Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 * - 译解目录


含义的翻译 章: 嘎夫   段:

Qaf

قٓۚ وَٱلۡقُرۡءَانِ ٱلۡمَجِيدِ
Qaaf.[1] Ninaapa kwa Qur-ani tukufu!
[1] Herufi hii "Qaaf" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
阿拉伯语经注:
بَلۡ عَجِبُوٓاْ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٞ مِّنۡهُمۡ فَقَالَ ٱلۡكَٰفِرُونَ هَٰذَا شَيۡءٌ عَجِيبٌ
Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao, na wakasema makafiri: 'Hili ni jambo la ajabu!
阿拉伯语经注:
أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗاۖ ذَٰلِكَ رَجۡعُۢ بَعِيدٞ
Ati tukifa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali!'
阿拉伯语经注:
قَدۡ عَلِمۡنَا مَا تَنقُصُ ٱلۡأَرۡضُ مِنۡهُمۡۖ وَعِندَنَا كِتَٰبٌ حَفِيظُۢ
Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinachopunguzwa na ardhi kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinachohifadhi vyema yote.
阿拉伯语经注:
بَلۡ كَذَّبُواْ بِٱلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمۡ فَهُمۡ فِيٓ أَمۡرٖ مَّرِيجٍ
Lakini waliikanusha Haki ilipowajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mchanganyiko.
阿拉伯语经注:
أَفَلَمۡ يَنظُرُوٓاْ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَوۡقَهُمۡ كَيۡفَ بَنَيۡنَٰهَا وَزَيَّنَّٰهَا وَمَا لَهَا مِن فُرُوجٖ
Je, hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyozijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa.
阿拉伯语经注:
وَٱلۡأَرۡضَ مَدَدۡنَٰهَا وَأَلۡقَيۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ وَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوۡجِۭ بَهِيجٖ
Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna.
阿拉伯语经注:
تَبۡصِرَةٗ وَذِكۡرَىٰ لِكُلِّ عَبۡدٖ مُّنِيبٖ
Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kurejea (kwa Mwenyezi Mungu).
阿拉伯语经注:
وَنَزَّلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ مُّبَٰرَكٗا فَأَنۢبَتۡنَا بِهِۦ جَنَّٰتٖ وَحَبَّ ٱلۡحَصِيدِ
Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyobarikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka za kuvunwa.
阿拉伯语经注:
وَٱلنَّخۡلَ بَاسِقَٰتٖ لَّهَا طَلۡعٞ نَّضِيدٞ
Na mitende mirefu yenye makole yaliyozaa kwa wingi.
阿拉伯语经注:
رِّزۡقٗا لِّلۡعِبَادِۖ وَأَحۡيَيۡنَا بِهِۦ بَلۡدَةٗ مَّيۡتٗاۚ كَذَٰلِكَ ٱلۡخُرُوجُ
Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyokuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyokuwa ufufuaji.
阿拉伯语经注:
كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحٖ وَأَصۡحَٰبُ ٱلرَّسِّ وَثَمُودُ
Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na wakazi wa Rassi na Thamudi.
阿拉伯语经注:
وَعَادٞ وَفِرۡعَوۡنُ وَإِخۡوَٰنُ لُوطٖ
Na A'di na Firauni na kaumu ya Luti.
阿拉伯语经注:
وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡأَيۡكَةِ وَقَوۡمُ تُبَّعٖۚ كُلّٞ كَذَّبَ ٱلرُّسُلَ فَحَقَّ وَعِيدِ
Na wakazi wa Machakani, na watu wa Tubbaa'. Wote hao waliwakanusha Mitume, kwa hivyo onyo likathibitika juu yao.
阿拉伯语经注:
أَفَعَيِينَا بِٱلۡخَلۡقِ ٱلۡأَوَّلِۚ بَلۡ هُمۡ فِي لَبۡسٖ مِّنۡ خَلۡقٖ جَدِيدٖ
Kwani tulichoka kwa kuumba mara ya kwanza? Bali wao wamo katika shaka tu juu ya umbo jipya.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ وَنَعۡلَمُ مَا تُوَسۡوِسُ بِهِۦ نَفۡسُهُۥۖ وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنۡ حَبۡلِ ٱلۡوَرِيدِ
Na hakika tulimuumba mtu, nasi tunayajua yanayomtia wasiwasi katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake.
阿拉伯语经注:
إِذۡ يَتَلَقَّى ٱلۡمُتَلَقِّيَانِ عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ قَعِيدٞ
Wanapopokea wapokeaji wawili, wanaokaa kuliani na kushotoni.
阿拉伯语经注:
مَّا يَلۡفِظُ مِن قَوۡلٍ إِلَّا لَدَيۡهِ رَقِيبٌ عَتِيدٞ
Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.
阿拉伯语经注:
وَجَآءَتۡ سَكۡرَةُ ٱلۡمَوۡتِ بِٱلۡحَقِّۖ ذَٰلِكَ مَا كُنتَ مِنۡهُ تَحِيدُ
Na uchungu wa kutoka roho utamjia kwa haki. Hayo ndiyo uliyokuwa ukiyakimbia.
阿拉伯语经注:
وَنُفِخَ فِي ٱلصُّورِۚ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلۡوَعِيدِ
Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi.
阿拉伯语经注:
وَجَآءَتۡ كُلُّ نَفۡسٖ مَّعَهَا سَآئِقٞ وَشَهِيدٞ
Na kila nafsi itakuja na pamoja nayo mchungaji na shahidi.
阿拉伯语经注:
لَّقَدۡ كُنتَ فِي غَفۡلَةٖ مِّنۡ هَٰذَا فَكَشَفۡنَا عَنكَ غِطَآءَكَ فَبَصَرُكَ ٱلۡيَوۡمَ حَدِيدٞ
(Aambiwe): 'Kwa hakika ulikuwa umeghafilika mbali na haya. Basi leo tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali mno.'
阿拉伯语经注:
وَقَالَ قَرِينُهُۥ هَٰذَا مَا لَدَيَّ عَتِيدٌ
Na mwenzake atasema: 'Huyu niliye naye mimi keshatayarishwa.
阿拉伯语经注:
أَلۡقِيَا فِي جَهَنَّمَ كُلَّ كَفَّارٍ عَنِيدٖ
Mtupeni katika Jahanamu kila kafiri mwenye inda.
阿拉伯语经注:
مَّنَّاعٖ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدٖ مُّرِيبٍ
Akatazaye mno heri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka.
阿拉伯语经注:
ٱلَّذِي جَعَلَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَأَلۡقِيَاهُ فِي ٱلۡعَذَابِ ٱلشَّدِيدِ
Aliyeweka mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu kali.'
阿拉伯语经注:
۞ قَالَ قَرِينُهُۥ رَبَّنَا مَآ أَطۡغَيۡتُهُۥ وَلَٰكِن كَانَ فِي ضَلَٰلِۭ بَعِيدٖ
Mwenzake aseme: 'Ewe Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali.'
阿拉伯语经注:
قَالَ لَا تَخۡتَصِمُواْ لَدَيَّ وَقَدۡ قَدَّمۡتُ إِلَيۡكُم بِٱلۡوَعِيدِ
(Mwenyezi Mungu) aseme: 'Msigombane mbele yangu. Tayari niliwaletea mbele onyo langu.
阿拉伯语经注:
مَا يُبَدَّلُ ٱلۡقَوۡلُ لَدَيَّ وَمَآ أَنَا۠ بِظَلَّٰمٖ لِّلۡعَبِيدِ
Mbele yangu haibadilishwi kauli, wala Mimi siwadhulumu waja wangu.
阿拉伯语经注:
يَوۡمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ ٱمۡتَلَأۡتِ وَتَقُولُ هَلۡ مِن مَّزِيدٖ
Siku tutakapoiambia Jahanamu: 'Je, umejaa?' Nayo itasema: 'Je, kuna ziada?'
阿拉伯语经注:
وَأُزۡلِفَتِ ٱلۡجَنَّةُ لِلۡمُتَّقِينَ غَيۡرَ بَعِيدٍ
Na Bustani ya mbinguni italetwa karibu mno kwa ajili ya wacha Mungu, haitakuwa mbali.
阿拉伯语经注:
هَٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِكُلِّ أَوَّابٍ حَفِيظٖ
Haya ndiyo mnayoahidiwa kwa kila mwenye kurejea mno kwa Mwenyezi Mungu na akajilinda vyema.
阿拉伯语经注:
مَّنۡ خَشِيَ ٱلرَّحۡمَٰنَ بِٱلۡغَيۡبِ وَجَآءَ بِقَلۡبٖ مُّنِيبٍ
Mwenye kumwogopa mno Mwingi wa rehema hali kuwa hamwoni, na akaja kwa moyo uliotubia.
阿拉伯语经注:
ٱدۡخُلُوهَا بِسَلَٰمٖۖ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلۡخُلُودِ
(Ataambiwa) ingieni humo kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya kudumu daima dawamu.
阿拉伯语经注:
لَهُم مَّا يَشَآءُونَ فِيهَا وَلَدَيۡنَا مَزِيدٞ
Humo watapata wakitakacho, na kwetu yako ya ziada.
阿拉伯语经注:
وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّن قَرۡنٍ هُمۡ أَشَدُّ مِنۡهُم بَطۡشٗا فَنَقَّبُواْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ هَلۡ مِن مَّحِيصٍ
Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, waliokuwa na nguvu zaidi kuliko hawa! Nao walitanga tanga katika nchi nyingi. Je, walipata pa kukimbilia?
阿拉伯语经注:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكۡرَىٰ لِمَن كَانَ لَهُۥ قَلۡبٌ أَوۡ أَلۡقَى ٱلسَّمۡعَ وَهُوَ شَهِيدٞ
Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٖ
Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita; na wala hayakutugusa machofu yoyote.
阿拉伯语经注:
فَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ قَبۡلَ طُلُوعِ ٱلشَّمۡسِ وَقَبۡلَ ٱلۡغُرُوبِ
Basi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa.
阿拉伯语经注:
وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَسَبِّحۡهُ وَأَدۡبَٰرَ ٱلسُّجُودِ
Na katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu.
阿拉伯语经注:
وَٱسۡتَمِعۡ يَوۡمَ يُنَادِ ٱلۡمُنَادِ مِن مَّكَانٖ قَرِيبٖ
Na sikiliza siku atakaponadi mwenye kunadi kutoka mahali karibu.
阿拉伯语经注:
يَوۡمَ يَسۡمَعُونَ ٱلصَّيۡحَةَ بِٱلۡحَقِّۚ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلۡخُرُوجِ
Siku watakaposikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya kufufuka.
阿拉伯语经注:
إِنَّا نَحۡنُ نُحۡيِۦ وَنُمِيتُ وَإِلَيۡنَا ٱلۡمَصِيرُ
Hakika Sisi tunahuisha na tunafisha, na kwetu Sisi ndio marejeo.
阿拉伯语经注:
يَوۡمَ تَشَقَّقُ ٱلۡأَرۡضُ عَنۡهُمۡ سِرَاعٗاۚ ذَٰلِكَ حَشۡرٌ عَلَيۡنَا يَسِيرٞ
Siku itapowapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi.
阿拉伯语经注:
نَّحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا يَقُولُونَۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡهِم بِجَبَّارٖۖ فَذَكِّرۡ بِٱلۡقُرۡءَانِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ
Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur-ani anayeliogopa onyo.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 嘎夫
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 - 译解目录

由拉瓦德翻译中心团队与拉布瓦 الدعوة协会和伊斯兰内容服务协会合作翻译。

关闭