prev

Al-Jinn

next

1 : 72

قُلۡ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ ٱسۡتَمَعَ نَفَرٞ مِّنَ ٱلۡجِنِّ فَقَالُوٓاْ إِنَّا سَمِعۡنَا قُرۡءَانًا عَجَبٗا

Sema, (ewe Mtume), Allah Mtukufu Ameniletea wahyi kwamba kundi la majini walisikiliza kisomo changu cha Qur’ani, na baada ya kusikia walisema kuwaambia watu wao, «Sisi tumeisikia Qur’ani iliyopambika katika uzuri wa maneno yake, ufasaha wake, hekima zake, hukumu zake na habari inazozielezea». info
التفاسير: |

2 : 72

يَهۡدِيٓ إِلَى ٱلرُّشۡدِ فَـَٔامَنَّا بِهِۦۖ وَلَن نُّشۡرِكَ بِرَبِّنَآ أَحَدٗا

Inalingania watu kwenye ukweli na uongofu, na sisi tukaiamini na kuifuata kivitendo, na hatutomshirikisha Mola wetu Aliyetuumba na yoyote katika kumuabudu. info
التفاسير: |

3 : 72

وَأَنَّهُۥ تَعَٰلَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا ٱتَّخَذَ صَٰحِبَةٗ وَلَا وَلَدٗا

Na kwamba Yeye Ambaye utukufu Wake uko juu pamoja na haiba Yake, Hakumfanya yoyote kuwa mke au mtoto. info
التفاسير: |

4 : 72

وَأَنَّهُۥ كَانَ يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى ٱللَّهِ شَطَطٗا

Na kwamba fedhuli wetu, Iblisi, alikuwa akisema kumsingizia Allah Mtukufu aliyetukuka neno lililo mbali na ukweli na usawa, la kudai kuwa Yeye ana mke au mtoto. info
التفاسير: |

5 : 72

وَأَنَّا ظَنَنَّآ أَن لَّن تَقُولَ ٱلۡإِنسُ وَٱلۡجِنُّ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبٗا

Na kwamba sisi tulidhani kuwa hakuna yoyote atakayemzulia Allah Mtukufu Aliyetukuka urongo, si katika binadamu na si katika majini, wa kumnasibishia Yeye mke na mtoto. info
التفاسير: |

6 : 72

وَأَنَّهُۥ كَانَ رِجَالٞ مِّنَ ٱلۡإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٖ مِّنَ ٱلۡجِنِّ فَزَادُوهُمۡ رَهَقٗا

Na kwamba wanaume miongoni mwa binadamu walikuwa wakijilinda na wanaume miongoni mwa majini, na hawa wanaume wa kijini hawakua isipokua wakiwazidishia binadamu hofu, na kutishika. Kujilinda huku na asiyekuwa Allah Mtukufu, ambako Allah Mtukufu aliwakataza watu wa zama za ujinga, ni katika ushirikina mkubwa ambao Allah Mtukufu hausamehe isipokuwa kwa kutubia kidhati kutokana nao. Katika aya hii pana onyo kali juu ya kitendo cha kuwaendea wachawi, makuhani na mfano wao. info
التفاسير: |

7 : 72

وَأَنَّهُمۡ ظَنُّواْ كَمَا ظَنَنتُمۡ أَن لَّن يَبۡعَثَ ٱللَّهُ أَحَدٗا

Na kwamba makafiri wa kibinadamu walidhania kama mlivyodhania, (enyi majini), kuwa Allah Mtukufu Aliyetukuka hatamfufua yoyote baada ya kufa. info
التفاسير: |

8 : 72

وَأَنَّا لَمَسۡنَا ٱلسَّمَآءَ فَوَجَدۡنَٰهَا مُلِئَتۡ حَرَسٗا شَدِيدٗا وَشُهُبٗا

Na kwamba sisi, mkusanyiko wa majini, tulitaka kufika mbinguni, kusikiliza maneno ya watu wake, tukaikuta imejazwa Malaika wengi wenye kuilinda na vimondo vya moto ambavyo wanarushiwa wenye kuikaribia. info
التفاسير: |

9 : 72

وَأَنَّا كُنَّا نَقۡعُدُ مِنۡهَا مَقَٰعِدَ لِلسَّمۡعِۖ فَمَن يَسۡتَمِعِ ٱلۡأٓنَ يَجِدۡ لَهُۥ شِهَابٗا رَّصَدٗا

Na sisi tulikuwa kabla ya hapo tunakalia sehemu fulani za mbingu ili kusikiliza habari zake. Basi mwenye kujaribu sasa kusikiliza kwa kuiba atapata kimondo cha moto chenye kumngojea kimchome na kimuangamize. Na katika aya mbili hizi pana kubatilisha madai ya wachawi na makuhani wanaodai kuwa wanajua ghaibu na kuwadanganya wachache wa akili kwa urongo wao na uzushi wao. info
التفاسير: |

10 : 72

وَأَنَّا لَا نَدۡرِيٓ أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ أَمۡ أَرَادَ بِهِمۡ رَبُّهُمۡ رَشَدٗا

Na kwamba sisi, mkusanyiko wa majini, hatujui: ni mabaya Allah Mtukufu Anataka kuwateremshia watu wa ardhini au Anawatakia mazuri na uongofu? info
التفاسير: |

11 : 72

وَأَنَّا مِنَّا ٱلصَّٰلِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَۖ كُنَّا طَرَآئِقَ قِدَدٗا

Na kwamba sisi, miongoni mwetu kuna wema wachamungu na miongoni mwetu kuna watu ambao wako chini ya hapo: wao ni makafiri na wenye kuasi. Sisi tuko mapote na mila tofauti. info
التفاسير: |

12 : 72

وَأَنَّا ظَنَنَّآ أَن لَّن نُّعۡجِزَ ٱللَّهَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَن نُّعۡجِزَهُۥ هَرَبٗا

Na kwamba sisi tuna yakini kuwa Allah Mtukufu Ana uwezo juu yetu, na sisi tuko kwenye mkamato Wake na mamlaka Yake; hatuwezi kumponyoka Anapotaka kutufanya jambo lolote popote pale tulipo. Na hatutaweza kuyakwepa mateso Yake kwa kukimbilia kwenda mbinguni iwapo atatutakia mabaya. info
التفاسير: |

13 : 72

وَأَنَّا لَمَّا سَمِعۡنَا ٱلۡهُدَىٰٓ ءَامَنَّا بِهِۦۖ فَمَن يُؤۡمِنۢ بِرَبِّهِۦ فَلَا يَخَافُ بَخۡسٗا وَلَا رَهَقٗا

Na sisi tulipoisikia Qur’ani tuliiamini na tukakubali kuwa ni ukweli unaotoka kwa Allah Mtukufu. Basi mwenye kumuamini Mola wake, kwa hakika yeye hataogopa kupunguziwa mema yake wala kudhulumiwa kwa kuongezewa makosa yake. info
التفاسير: |
prev

Al-Jinn

next
:
0:00 0:00