prev

Al-Hashr

next

1 : 59

سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Vimemtakasa Allah Mtukufu na kila kisichonasibiana naye, vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini, na Yeye Ndiye Mshindi Asiyekuwa na mwenye kushindana naye, Mwingi wa hekima katika makadirio Yake, uendeshaji Wake na utengenezaji Wake na Sheria Zake, Anaweka kila jambo mahali pake panapostahiki. info
التفاسير: |

2 : 59

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ مِن دِيَٰرِهِمۡ لِأَوَّلِ ٱلۡحَشۡرِۚ مَا ظَنَنتُمۡ أَن يَخۡرُجُواْۖ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُم مَّانِعَتُهُمۡ حُصُونُهُم مِّنَ ٱللَّهِ فَأَتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِنۡ حَيۡثُ لَمۡ يَحۡتَسِبُواْۖ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ ٱلرُّعۡبَۚ يُخۡرِبُونَ بُيُوتَهُم بِأَيۡدِيهِمۡ وَأَيۡدِي ٱلۡمُؤۡمِنِينَ فَٱعۡتَبِرُواْ يَٰٓأُوْلِي ٱلۡأَبۡصَٰرِ

Yeye, kutakasika ni Kwake, Ndiye Aliyewatoa wale walioukanusha unabii wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), miongoni mwa watu waliopewa Kitabu, nao ni Mayahudi wa ukoo wa (Banū al Naḍīr), kutoka majumbani mwao ambayo wakiwa humo walikuwa ni majirani na Waislamu pembezoni mwa Madina. Huko kulikuwa ndio mwanzo wa kutolewa nje ya Bara Arabu hadi Shām. Hamkudhani, (enyi Waislamu), kuwa watatoka majumbani mwao kwa unyonge huu na utwevu, kwa silaha kali walizokua nazo na ngome waliokuwa nayo. Na walidhani Mayahudi kuwa ngome zao zitawakinga na adhabu ya Allah Mtukufu na kuwa hakuna anayeziweza. Basi amri ya Allah Mtukufu ilizijia kwa namna ambayo haikupita kwenye akili zao, na Allah Mtukufu Akawatia hofu kubwa, wakawa wanazivunja nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya waumini pia ikazivunja, basi zingatieni, enyi wenye busara timamu na akili nyingi kwa hayo yaliyowafika wao. info
التفاسير: |

3 : 59

وَلَوۡلَآ أَن كَتَبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمُ ٱلۡجَلَآءَ لَعَذَّبَهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَاۖ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابُ ٱلنَّارِ

Na lau si Allah Mtukufu kupitisha na kuamua kuwa watoke kwenye miji yao angewaadhibu duniani kwa kuuawa na kutekwa, na huko Akhera watakuwa na adhabu ya Motoni. info
التفاسير: |
prev

Al-Hashr

next
:
0:00 0:00