Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 * - 译解目录


含义的翻译 章: 哈吉拉   段:

Al-hijr

الٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ وَقُرۡءَانٖ مُّبِينٖ
Alif Lam Ra. Hizi ni Aya za Kitabu na Qur-ani inayobainisha.
阿拉伯语经注:
رُّبَمَا يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡ كَانُواْ مُسۡلِمِينَ
Huenda ikawa wale waliokufuru wakatamani kwamba wangekuwa Waislamu.
阿拉伯语经注:
ذَرۡهُمۡ يَأۡكُلُواْ وَيَتَمَتَّعُواْ وَيُلۡهِهِمُ ٱلۡأَمَلُۖ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ
Waache wale, na wastarehe, na yawazuge matumaini. Watakuja jua.
阿拉伯语经注:
وَمَآ أَهۡلَكۡنَا مِن قَرۡيَةٍ إِلَّا وَلَهَا كِتَابٞ مَّعۡلُومٞ
Na hatukuuangamiza mji wowote ule isipokuwa ulikuwa na muda wake maalumu.
阿拉伯语经注:
مَّا تَسۡبِقُ مِنۡ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ
Hawawezi umma wowote kuutangulia muda wao, wala kuchelewa.
阿拉伯语经注:
وَقَالُواْ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِي نُزِّلَ عَلَيۡهِ ٱلذِّكۡرُ إِنَّكَ لَمَجۡنُونٞ
Na walisema, "Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu.
阿拉伯语经注:
لَّوۡمَا تَأۡتِينَا بِٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli?
阿拉伯语经注:
مَا نُنَزِّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَمَا كَانُوٓاْ إِذٗا مُّنظَرِينَ
Sisi hatuwateremshi Malaika isipokuwa kwa sababu ya haki, na hapo hawatapewa muhula.
阿拉伯语经注:
إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا ٱلذِّكۡرَ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ
Hakika Sisi ndio tuliouteremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakoulinda.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ فِي شِيَعِ ٱلۡأَوَّلِينَ
Na hakika tulikwisha watumia Mitume mataifa ya mwanzo.
阿拉伯语经注:
وَمَا يَأۡتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ
Na hakuwajia Mtume isipokuwa walikuwa wakimfanyia stihizai.
阿拉伯语经注:
كَذَٰلِكَ نَسۡلُكُهُۥ فِي قُلُوبِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ
Na kama hivi ndivyo tunavyoyaingiza katika nyoyo za wakosefu.
阿拉伯语经注:
لَا يُؤۡمِنُونَ بِهِۦ وَقَدۡ خَلَتۡ سُنَّةُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Hawayaamini haya, na ilhali imekwisha wapitia desturi ya wa mwanzo.
阿拉伯语经注:
وَلَوۡ فَتَحۡنَا عَلَيۡهِم بَابٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فَظَلُّواْ فِيهِ يَعۡرُجُونَ
Na lau tungeliwafungulia mlango huko mbinguni, wakawa wanapanda kupitia humo,
阿拉伯语经注:
لَقَالُوٓاْ إِنَّمَا سُكِّرَتۡ أَبۡصَٰرُنَا بَلۡ نَحۡنُ قَوۡمٞ مَّسۡحُورُونَ
Basi wangelisema: Hakika macho yetu yameleweshwa tu. Bali sisi wenyewe ni kaumu tuliofanyiwa uchawi.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ جَعَلۡنَا فِي ٱلسَّمَآءِ بُرُوجٗا وَزَيَّنَّٰهَا لِلنَّٰظِرِينَ
Na hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari, na tumezipamba kwa wenye kuangalia.
阿拉伯语经注:
وَحَفِظۡنَٰهَا مِن كُلِّ شَيۡطَٰنٖ رَّجِيمٍ
Na tumezilinda kutokana na kila shetani aliyelaaniwa.
阿拉伯语经注:
إِلَّا مَنِ ٱسۡتَرَقَ ٱلسَّمۡعَ فَأَتۡبَعَهُۥ شِهَابٞ مُّبِينٞ
Isipokuwa mwenye kusikiliza kwa kuibia, naye hufuatwa na kijinga cha moto kilicho dhahiri.
阿拉伯语经注:
وَٱلۡأَرۡضَ مَدَدۡنَٰهَا وَأَلۡقَيۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ وَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ شَيۡءٖ مَّوۡزُونٖ
Na ardhi tumeitandaza, na humo tumeweka milima madhubuti, na tumeotesha katika kila kitu kwa kiasi chake.
阿拉伯语经注:
وَجَعَلۡنَا لَكُمۡ فِيهَا مَعَٰيِشَ وَمَن لَّسۡتُمۡ لَهُۥ بِرَٰزِقِينَ
Na tumewajaalia humo vitu vya maisha yenu, na ya hao ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku.
阿拉伯语经注:
وَإِن مِّن شَيۡءٍ إِلَّا عِندَنَا خَزَآئِنُهُۥ وَمَا نُنَزِّلُهُۥٓ إِلَّا بِقَدَرٖ مَّعۡلُومٖ
Na hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi; wala hatukiteremshi isipokuwa kwa kipimo maalumu.
阿拉伯语经注:
وَأَرۡسَلۡنَا ٱلرِّيَٰحَ لَوَٰقِحَ فَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَسۡقَيۡنَٰكُمُوهُ وَمَآ أَنتُمۡ لَهُۥ بِخَٰزِنِينَ
Na tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mbinguni maji, kisha tukakunywesheni maji hayo. Wala si nyinyi mnayoyaweka.
阿拉伯语经注:
وَإِنَّا لَنَحۡنُ نُحۡيِۦ وَنُمِيتُ وَنَحۡنُ ٱلۡوَٰرِثُونَ
Na hakika Sisi ndio tunaohuisha na tunaofisha. Na Sisi ndio Warithi.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ عَلِمۡنَا ٱلۡمُسۡتَقۡدِمِينَ مِنكُمۡ وَلَقَدۡ عَلِمۡنَا ٱلۡمُسۡتَـٔۡخِرِينَ
Na hakika tunawajua waliotangulia katika nyinyi, na tunawajua waliobaki nyuma.
阿拉伯语经注:
وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحۡشُرُهُمۡۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٞ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye atakayewakusanya. Hakika Yeye ni Mwenye hekima, Mjuzi.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ
Na hakika tulimuumba Mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura.
阿拉伯语经注:
وَٱلۡجَآنَّ خَلَقۡنَٰهُ مِن قَبۡلُ مِن نَّارِ ٱلسَّمُومِ
Naye Jini tulimuumba hapo kabla kutokana na moto wa upepo moto.
阿拉伯语经注:
وَإِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ إِنِّي خَٰلِقُۢ بَشَرٗا مِّن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ
Na Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura.
阿拉伯语经注:
فَإِذَا سَوَّيۡتُهُۥ وَنَفَخۡتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُواْ لَهُۥ سَٰجِدِينَ
Basi nitakapomtengeneza sawasawa, na nikampulizia roho yangu, basi mmwangukie kumsujudia.
阿拉伯语经注:
فَسَجَدَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ كُلُّهُمۡ أَجۡمَعُونَ
Basi Malaika wote pamoja walimsujudia.
阿拉伯语经注:
إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰٓ أَن يَكُونَ مَعَ ٱلسَّٰجِدِينَ
Isipokuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na waliosujudu.
阿拉伯语经注:
قَالَ يَٰٓإِبۡلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ ٱلسَّٰجِدِينَ
(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na waliosujudu?
阿拉伯语经注:
قَالَ لَمۡ أَكُن لِّأَسۡجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقۡتَهُۥ مِن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ
Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliyemuumba kutokana na udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura.
阿拉伯语经注:
قَالَ فَٱخۡرُجۡ مِنۡهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٞ
(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umefukuziliwa mbali!
阿拉伯语经注:
وَإِنَّ عَلَيۡكَ ٱللَّعۡنَةَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلدِّينِ
Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo.
阿拉伯语经注:
قَالَ رَبِّ فَأَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ
Akasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watakapofufuliwa.
阿拉伯语经注:
قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ
(Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika waliopewa muhula.
阿拉伯语经注:
إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡوَقۡتِ ٱلۡمَعۡلُومِ
Mpaka siku ya wakati maalumu.
阿拉伯语经注:
قَالَ رَبِّ بِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَأُغۡوِيَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyokuwa umenitia makosani, basi hakika nitawapambia katika dunia na hakika nitawapoteza wote.
阿拉伯语经注:
إِلَّا عِبَادَكَ مِنۡهُمُ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Isipokuwa waja wako walioteuliwa miongoni mwao.
阿拉伯语经注:
قَالَ هَٰذَا صِرَٰطٌ عَلَيَّ مُسۡتَقِيمٌ
Akasema: Hii ni njia ya kujia kwangu iliyonyooka.
阿拉伯语经注:
إِنَّ عِبَادِي لَيۡسَ لَكَ عَلَيۡهِمۡ سُلۡطَٰنٌ إِلَّا مَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡغَاوِينَ
Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipokuwa wale wapotofu waliokufuata.
阿拉伯语经注:
وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوۡعِدُهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Na hakika Jahannamu ndipo mahali pao walipoahidiwa wote.
阿拉伯语经注:
لَهَا سَبۡعَةُ أَبۡوَٰبٖ لِّكُلِّ بَابٖ مِّنۡهُمۡ جُزۡءٞ مَّقۡسُومٌ
Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu waliotengewa.
阿拉伯语经注:
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٍ
Hakika wachamungu watakuwa katika Mabustani na chemchemi.
阿拉伯语经注:
ٱدۡخُلُوهَا بِسَلَٰمٍ ءَامِنِينَ
(Wataambiwa:) Ingieni humo kwa salama na amani.
阿拉伯语经注:
وَنَزَعۡنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنۡ غِلٍّ إِخۡوَٰنًا عَلَىٰ سُرُرٖ مُّتَقَٰبِلِينَ
Na tutaondoa chuki iliyokuwa vifuani mwao, wawe ndugu, juu ya viti vya enzi huku wameelekeana.
阿拉伯语经注:
لَا يَمَسُّهُمۡ فِيهَا نَصَبٞ وَمَا هُم مِّنۡهَا بِمُخۡرَجِينَ
Humo hayatawagusa machovu, wala hawatatolewa humo.
阿拉伯语经注:
۞ نَبِّئۡ عِبَادِيٓ أَنِّيٓ أَنَا ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
Wape habari waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe zaidi, Mwingi wa kurehemu.
阿拉伯语经注:
وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ ٱلۡعَذَابُ ٱلۡأَلِيمُ
Na kwamba adhabu yangu ndiyo adhabu iliyo chungu!
阿拉伯语经注:
وَنَبِّئۡهُمۡ عَن ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ
Na wape habari za wageni wa Ibrahim.
阿拉伯语经注:
إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗا قَالَ إِنَّا مِنكُمۡ وَجِلُونَ
Walipoingia kwake na wakasema: Salama! Yeye akasema: Hakika sisi tunawaogopa.
阿拉伯语经注:
قَالُواْ لَا تَوۡجَلۡ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ
Wakasema: Usiogope. Hakika, Sisi tunakubashiria kijana mwenye elimu mno.
阿拉伯语经注:
قَالَ أَبَشَّرۡتُمُونِي عَلَىٰٓ أَن مَّسَّنِيَ ٱلۡكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ
Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanibashiria?
阿拉伯语经注:
قَالُواْ بَشَّرۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡقَٰنِطِينَ
Wakasema: Tunakubashiria kwa haki, basi usiwe miongoni mwa wanaokata tamaa.
阿拉伯语经注:
قَالَ وَمَن يَقۡنَطُ مِن رَّحۡمَةِ رَبِّهِۦٓ إِلَّا ٱلضَّآلُّونَ
Akasema: Na ni nani anayekata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi isipokuwa wapotovu?
阿拉伯语经注:
قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ
Akasema: Hebu mna jambo gani, enyi wajumbe?
阿拉伯语经注:
قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمٖ مُّجۡرِمِينَ
Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wahalifu!
阿拉伯语经注:
إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Isipokuwa watu wa familia ya Lut'. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote.
阿拉伯语经注:
إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ قَدَّرۡنَآ إِنَّهَا لَمِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ
Isipokuwa mkewe. Tumekwisha pitisha kwamba huyo hakika atakuwa miongoni mwa watakaobakia nyuma.
阿拉伯语经注:
فَلَمَّا جَآءَ ءَالَ لُوطٍ ٱلۡمُرۡسَلُونَ
Basi wale wajumbe walipowajia watu wa familia ya Lut'.
阿拉伯语经注:
قَالَ إِنَّكُمۡ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ
(Lut') Alisema: Hakika nyinyi ni kaumu msiojulikana.
阿拉伯语经注:
قَالُواْ بَلۡ جِئۡنَٰكَ بِمَا كَانُواْ فِيهِ يَمۡتَرُونَ
Wakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyokuwa wakiyafanyia shaka.
阿拉伯语经注:
وَأَتَيۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ
Na tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi ni wakweli.
阿拉伯语经注:
فَأَسۡرِ بِأَهۡلِكَ بِقِطۡعٖ مِّنَ ٱلَّيۡلِ وَٱتَّبِعۡ أَدۡبَٰرَهُمۡ وَلَا يَلۡتَفِتۡ مِنكُمۡ أَحَدٞ وَٱمۡضُواْ حَيۡثُ تُؤۡمَرُونَ
Basi ondoka na ahali zako usiku ungalipo, nawe ufuate nyuma yao, wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende huko mnakoamrishwa.
阿拉伯语经注:
وَقَضَيۡنَآ إِلَيۡهِ ذَٰلِكَ ٱلۡأَمۡرَ أَنَّ دَابِرَ هَٰٓؤُلَآءِ مَقۡطُوعٞ مُّصۡبِحِينَ
Na tukamfunulia hukumu hiyo, ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi atakuwa amekwisha katiliwa mbali.
阿拉伯语经注:
وَجَآءَ أَهۡلُ ٱلۡمَدِينَةِ يَسۡتَبۡشِرُونَ
Na wakaja watu wa mji ule huku wamefurahi.
阿拉伯语经注:
قَالَ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ ضَيۡفِي فَلَا تَفۡضَحُونِ
Akasema: Hakika hawa ni wageni wangu. Basi msinifedheheshe.
阿拉伯语经注:
وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ
Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi.
阿拉伯语经注:
قَالُوٓاْ أَوَلَمۡ نَنۡهَكَ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Wakasema: Kwani hatukukukataza (kuwakaribisha) walimwengu hawa?
阿拉伯语经注:
قَالَ هَٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِيٓ إِن كُنتُمۡ فَٰعِلِينَ
Akasema, "Hawa binti zangu, ikiwa nyinyi ni watendaji."
阿拉伯语经注:
لَعَمۡرُكَ إِنَّهُمۡ لَفِي سَكۡرَتِهِمۡ يَعۡمَهُونَ
Ninaapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo.
阿拉伯语经注:
فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ مُشۡرِقِينَ
Basi ukelele ukawatwaa wakipambaukiwa.
阿拉伯语经注:
فَجَعَلۡنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةٗ مِّن سِجِّيلٍ
Kwa hivyo, tukaugeuza mji huo juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa kutoka Motoni.
阿拉伯语经注:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّلۡمُتَوَسِّمِينَ
Hakika katika hayo zipo ishara kwa wanaotafakari na kuzingatia.
阿拉伯语经注:
وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٖ مُّقِيمٍ
Na hakika miji hii ipo kwenye njia inayopitiwa.
阿拉伯语经注:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ
Hakika katika hayo ipo ishara kwa Waumini.
阿拉伯语经注:
وَإِن كَانَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأَيۡكَةِ لَظَٰلِمِينَ
Na hakika watu wa Kichakani walikuwa wenye kudhulumu.
阿拉伯语经注:
فَٱنتَقَمۡنَا مِنۡهُمۡ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٖ مُّبِينٖ
Kwa hivyo tukawaadhibu. Na hakika miji miwili hii iko kwenye njia iliyo wazi.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ كَذَّبَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡحِجۡرِ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na bila ya shaka wakaazi wa Hijr waliwakadhibisha Mitume.
阿拉伯语经注:
وَءَاتَيۡنَٰهُمۡ ءَايَٰتِنَا فَكَانُواْ عَنۡهَا مُعۡرِضِينَ
Na tuliwaletea ishara zetu, nao wakawa wanazipa migongo.
阿拉伯语经注:
وَكَانُواْ يَنۡحِتُونَ مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتًا ءَامِنِينَ
Nao walikuwa wakichonga majumba katika milima kwa amani.
阿拉伯语经注:
فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ مُصۡبِحِينَ
Basi ukelele ukawatwaa asubuhi.
阿拉伯语经注:
فَمَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Na hayakuwafaa yale waliyokuwa wakiyachuma.
阿拉伯语经注:
وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۗ وَإِنَّ ٱلسَّاعَةَ لَأٓتِيَةٞۖ فَٱصۡفَحِ ٱلصَّفۡحَ ٱلۡجَمِيلَ
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake isipokuwa kwa haki. Na hakika Saa ya Qiyama itafika. Basi samehe msamaha mzuri.
阿拉伯语经注:
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡخَلَّٰقُ ٱلۡعَلِيمُ
Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji, Mwenye kujua zaidi.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَٰكَ سَبۡعٗا مِّنَ ٱلۡمَثَانِي وَٱلۡقُرۡءَانَ ٱلۡعَظِيمَ
Na hakika tumekupa saba zinazosomwa mara kwa mara, na Qur-ani Tukufu.
阿拉伯语经注:
لَا تَمُدَّنَّ عَيۡنَيۡكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعۡنَا بِهِۦٓ أَزۡوَٰجٗا مِّنۡهُمۡ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَٱخۡفِضۡ جَنَاحَكَ لِلۡمُؤۡمِنِينَ
Kamwe usivinyoshee macho yako vitu tulivyowastarehesha kwavyo makundi fulani kati yao, wala usiwahuzunikie. Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini.
阿拉伯语经注:
وَقُلۡ إِنِّيٓ أَنَا ٱلنَّذِيرُ ٱلۡمُبِينُ
Na sema, "Hakika mimi ni mwonyaji mwenye kubainisha."
阿拉伯语经注:
كَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَى ٱلۡمُقۡتَسِمِينَ
Kama hivyo tuliwateremshia waliogawa.
阿拉伯语经注:
ٱلَّذِينَ جَعَلُواْ ٱلۡقُرۡءَانَ عِضِينَ
Ambao wakaifanya Qur-ani vipande vipande.
阿拉伯语经注:
فَوَرَبِّكَ لَنَسۡـَٔلَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Basi ninaapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawauliza wote.
阿拉伯语经注:
عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Kuhusu yale waliyokuwa wakiyatenda.
阿拉伯语经注:
فَٱصۡدَعۡ بِمَا تُؤۡمَرُ وَأَعۡرِضۡ عَنِ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Basi wewe yadhihirishe yale uliyoamrishwa, na jitenge na washirikina.
阿拉伯语经注:
إِنَّا كَفَيۡنَٰكَ ٱلۡمُسۡتَهۡزِءِينَ
Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanaofanya stihizai.
阿拉伯语经注:
ٱلَّذِينَ يَجۡعَلُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۚ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ
Ambao wanafanya mungu mwingine kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi, watakuja jua!
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ نَعۡلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدۡرُكَ بِمَا يَقُولُونَ
Na Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo.
阿拉伯语经注:
فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ ٱلسَّٰجِدِينَ
Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni mwa wanaomsujudia.
阿拉伯语经注:
وَٱعۡبُدۡ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأۡتِيَكَ ٱلۡيَقِينُ
Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 哈吉拉
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 - 译解目录

由拉瓦德翻译中心团队与拉布瓦 الدعوة协会和伊斯兰内容服务协会合作翻译。

关闭