Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 * - 译解目录


含义的翻译 章: 艾奈尔姆   段:

Al-An'am

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَجَعَلَ ٱلظُّلُمَٰتِ وَٱلنُّورَۖ ثُمَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِرَبِّهِمۡ يَعۡدِلُونَ
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye aliumba mbingu na ardhi, na akafanya giza mbalimbali na nuru. Kisha wale waliokufuru wanawafanya wengine kuwa sawa na Mola wao Mlezi.
阿拉伯语经注:
هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن طِينٖ ثُمَّ قَضَىٰٓ أَجَلٗاۖ وَأَجَلٞ مُّسَمًّى عِندَهُۥۖ ثُمَّ أَنتُمۡ تَمۡتَرُونَ
Yeye ndiye aliyewaumba kutokana na udongo, kisha akawahukumia muda, na muda maalumu uko kwake tu. Kisha nyinyi mnatia shaka.
阿拉伯语经注:
وَهُوَ ٱللَّهُ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَفِي ٱلۡأَرۡضِ يَعۡلَمُ سِرَّكُمۡ وَجَهۡرَكُمۡ وَيَعۡلَمُ مَا تَكۡسِبُونَ
Na Yeye ndiye Mwenyezi Mungu katika mbingu na katika ardhi. Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu. Na anajua mnayoyachuma.
阿拉伯语经注:
وَمَا تَأۡتِيهِم مِّنۡ ءَايَةٖ مِّنۡ ءَايَٰتِ رَبِّهِمۡ إِلَّا كَانُواْ عَنۡهَا مُعۡرِضِينَ
Na haiwajii ishara miongoni mwa ishara za Mola wao Mlezi isipokuwa walikuwa wakiipa mgongo.
阿拉伯语经注:
فَقَدۡ كَذَّبُواْ بِٱلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمۡ فَسَوۡفَ يَأۡتِيهِمۡ أَنۢبَٰٓؤُاْ مَا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ
Basi hakika walikwishaikadhibisha haki ilipowajia. Kwa hivyo, zitawajia habari za yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.
阿拉伯语经注:
أَلَمۡ يَرَوۡاْ كَمۡ أَهۡلَكۡنَا مِن قَبۡلِهِم مِّن قَرۡنٖ مَّكَّنَّٰهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مَا لَمۡ نُمَكِّن لَّكُمۡ وَأَرۡسَلۡنَا ٱلسَّمَآءَ عَلَيۡهِم مِّدۡرَارٗا وَجَعَلۡنَا ٱلۡأَنۡهَٰرَ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهِمۡ فَأَهۡلَكۡنَٰهُم بِذُنُوبِهِمۡ وَأَنشَأۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِمۡ قَرۡنًا ءَاخَرِينَ
Je, hawakuona ni vizazi vingapi tulivyoviangamiza kabla yao? Tuliwaimarisha katika dunia namna ambavyo hatukuwaimarisha nyinyi; na tukawatumia mvua nyingi na tukaifanya mito inapita kwa chini yao. Mwishowe tukawaangamiza kwa madhambi yao; na tukaanzisha baada yao kizazi kingine.
阿拉伯语经注:
وَلَوۡ نَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ كِتَٰبٗا فِي قِرۡطَاسٖ فَلَمَسُوهُ بِأَيۡدِيهِمۡ لَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ
Na lau tungelikuteremshia kitabu cha karatasi, wakakigusa kwa mikono yao, wangelisema wale waliokufuru: Haya si chochote isipokuwa ni uchawi ulio wazi.
阿拉伯语经注:
وَقَالُواْ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ مَلَكٞۖ وَلَوۡ أَنزَلۡنَا مَلَكٗا لَّقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ ثُمَّ لَا يُنظَرُونَ
Na walisema, "Mbona hakuteremshiwa Malaika?" Na kama tungelimteremsha Malaika, basi bila ya shaka ingeshahukumiwa amri, kisha wasingelipewa muhula.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 艾奈尔姆
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 - 译解目录

由拉瓦德翻译中心团队与拉布瓦 الدعوة协会和伊斯兰内容服务协会合作翻译。

关闭