Prijevod značenja časnog Kur'ana - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس * - Sadržaj prijevodā


Prijevod značenja Sura: Sura el-Džinn   Ajet:

Surat Al-Jinn

قُلۡ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ ٱسۡتَمَعَ نَفَرٞ مِّنَ ٱلۡجِنِّ فَقَالُوٓاْ إِنَّا سَمِعۡنَا قُرۡءَانًا عَجَبٗا
Sema, ewe Mtume, «Mwenyezi Mungu Ameniletea wahyi kwamba kundi la majini walisikiliza kisomo changu cha Qur’ani, na baada ya kusikia walisema kuwaambia watu wao, «Sisi tumeisikia Qur’ani iliyopambika katika uzuri wa maneno yake, ufasaha wake, hekima zake, hukumuzake na habari inazozielezea,
Tefsiri na arapskom jeziku:
يَهۡدِيٓ إِلَى ٱلرُّشۡدِ فَـَٔامَنَّا بِهِۦۖ وَلَن نُّشۡرِكَ بِرَبِّنَآ أَحَدٗا
inalingania watu kwenye ukweli na uongofu, na sisi tukaiamini na kuifuata kivitendo, na hatutomshirikisha Mola wetu Aliyetuumba na yoyote katika kumuabudu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّهُۥ تَعَٰلَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا ٱتَّخَذَ صَٰحِبَةٗ وَلَا وَلَدٗا
«Na kwamba Yeye Ambaye utukufu Wake uko juu na haiba Yake, Hakumfanya yoyote kuwa mke au mtoto.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّهُۥ كَانَ يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى ٱللَّهِ شَطَطٗا
«Na kwamba fidhuli wet, Iblisi, alikuwa akisema kumsingizia Mwenyezi Mungu aliyetukuka neno lililo mbali na ukweli na usawa, la kudai kuwa Yeye ana mke au mtoto.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّا ظَنَنَّآ أَن لَّن تَقُولَ ٱلۡإِنسُ وَٱلۡجِنُّ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبٗا
«Na kwamba sisi tulidhani kuwa hakuna yoyote atakayemzulia Mwenyezi Mungu Aliyetukuka urongo, si katika binadamu na si katika majini, wa kumnasibishia Yeye mke na mtoto.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّهُۥ كَانَ رِجَالٞ مِّنَ ٱلۡإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٖ مِّنَ ٱلۡجِنِّ فَزَادُوهُمۡ رَهَقٗا
«Na kwamba wanaume miongoni mwa binadamu walikuwa wakijilinda na wanaume miongoni mwa majini, na hawa wanaume wa kijini wakawazidi binadamu kwa kuwa binadamu wanajilinda nao kwa hofu, kicho na kutishika.» Kujilinda huku na asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ambako Mwenyezi Munghu Aliwatangazia watu wa zama za watu wa ujinga, ni katika ushirikina mkubwa ambao Mwenyezi Mungu hausamehe isipokuwa kwa kutubia kidhati kutokana nao. Katika aya hii pana onyo kali juu ya kitendo cha kuwaewndea wachawi, makuhani na mfano wao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّهُمۡ ظَنُّواْ كَمَا ظَنَنتُمۡ أَن لَّن يَبۡعَثَ ٱللَّهُ أَحَدٗا
«Na kwamba makafiri wa kibinadamu walidhania kama mlivyodhania, enyi majini, kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka hatamfufua yoyote baada ya kufa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّا لَمَسۡنَا ٱلسَّمَآءَ فَوَجَدۡنَٰهَا مُلِئَتۡ حَرَسٗا شَدِيدٗا وَشُهُبٗا
«Na kwamba sisi, mkusanyiko wa majini, tulitaka kufika mbinguni,kusikiliza maneno ya watu wake, tukaipata imejazwa Malaika wengi wenye kuilinda na vimondo vya moto ambavyo wanarushiwa wenye kuikaribia.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّا كُنَّا نَقۡعُدُ مِنۡهَا مَقَٰعِدَ لِلسَّمۡعِۖ فَمَن يَسۡتَمِعِ ٱلۡأٓنَ يَجِدۡ لَهُۥ شِهَابٗا رَّصَدٗا
«Na sisi tulikuwa kabla ya hapo tunakalia sehemu fulani za mbingu ili kusikiliza habari zake. Basi mwenye kujaribu sasa kusikiliza kwa kuiba atapata kimondo cha moto chenye kumngojea kimchome na kimuangamize.» Na katika aya mbili hizi pana kubatilisha madai ya wachawi na makuhani wanaodai kuwa wanajua ghaibu na kuwadanganya wachache wa akili kwa urongo wao na uzushi wao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّا لَا نَدۡرِيٓ أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ أَمۡ أَرَادَ بِهِمۡ رَبُّهُمۡ رَشَدٗا
«Na kwamba sisi, mkusanyiko wa majini, hatujui: ni mabaya ambayo Mwenyezi Mungu Anataka kuwateremshia watu wa ardhini au Anawatakia mazuri na uongofu?
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّا مِنَّا ٱلصَّٰلِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَۖ كُنَّا طَرَآئِقَ قِدَدٗا
«Na kwamba sisi, miongoni mwetu kuna wema wachamungu na miongoni mwetu kuna watu ambao wako chini ya hapo: wao ni makafiri na wenye kuasi. Sisi tuko mapote na mila tofauti.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّا ظَنَنَّآ أَن لَّن نُّعۡجِزَ ٱللَّهَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَن نُّعۡجِزَهُۥ هَرَبٗا
«Na kwamba sisi tuna yakini kuwa mwenyezi Mungu Ana uweza juu yetu, na sisi tuko kwenye mkamato Wake na mamlaka Yake; hatuwezi kumponyoka Anapotaka kutufanya jambo popote pale tulipo. Na hatutaweza kuyahepa mateso Yake kwa kukimbila kwenda mbinguni iwapo Anatutakia mabaya.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّا لَمَّا سَمِعۡنَا ٱلۡهُدَىٰٓ ءَامَنَّا بِهِۦۖ فَمَن يُؤۡمِنۢ بِرَبِّهِۦ فَلَا يَخَافُ بَخۡسٗا وَلَا رَهَقٗا
«Na sisi tulipoisikia Qur’ani tuliiamini na tukakubali kuwa ni ukweli unaotoka kwa Mwenyezi Mungu. Basi mwenye kumuamini Mola wake, kwa hakika yeye hataogopa kupunguziwa mema yake wala kudhulumiwa kwa kuongezewa makosa yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّا مِنَّا ٱلۡمُسۡلِمُونَ وَمِنَّا ٱلۡقَٰسِطُونَۖ فَمَنۡ أَسۡلَمَ فَأُوْلَٰٓئِكَ تَحَرَّوۡاْ رَشَدٗا
«Na kwamba miongoni mwetu kuna wenye kumnyenyekea Mwenyezi Mungu kwa kumtii, na miongoni mwetu kuna waliopotoka walio madhalimu ambao walienda kombo na njia ya haki. Basi mwenye kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea kwa utiifu, hao ndio walioelekea njia ya haki na usawa, wakajibidiisha kuichagua na Mwenyezi Mungu Akawaongoza kuifikia.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَمَّا ٱلۡقَٰسِطُونَ فَكَانُواْ لِجَهَنَّمَ حَطَبٗا
Ama wale waliopotoka na njia ya Uislamu, watakuwa ni kuni za Moto wa Jahanamu.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَلَّوِ ٱسۡتَقَٰمُواْ عَلَى ٱلطَّرِيقَةِ لَأَسۡقَيۡنَٰهُم مَّآءً غَدَقٗا
Na lau makafiri wa kibinadamu na kijini wangalifuata njia ya Uislamu na wasijiepushe nayo, tungaliwateremshia maji mengi na tungaliwakunjulia riziki duniani,
Tefsiri na arapskom jeziku:
لِّنَفۡتِنَهُمۡ فِيهِۚ وَمَن يُعۡرِضۡ عَن ذِكۡرِ رَبِّهِۦ يَسۡلُكۡهُ عَذَابٗا صَعَدٗا
ili tuwafanyie mtihani: vipi watazishukuru neema za Mwenyezi Mungu juu yao? Na yoyote mwenye kupa mgongo utiifu wa Mwenyezi Mungu na kusikiliza Qur’ani na kuizingatia na kuifuata kivitendo, Mwenyezi Mungu Atamuingiza kwenye adhabu kali iliyo ngumu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّ ٱلۡمَسَٰجِدَ لِلَّهِ فَلَا تَدۡعُواْ مَعَ ٱللَّهِ أَحَدٗا
Na kwa hakika misikiti ni ya kuabudiwa Mwenyezi Mungu Peke Yake, basi msiabudu humo asiyekuwa Yeye. Na mtakasieni maombi na ibada humo, kwani misikiti haikujengwa isipokuwa kwa ajili Mwenyezi Mungu Aabudiwe humo Peke Yake, na sio mwingine asiyekuwa Yeye. Katika haya kuna ulazima wa kuiepusha misikiti na kila kinachokoroga utakasaji wa Mwenyezi Mungu na ufuataji Mtume Wake, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَنَّهُۥ لَمَّا قَامَ عَبۡدُ ٱللَّهِ يَدۡعُوهُ كَادُواْ يَكُونُونَ عَلَيۡهِ لِبَدٗا
Na kwa hakika Aliposimama Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kumuabudu Mola wake, walikaribia majini kumwangukia wakiwa makundi yaliyojikusanya na kupandana kwa kusongamana sana ili wapate kuisikia Qur’ani kutoka kwake
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ إِنَّمَآ أَدۡعُواْ رَبِّي وَلَآ أُشۡرِكُ بِهِۦٓ أَحَدٗا
Waambie, ewe Mtume, hawa makafiri, «Kwa hakika mimi ninamuabudu Mola wangu Peke Yake, wala simshirikishi na Yeye kitu chochote katika kuabudu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ إِنِّي لَآ أَمۡلِكُ لَكُمۡ ضَرّٗا وَلَا رَشَدٗا
Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa makafiri, «Mimi siwezi kuwaondolea shida yoyote wala kuwaletea manufaa yoyote.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ ٱللَّهِ أَحَدٞ وَلَنۡ أَجِدَ مِن دُونِهِۦ مُلۡتَحَدًا
Sema, «Hakika mimi sina yoyote wa kuniokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu iwapo nitamuasi, na sitapata asiyekuwa Yeye mahali pa kukimbilia niepukane na adhabu Yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
إِلَّا بَلَٰغٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَرِسَٰلَٰتِهِۦۚ وَمَن يَعۡصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَإِنَّ لَهُۥ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا
Ninachokiweza mimi na kukimiliki ni kuwafikishia kutoka kwa Mwenyezi Mungu kile Alichoniamrisha niwafikishie na ujumbe Wake ambao Alinituma niwaletee. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na akaipa mgongo Dini ya Mwenyezi Mungu, basi malipo yake ni moto wa Jahanamu ambao hatatoka humo milele.
Tefsiri na arapskom jeziku:
حَتَّىٰٓ إِذَا رَأَوۡاْ مَا يُوعَدُونَ فَسَيَعۡلَمُونَ مَنۡ أَضۡعَفُ نَاصِرٗا وَأَقَلُّ عَدَدٗا
Mpaka watakapoishuhudia washirikina adhabu anayoahidiwa, hapo watajua itakapowashukia wao: ni nani ambaye mtetezi wake na msaidizi ni mnyonge zaidi na ambaye askari wake ni wachache zaid?
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ إِنۡ أَدۡرِيٓ أَقَرِيبٞ مَّا تُوعَدُونَ أَمۡ يَجۡعَلُ لَهُۥ رَبِّيٓ أَمَدًا
Waambie hawa washirikina, ewe Mtume, Mimi sijui: Je adhabu hii mliyoahidiwa zishakaribia zama zake au Mola wangu ataufanya muda wake wa kuja uwe mrefu?
Tefsiri na arapskom jeziku:
عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ فَلَا يُظۡهِرُ عَلَىٰ غَيۡبِهِۦٓ أَحَدًا
Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ni mjuzi wa kisichoonekana na macho. Hatakitoa wazi hiko kisichoonekana kwa yoyote miongoni mwa viumbe Wake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
إِلَّا مَنِ ٱرۡتَضَىٰ مِن رَّسُولٖ فَإِنَّهُۥ يَسۡلُكُ مِنۢ بَيۡنِ يَدَيۡهِ وَمِنۡ خَلۡفِهِۦ رَصَدٗا
Isipokuwa kwa yule Aliyemchagua Mwenyezi Mungu na kumpendelea kwa kumpa utume, kwani Yeye huwajuza baadhi ya yale yaliyofichika yasionekane. Na Anatuma, mbele ya huyo Mtume na nyuma yake, Malaika wenye kumhifadhi na majini, ili wasiisikilize kwa kuiba jambo hilo la ghaibu, kisha wakaambiana kwa siri kisha wakawadokeza makuhani.
Tefsiri na arapskom jeziku:
لِّيَعۡلَمَ أَن قَدۡ أَبۡلَغُواْ رِسَٰلَٰتِ رَبِّهِمۡ وَأَحَاطَ بِمَا لَدَيۡهِمۡ وَأَحۡصَىٰ كُلَّ شَيۡءٍ عَدَدَۢا
Ili Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ajue kwamba Mitume kabla yake walikuwa kwenye hali kama yake ya ufikishaji haki na ukweli, na kwamba yeye atalindwa kutokana na majini kama walivyolindwa wao, na kwamba Mwenyezi Mungu, ujuzi Wake umeyazunguka mambo yao waliyonayo ya nje na ya ndani, miongoni mwa sheria na hukumu na mengineyo, hakuna chochote kinachompita katika hayo, na kwamba Yeye Amekidhibiti kila kitu kwa hesabu, hakuna chochote kinachofichamana Kwake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
 
Prijevod značenja Sura: Sura el-Džinn
Indeks sura Broj stranice
 
Prijevod značenja časnog Kur'ana - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس - Sadržaj prijevodā

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها الدكتور عبد الله محمد أبو بكر والشيخ ناصر خميس.

Zatvaranje