۡءٖ فَمَتَٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَزِينَتُهَاۚ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ
Na chochote mlichopewa, ni matumizi ya maisha ya dunia na pambo lake. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ndiyo bora na yatakayobaki zaidi. Basi je, hamfahamu?
阿拉伯语经注:
أَفَمَن وَعَدۡنَٰهُ وَعۡدًا حَسَنٗا فَهُوَ لَٰقِيهِ كَمَن مَّتَّعۡنَٰهُ مَتَٰعَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا ثُمَّ هُوَ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ مِنَ ٱلۡمُحۡضَرِينَ
Je, yule tuliyemuahidi ahadi nzuri, tena naye akayapata, ni kama tuliyemstarehesha kwa starehe za maisha ya duniani, na kisha Siku ya Qiyama akawa miongoni mwa wanaohudhurishwa?
阿拉伯语经注:
وَيَوۡمَ يُنَادِيهِمۡ فَيَقُولُ أَيۡنَ شُرَكَآءِيَ ٱلَّذِينَ كُنتُمۡ تَزۡعُمُونَ
Na siku atakapowaita na akasema, "Wako wapi mliokuwa mkidai kuwa ni washirika wangu?"
阿拉伯语经注:
قَالَ ٱلَّذِينَ حَقَّ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقَوۡلُ رَبَّنَا هَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَغۡوَيۡنَآ أَغۡوَيۡنَٰهُمۡ كَمَا غَوَيۡنَاۖ تَبَرَّأۡنَآ إِلَيۡكَۖ مَا كَانُوٓاْ إِيَّانَا يَعۡبُدُونَ
Watasema wale iliyothibiti juu yao kauli, "Mola wetu Mlezi! Hawa ndio tuliowapoteza. Tuliwapoteza kama tulivyopotea sisi. Tunajitenga nao mbele yako. Hawakuwa wakituabudu sisi."
阿拉伯语经注:
وَقِيلَ ٱدۡعُواْ شُرَكَآءَكُمۡ فَدَعَوۡهُمۡ فَلَمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَهُمۡ وَرَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَۚ لَوۡ أَنَّهُمۡ كَانُواْ يَهۡتَدُونَ
Na itasemwa, "Waiteni hao miungu wa kishirikina wenu!" Basi watawaita, lakini hawatawaitikia, na wataiona adhabu; laiti wangelikuwa wameongoka!
阿拉伯语经注:
وَيَوۡمَ يُنَادِيهِمۡ فَيَقُولُ مَاذَآ أَجَبۡتُمُ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na siku atakapowaita na akasema, "Mliwajibu nini Mitume?"
阿拉伯语经注:
فَعَمِيَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَنۢبَآءُ يَوۡمَئِذٖ فَهُمۡ لَا يَتَسَآءَلُونَ
Basi zitawapotea habari siku hiyo, nao hawataulizana.
阿拉伯语经注:
فَأَمَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَعَسَىٰٓ أَن يَكُونَ مِنَ ٱلۡمُفۡلِحِينَ
Ama mwenye kutubu na akaamini na akatenda mema, huyo atakuwa miongoni mwa wenye kufaulu.
阿拉伯语经注:
وَرَبُّكَ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُ وَيَخۡتَارُۗ مَا كَانَ لَهُمُ ٱلۡخِيَرَةُۚ سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ
Na Mola wako Mlezi huumba na huteua atakavyo. Viumbe hawana hiari. Mwenyezi Mungu ametukuka na ametakasika na hao wanaowashirikisha naye.
阿拉伯语经注:
وَرَبُّكَ يَعۡلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمۡ وَمَا يُعۡلِنُونَ
Na Mola wako Mlezi anayajua viliyoyaficha vifua vyao, na wanayoyaweka hadharani.
阿拉伯语经注:
وَهُوَ ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ لَهُ ٱلۡحَمۡدُ فِي ٱلۡأُولَىٰ وَٱلۡأٓخِرَةِۖ وَلَهُ ٱلۡحُكۡمُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho. Na hukumu ni yake Yeye. Na kwake Yeye mtarejeshwa.
阿拉伯语经注:
قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِن جَعَلَ ٱللَّهُ عَلَيۡكُمُ ٱلَّيۡلَ سَرۡمَدًا إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَنۡ إِلَٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِ يَأۡتِيكُم بِضِيَآءٍۚ أَفَلَا تَسۡمَعُونَ
Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeliufanya usiku umekukalieni moja kwa moja mpaka Siku ya Qiyama, mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayewaletea mwangaza? Basi je, hamsikii?
阿拉伯语经注:
قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِن جَعَلَ ٱللَّهُ عَلَيۡكُمُ ٱلنَّهَارَ سَرۡمَدًا إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَنۡ إِلَٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِ يَأۡتِيكُم بِلَيۡلٖ تَسۡكُنُونَ فِيهِۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ
Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeliufanya mchana umewakalia moja kwa moja mpaka Siku ya Qiyama, mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atayewaletea usiku mkapumzika humo? Basi je, hamwoni?
阿拉伯语经注:
وَمِن رَّحۡمَتِهِۦ جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ لِتَسۡكُنُواْ فِيهِ وَلِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ
Na ni katika rehema zake amewafanyia usiku na mchana ili mpate kupumzika humo na mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru.
阿拉伯语经注:
وَيَوۡمَ يُنَادِيهِمۡ فَيَقُولُ أَيۡنَ شُرَكَآءِيَ ٱلَّذِينَ كُنتُمۡ تَزۡعُمُونَ
Na siku atakapowaita na akasema, "Wako wapi hao mliokuwa mkidai kuwa ni washirika wangu?"
阿拉伯语经注:
وَنَزَعۡنَا مِن كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدٗا فَقُلۡنَا هَاتُواْ بُرۡهَٰنَكُمۡ فَعَلِمُوٓاْ أَنَّ ٱلۡحَقَّ لِلَّهِ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ
Na tutatoa shahidi katika kila umma, na tutasema, "Leteni hoja zenu!" Hapo watajua kwamba hakika haki ni ya Mwenyezi Mungu, na yatawapotea yale waliyokuwa wakiyazua.
阿拉伯语经注:
۞ إِنَّ قَٰرُونَ كَانَ مِن قَوۡمِ مُوسَىٰ فَبَغَىٰ عَلَيۡهِمۡۖ وَءَاتَيۡنَٰهُ مِنَ ٱلۡكُنُوزِ مَآ إِنَّ مَفَاتِحَهُۥ لَتَنُوٓأُ بِٱلۡعُصۡبَةِ أُوْلِي ٱلۡقُوَّةِ إِذۡ قَالَ لَهُۥ قَوۡمُهُۥ لَا تَفۡرَحۡۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡفَرِحِينَ
Hakika Qaruni alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia dhuluma. Na tulimpa hazina ambazo funguo zake zinawatopeza watu wenye nguvu kuzibeba. Watu wake walipomwambia, "Usijigambe! Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaojigamba."
阿拉伯语经注:
وَٱبۡتَغِ فِيمَآ ءَاتَىٰكَ ٱللَّهُ ٱلدَّارَ ٱلۡأٓخِرَةَۖ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ ٱلدُّنۡيَاۖ وَأَحۡسِن كَمَآ أَحۡسَنَ ٱللَّهُ إِلَيۡكَۖ وَلَا تَبۡغِ ٱلۡفَسَادَ فِي ٱلۡأَرۡضِۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Na utafute, kwa aliyokupa Mwenyezi Mungu, makazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la duniani. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyokufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya uharibifu ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wafanyao uharibifu.
阿拉伯语经注:
قَالَ إِنَّمَآ أُوتِيتُهُۥ عَلَىٰ عِلۡمٍ عِندِيٓۚ أَوَلَمۡ يَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ قَدۡ أَهۡلَكَ مِن قَبۡلِهِۦ مِنَ ٱلۡقُرُونِ مَنۡ هُوَ أَشَدُّ مِنۡهُ قُوَّةٗ وَأَكۡثَرُ جَمۡعٗاۚ وَلَا يُسۡـَٔلُ عَن ذُنُوبِهِمُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ
Akasema, "Kwa hakika nimepewa haya kwa sababu ya elimu niliyo nayo." Je, hakujua kwamba Mwenyezi Mungu alikwisha waangamiza, katika vizazi vya walio kabla yake, watu waliokuwa wenye nguvu zaidi kuliko yeye, na wenye makundi makubwa zaidi kuliko yake. Na wahalifu hawataulizwa habari ya dhambi zao."
阿拉伯语经注:
فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوۡمِهِۦ فِي زِينَتِهِۦۖ قَالَ ٱلَّذِينَ يُرِيدُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا يَٰلَيۡتَ لَنَا مِثۡلَ مَآ أُوتِيَ قَٰرُونُ إِنَّهُۥ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٖ
Basi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale waliokuwa wanataka maisha ya duniani, "Laiti tungelikuwa tunayo kama aliyopewa Qaruni! Hakika yeye ni mwenye bahati kubwa."
阿拉伯语经注:
وَقَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ وَيۡلَكُمۡ ثَوَابُ ٱللَّهِ خَيۡرٞ لِّمَنۡ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗاۚ وَلَا يُلَقَّىٰهَآ إِلَّا ٱلصَّٰبِرُونَ
Na wakasema wale waliopewa elimu, "Ole wenu! Malipo ya Mwenyezi Mungu ni bora kwa mwenye kuamini na akatenda mema. Wala hawatapewa hayo isipokuwa wenye subira."
阿拉伯语经注:
فَخَسَفۡنَا بِهِۦ وَبِدَارِهِ ٱلۡأَرۡضَ فَمَا كَانَ لَهُۥ مِن فِئَةٖ يَنصُرُونَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُنتَصِرِينَ
Basi tukamdidimiza yeye na nyumba yake katika ardhi; wala halikuwepo kundi lolote la kumnusuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa wanaojitetea.
阿拉伯语经注:
وَأَصۡبَحَ ٱلَّذِينَ تَمَنَّوۡاْ مَكَانَهُۥ بِٱلۡأَمۡسِ يَقُولُونَ وَيۡكَأَنَّ ٱللَّهَ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦ وَيَقۡدِرُۖ لَوۡلَآ أَن مَّنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡنَا لَخَسَفَ بِنَاۖ وَيۡكَأَنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلۡكَٰفِرُونَ
Na wale waliotamani kuwa pahala pake jana, wakawa wanasema, "Kumbe Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humkunjia amtakaye. Ingelikuwa Mwenyezi Mungu hakutufanyia hisani, angelitudidimiza. Kumbe makafiri hawafanikiwi!"
阿拉伯语经注:
تِلۡكَ ٱلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ نَجۡعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوّٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فَسَادٗاۚ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلۡمُتَّقِينَ
Hayo ndiyo makazi ya Akhera, tumewafanyia wale wasiotaka kujiinua juu katika dunia wala uharibifu. Na mwisho mwema ni wa wacha Mungu.
阿拉伯语经注:
مَن جَآءَ بِٱلۡحَسَنَةِ فَلَهُۥ خَيۡرٞ مِّنۡهَاۖ وَمَن جَآءَ بِٱلسَّيِّئَةِ فَلَا يُجۡزَى ٱلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسَّيِّـَٔاتِ إِلَّا مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Atakayetenda mazuri, atapata malipo bora kuliko hayo mazuri aliyoyatenda. Na atakayetenda mabaya, hawalipwi watendao mabaya isipokuwa yale waliyokuwa wakiyatenda.
阿拉伯语经注:
إِنَّ ٱلَّذِي فَرَضَ عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ لَرَآدُّكَ إِلَىٰ مَعَادٖۚ قُل رَّبِّيٓ أَعۡلَمُ مَن جَآءَ بِٱلۡهُدَىٰ وَمَنۡ هُوَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ
Hakika yule aliyekulazimisha kuifuata Qur-ani, hapana shaka atakurudisha pahala pa marejeo. Sema, "Mola wangu Mlezi ndiye anayemjua zaidi mwenye kuja na uwongofu, na ni nani aliyemo katika upotofu ulio dhahiri."
阿拉伯语经注:
وَمَا كُنتَ تَرۡجُوٓاْ أَن يُلۡقَىٰٓ إِلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبُ إِلَّا رَحۡمَةٗ مِّن رَّبِّكَۖ فَلَا تَكُونَنَّ ظَهِيرٗا لِّلۡكَٰفِرِينَ
Nawe hukuwa unataraji kuletewa Kitabu; lakini ni rehema tu ya Mola wako Mlezi. Basi usiwe msaidizi wa makafiri.
阿拉伯语经注:
وَلَا يَصُدُّنَّكَ عَنۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ بَعۡدَ إِذۡ أُنزِلَتۡ إِلَيۡكَۖ وَٱدۡعُ إِلَىٰ رَبِّكَۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Wala kamwe wasikuzuie kuzifuata Aya za Mwenyezi Mungu baada ya kuteremshiwa wewe. Na lingania kwa Mola wako Mlezi, wala kamwe usiwe miongoni mwa washirikina.
阿拉伯语经注:
وَلَا تَدۡعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۘ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ كُلُّ شَيۡءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجۡهَهُۥۚ لَهُ ٱلۡحُكۡمُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
Wala usimwombe pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwinginewe. Hapana mungu isipokuwa Yeye. Kila kitu kitaangamia isipokuwa uso wake. Hukumu iko kwake, na kwake mtarejeshwa.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 盖萨斯
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 - 译解目录

由拉瓦德翻译中心团队与拉布瓦 الدعوة协会和伊斯兰内容服务协会合作翻译。

关闭