Check out the new design

আল-কোৰআনুল কাৰীমৰ অৰ্থানুবাদ - শ্বাহিলি অনুবাদ- ৰুওৱাদ অনুবাদ চেণ্টাৰ * - অনুবাদসমূহৰ সূচীপত্ৰ


অৰ্থানুবাদ ছুৰা: আল-হিজৰ   আয়াত:

Al-hijr

الٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ وَقُرۡءَانٖ مُّبِينٖ
Alif Lam Ra.[1] Hizi ni Aya za Kitabu na Qur-ani inayobainisha.
[1] Herufi hizi "Alif Laam Raa" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
رُّبَمَا يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡ كَانُواْ مُسۡلِمِينَ
Huenda ikawa wale waliokufuru wakatamani kwamba wangekuwa Waislamu.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
ذَرۡهُمۡ يَأۡكُلُواْ وَيَتَمَتَّعُواْ وَيُلۡهِهِمُ ٱلۡأَمَلُۖ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ
Waache wale, na wastarehe, na yawazuge matumaini. Basi watakujajua.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَمَآ أَهۡلَكۡنَا مِن قَرۡيَةٍ إِلَّا وَلَهَا كِتَابٞ مَّعۡلُومٞ
Na hatukuuangamiza mji wowote ule isipokuwa ulikuwa na muda wake maalumu ulioandikiwa.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
مَّا تَسۡبِقُ مِنۡ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ
Hawawezi umma wowote kuutangulia muda wao, wala kuchelewa.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَقَالُواْ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِي نُزِّلَ عَلَيۡهِ ٱلذِّكۡرُ إِنَّكَ لَمَجۡنُونٞ
Na walisema, "Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
لَّوۡمَا تَأۡتِينَا بِٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli?"
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
مَا نُنَزِّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَمَا كَانُوٓاْ إِذٗا مُّنظَرِينَ
Sisi hatuwateremshi Malaika isipokuwa kwa sababu ya haki, na hapo hawatapewa muhula.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا ٱلذِّكۡرَ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ
Hakika Sisi ndio tuliouteremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakaoulinda.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ فِي شِيَعِ ٱلۡأَوَّلِينَ
Na hakika tulikwishatuma Mitume kabla yako kwa mataifa ya mwanzo.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَمَا يَأۡتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ
Na hakuwajia Mtume yeyote isipokuwa walikuwa wakimfanyia stihizai.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
كَذَٰلِكَ نَسۡلُكُهُۥ فِي قُلُوبِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ
Na kama hivi ndivyo tunavyoyaingiza katika nyoyo za wahalifu.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
لَا يُؤۡمِنُونَ بِهِۦ وَقَدۡ خَلَتۡ سُنَّةُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Hawayaamini haya, na ilhali imekwishawapitia desturi ya wa mwanzo.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَلَوۡ فَتَحۡنَا عَلَيۡهِم بَابٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فَظَلُّواْ فِيهِ يَعۡرُجُونَ
Na lau tungeliwafungulia mlango huko mbinguni, wakawa wanapanda kupitia humo,
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
لَقَالُوٓاْ إِنَّمَا سُكِّرَتۡ أَبۡصَٰرُنَا بَلۡ نَحۡنُ قَوۡمٞ مَّسۡحُورُونَ
Basi wangelisema: Hakika macho yetu yameleweshwa tu. Bali sisi wenyewe ni kaumu tuliofanyiwa uchawi.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَلَقَدۡ جَعَلۡنَا فِي ٱلسَّمَآءِ بُرُوجٗا وَزَيَّنَّٰهَا لِلنَّٰظِرِينَ
Na hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari, na tumezipamba kwa wenye kuangalia.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَحَفِظۡنَٰهَا مِن كُلِّ شَيۡطَٰنٖ رَّجِيمٍ
Na tumezilinda kutokana na kila shetani aliyelaaniwa.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِلَّا مَنِ ٱسۡتَرَقَ ٱلسَّمۡعَ فَأَتۡبَعَهُۥ شِهَابٞ مُّبِينٞ
Isipokuwa mwenye kusikiliza kwa kuibia, naye hufuatwa na kijinga cha moto kilicho dhahiri.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَٱلۡأَرۡضَ مَدَدۡنَٰهَا وَأَلۡقَيۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ وَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ شَيۡءٖ مَّوۡزُونٖ
Na ardhi tumeitandaza, na humo tumeweka milima madhubuti, na tumeotesha ndani yake katika kila kitu kwa kiasi chake.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَجَعَلۡنَا لَكُمۡ فِيهَا مَعَٰيِشَ وَمَن لَّسۡتُمۡ لَهُۥ بِرَٰزِقِينَ
Na tumewafanyia humo vitu vya maisha yenu, na ya hao ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَإِن مِّن شَيۡءٍ إِلَّا عِندَنَا خَزَآئِنُهُۥ وَمَا نُنَزِّلُهُۥٓ إِلَّا بِقَدَرٖ مَّعۡلُومٖ
Na hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi; wala hatukiteremshi isipokuwa kwa kipimo maalumu.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَأَرۡسَلۡنَا ٱلرِّيَٰحَ لَوَٰقِحَ فَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَسۡقَيۡنَٰكُمُوهُ وَمَآ أَنتُمۡ لَهُۥ بِخَٰزِنِينَ
Na tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mbinguni maji, kisha tukakunywesheni maji hayo. Wala si nyinyi mnayoyaweka.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَإِنَّا لَنَحۡنُ نُحۡيِۦ وَنُمِيتُ وَنَحۡنُ ٱلۡوَٰرِثُونَ
Na hakika Sisi ndio tunaohuisha na tunaofisha. Na Sisi ndio Warithi.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَلَقَدۡ عَلِمۡنَا ٱلۡمُسۡتَقۡدِمِينَ مِنكُمۡ وَلَقَدۡ عَلِمۡنَا ٱلۡمُسۡتَـٔۡخِرِينَ
Na hakika tunawajua waliotangulia katika nyinyi, na tunawajua waliobaki nyuma.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحۡشُرُهُمۡۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٞ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye atakayewakusanya. Hakika Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye kujua mno.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ
Na hakika tulimuumba Mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَٱلۡجَآنَّ خَلَقۡنَٰهُ مِن قَبۡلُ مِن نَّارِ ٱلسَّمُومِ
Naye Jini tulimuumba hapo kabla kutokana na moto wa upepo umoto.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَإِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ إِنِّي خَٰلِقُۢ بَشَرٗا مِّن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ
Na Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
فَإِذَا سَوَّيۡتُهُۥ وَنَفَخۡتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُواْ لَهُۥ سَٰجِدِينَ
Basi nitakapomtengeneza sawasawa, na nikampulizia roho yangu, basi angukeni kumsujudia.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
فَسَجَدَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ كُلُّهُمۡ أَجۡمَعُونَ
Basi Malaika wote pamoja walimsujudia.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰٓ أَن يَكُونَ مَعَ ٱلسَّٰجِدِينَ
Isipokuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na waliosujudu.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالَ يَٰٓإِبۡلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ ٱلسَّٰجِدِينَ
(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na waliosujudu?
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالَ لَمۡ أَكُن لِّأَسۡجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقۡتَهُۥ مِن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ
Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliyemuumba kutokana na udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالَ فَٱخۡرُجۡ مِنۡهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٞ
(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umefukuziliwa mbali!
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَإِنَّ عَلَيۡكَ ٱللَّعۡنَةَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلدِّينِ
Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالَ رَبِّ فَأَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ
Akasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watakapofufuliwa.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ
(Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika waliopewa muhula.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡوَقۡتِ ٱلۡمَعۡلُومِ
Mpaka siku ya wakati maalumu.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالَ رَبِّ بِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَأُغۡوِيَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyokuwa umenipoteza, basi hakika nitawapambia katika dunia na hakika nitawapoteza wote.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِلَّا عِبَادَكَ مِنۡهُمُ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Isipokuwa waja wako walioteuliwa miongoni mwao.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالَ هَٰذَا صِرَٰطٌ عَلَيَّ مُسۡتَقِيمٌ
Akasema: Hii ni njia ya kujia kwangu iliyonyooka.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِنَّ عِبَادِي لَيۡسَ لَكَ عَلَيۡهِمۡ سُلۡطَٰنٌ إِلَّا مَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡغَاوِينَ
Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipokuwa wale wapotofu waliokufuata.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوۡعِدُهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Na hakika Jahannamu ndipo mahali pao walipoahidiwa wote.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
لَهَا سَبۡعَةُ أَبۡوَٰبٖ لِّكُلِّ بَابٖ مِّنۡهُمۡ جُزۡءٞ مَّقۡسُومٌ
Ina milango saba; kila mlango ulitengewa sehemu miongoni mwao.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٍ
Hakika wachamungu watakuwa katika Mabustani na chemchemi.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
ٱدۡخُلُوهَا بِسَلَٰمٍ ءَامِنِينَ
(Wataambiwa:) Ingieni humo kwa salama na amani.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَنَزَعۡنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنۡ غِلٍّ إِخۡوَٰنًا عَلَىٰ سُرُرٖ مُّتَقَٰبِلِينَ
Na tutaondoa chuki iliyokuwa vifuani mwao, wawe ndugu, juu ya viti vya kifahari huku wameelekeana.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
لَا يَمَسُّهُمۡ فِيهَا نَصَبٞ وَمَا هُم مِّنۡهَا بِمُخۡرَجِينَ
Humo hayatawagusa machovu, wala hawatatolewa humo.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
۞ نَبِّئۡ عِبَادِيٓ أَنِّيٓ أَنَا ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
Wape habari waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe zaidi, Mwingi wa kurehemu.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ ٱلۡعَذَابُ ٱلۡأَلِيمُ
Na kwamba adhabu yangu ndiyo adhabu iliyo chungu!
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَنَبِّئۡهُمۡ عَن ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ
Na wape habari za wageni wa Ibrahim.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗا قَالَ إِنَّا مِنكُمۡ وَجِلُونَ
Walipoingia kwake na wakasema: Salama! Yeye akasema: Hakika sisi tunawaogopa.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالُواْ لَا تَوۡجَلۡ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ
Wakasema: Usiogope. Hakika, Sisi tunakubashiria kijana mwenye elimu mno.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالَ أَبَشَّرۡتُمُونِي عَلَىٰٓ أَن مَّسَّنِيَ ٱلۡكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ
Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi ni kwa njia gani mnanibashiria?
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالُواْ بَشَّرۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡقَٰنِطِينَ
Wakasema: Tunakubashiria kwa haki, basi usiwe miongoni mwa wanaokata tamaa.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالَ وَمَن يَقۡنَطُ مِن رَّحۡمَةِ رَبِّهِۦٓ إِلَّا ٱلضَّآلُّونَ
Akasema: Na ni nani anayekata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi isipokuwa wapotovu?
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ
Akasema: Hebu mna jambo gani, enyi wajumbe?
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمٖ مُّجۡرِمِينَ
Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wahalifu!
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Isipokuwa watu wa familia ya Lut'. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ قَدَّرۡنَآ إِنَّهَا لَمِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ
Isipokuwa mkewe. Tumekwishapitisha kwamba huyo hakika atakuwa miongoni mwa watakaosalia nyuma.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
فَلَمَّا جَآءَ ءَالَ لُوطٍ ٱلۡمُرۡسَلُونَ
Basi wajumbe hao walipowajia watu wa familia ya Lut'.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالَ إِنَّكُمۡ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ
(Lut') Alisema: Hakika nyinyi ni kaumu msiojulikana.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالُواْ بَلۡ جِئۡنَٰكَ بِمَا كَانُواْ فِيهِ يَمۡتَرُونَ
Wakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyokuwa wakiyafanyia shaka.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَأَتَيۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ
Na tumekujia kwa Haki, na hakika sisi ni wakweli.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
فَأَسۡرِ بِأَهۡلِكَ بِقِطۡعٖ مِّنَ ٱلَّيۡلِ وَٱتَّبِعۡ أَدۡبَٰرَهُمۡ وَلَا يَلۡتَفِتۡ مِنكُمۡ أَحَدٞ وَٱمۡضُواْ حَيۡثُ تُؤۡمَرُونَ
Basi ondoka na ahali zako usiku ungalipo, nawe ufuate nyuma yao, wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende huko mnakoamrishwa.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَقَضَيۡنَآ إِلَيۡهِ ذَٰلِكَ ٱلۡأَمۡرَ أَنَّ دَابِرَ هَٰٓؤُلَآءِ مَقۡطُوعٞ مُّصۡبِحِينَ
Na tukamfunulia hukumu hiyo, ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi atakuwa amekwishakatiliwa mbali.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَجَآءَ أَهۡلُ ٱلۡمَدِينَةِ يَسۡتَبۡشِرُونَ
Na wakaja watu wa mji huo huku wamefurahi.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالَ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ ضَيۡفِي فَلَا تَفۡضَحُونِ
Akasema: Hakika hawa ni wageni wangu. Basi msinifedheheshe.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ
Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالُوٓاْ أَوَلَمۡ نَنۡهَكَ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Wakasema: Kwani hatukukukataza (kuwakaribisha) walimwengu hawa?
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
قَالَ هَٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِيٓ إِن كُنتُمۡ فَٰعِلِينَ
Akasema, "Hawa binti zangu (waoeni)[1], ikiwa nyinyi ni watendaji."
[1] Lut'i, amani iwe juu yake, alimaanisha kwamba hawa ni binti zangu miongoni mwa wanawake wenu, basi waoeni hao.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
لَعَمۡرُكَ إِنَّهُمۡ لَفِي سَكۡرَتِهِمۡ يَعۡمَهُونَ
Ninaapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ مُشۡرِقِينَ
Basi ukelele ukawatwaa wakipambaukiwa.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
فَجَعَلۡنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةٗ مِّن سِجِّيلٍ
Kwa hivyo, tukaugeuza mji huo juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa kutoka Motoni.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّلۡمُتَوَسِّمِينَ
Hakika katika hayo zipo ishara kwa wanaotafakari na kuzingatia.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٖ مُّقِيمٍ
Na hakika miji hii ipo kwenye njia wazi inayopitiwa.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ
Hakika katika hayo ipo ishara kwa Waumini.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَإِن كَانَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأَيۡكَةِ لَظَٰلِمِينَ
Na hakika watu wa Kichakani walikuwa madhalimu.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
فَٱنتَقَمۡنَا مِنۡهُمۡ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٖ مُّبِينٖ
Kwa hivyo tukawaadhibu. Na hakika miji miwili hii iko kwenye njia iliyo wazi.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَلَقَدۡ كَذَّبَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡحِجۡرِ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na bila ya shaka wakazi wa Hijr waliwakadhibisha Mitume.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَءَاتَيۡنَٰهُمۡ ءَايَٰتِنَا فَكَانُواْ عَنۡهَا مُعۡرِضِينَ
Na tuliwaletea ishara zetu, nao wakawa wanazipa migongo.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَكَانُواْ يَنۡحِتُونَ مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتًا ءَامِنِينَ
Nao walikuwa wakichonga majumba katika milima kwa amani.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ مُصۡبِحِينَ
Basi ukelele ukawatwaa asubuhi.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
فَمَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Na hayakuwafaa yale waliyokuwa wakiyachuma.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۗ وَإِنَّ ٱلسَّاعَةَ لَأٓتِيَةٞۖ فَٱصۡفَحِ ٱلصَّفۡحَ ٱلۡجَمِيلَ
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo ndani yake isipokuwa kwa haki. Na hakika Saa ya Kiyama itafika. Basi samehe msamaha mzuri.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡخَلَّٰقُ ٱلۡعَلِيمُ
Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji, Mwenye kujua zaidi.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَٰكَ سَبۡعٗا مِّنَ ٱلۡمَثَانِي وَٱلۡقُرۡءَانَ ٱلۡعَظِيمَ
Na hakika tumekupa (aya) saba zinazosomwa mara kwa mara, na Qur-ani Tukufu.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
لَا تَمُدَّنَّ عَيۡنَيۡكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعۡنَا بِهِۦٓ أَزۡوَٰجٗا مِّنۡهُمۡ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَٱخۡفِضۡ جَنَاحَكَ لِلۡمُؤۡمِنِينَ
Kamwe usivinyoshee macho yako vitu tulivyowastarehesha kwavyo makundi fulani kati yao, wala usiwahuzunikie. Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَقُلۡ إِنِّيٓ أَنَا ٱلنَّذِيرُ ٱلۡمُبِينُ
Na sema: Hakika mimi ndiye mwonyaji mwenye kubainisha.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
كَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَى ٱلۡمُقۡتَسِمِينَ
Kama hivyo tuliwateremshia waliogawa.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
ٱلَّذِينَ جَعَلُواْ ٱلۡقُرۡءَانَ عِضِينَ
Ambao waliifanya Qur-ani vipande vipande.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
فَوَرَبِّكَ لَنَسۡـَٔلَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Basi ninaapa kwa Mola wako Mlezi! Lazima tutawauliza wote.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Kuhusu yale waliyokuwa wakiyatenda.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
فَٱصۡدَعۡ بِمَا تُؤۡمَرُ وَأَعۡرِضۡ عَنِ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Basi wewe yadhihirishe yale uliyoamrishwa, na jitenge mbali na washirikina.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِنَّا كَفَيۡنَٰكَ ٱلۡمُسۡتَهۡزِءِينَ
Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanaofanya stihizai.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
ٱلَّذِينَ يَجۡعَلُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۚ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ
Ambao wanafanya mungu mwingine kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi watakujajua!
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَلَقَدۡ نَعۡلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدۡرُكَ بِمَا يَقُولُونَ
Na Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ ٱلسَّٰجِدِينَ
Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumsifu, na uwe miongoni mwa wanaomsujudia.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَٱعۡبُدۡ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأۡتِيَكَ ٱلۡيَقِينُ
Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
 
অৰ্থানুবাদ ছুৰা: আল-হিজৰ
ছুৰাৰ তালিকা পৃষ্ঠা নং
 
আল-কোৰআনুল কাৰীমৰ অৰ্থানুবাদ - শ্বাহিলি অনুবাদ- ৰুওৱাদ অনুবাদ চেণ্টাৰ - অনুবাদসমূহৰ সূচীপত্ৰ

অনুবাদ কৰিছে جمعية الدعوة بالربوة আৰু جمعية خدمة المحتوى الإسلامي باللغاتৰ সহযোগত মৰ্কজ ৰুৱাদুত তাৰ্জামাৰ অনুবাদক গোষ্ঠীয়ে।

বন্ধ