Check out the new design

Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad * - Sadržaj prijevodā


Prijevod značenja Sura: El-Isra   Ajet:
وَبِٱلۡحَقِّ أَنزَلۡنَٰهُ وَبِٱلۡحَقِّ نَزَلَۗ وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا مُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا
Na kwa Haki tumeiteremsha, na kwa Haki imeteremka. Na hatukukutuma isipokuwa uwe mbashiri na mwonyaji.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَقُرۡءَانٗا فَرَقۡنَٰهُ لِتَقۡرَأَهُۥ عَلَى ٱلنَّاسِ عَلَىٰ مُكۡثٖ وَنَزَّلۡنَٰهُ تَنزِيلٗا
Na Qur-ani tumeigawanya sehemu mbalimbali ili uwasomee watu kwa kituo, na tumeiteremsha kidogo kidogo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ ءَامِنُواْ بِهِۦٓ أَوۡ لَا تُؤۡمِنُوٓاْۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ مِن قَبۡلِهِۦٓ إِذَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ يَخِرُّونَۤ لِلۡأَذۡقَانِۤ سُجَّدٗاۤ
Sema, "Iaminini au msiiamini. Hakika wale waliopewa elimu kabla yake, wanaposomewa hii, huanguka kifudifudi wanasujudu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَيَقُولُونَ سُبۡحَٰنَ رَبِّنَآ إِن كَانَ وَعۡدُ رَبِّنَا لَمَفۡعُولٗا
"Na wanasema, 'Subhana Rabbina (Ametakasika Mola wetu Mlezi)! Hakika ahadi ya Mola wetu Mlezi lazima itimizwe!'
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَيَخِرُّونَ لِلۡأَذۡقَانِ يَبۡكُونَ وَيَزِيدُهُمۡ خُشُوعٗا۩
"Na huanguka kifudifudi na huku wanalia, na inawazidisha unyenyekevu."
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلِ ٱدۡعُواْ ٱللَّهَ أَوِ ٱدۡعُواْ ٱلرَّحۡمَٰنَۖ أَيّٗا مَّا تَدۡعُواْ فَلَهُ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَلَا تَجۡهَرۡ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتۡ بِهَا وَٱبۡتَغِ بَيۡنَ ذَٰلِكَ سَبِيلٗا
Sema, "Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Ar-Rahman (Mwingi wa rehema), kwa jina lolote mnalomwita. Hakika, Yeye ana majina mazuri zaidi. Wala usiswali Swala yako kwa sauti kubwa sana, wala usiifiche kwa sauti ndogo sana, bali shika njia ya kati na kati ya hizo."
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَقُلِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي لَمۡ يَتَّخِذۡ وَلَدٗا وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ شَرِيكٞ فِي ٱلۡمُلۡكِ وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ وَلِيّٞ مِّنَ ٱلذُّلِّۖ وَكَبِّرۡهُ تَكۡبِيرَۢا
Na sema, "Alhamdulillah (sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu) ambaye hakujifanyia mwana yeyote, wala hana mshirika yeyote katika ufalme, wala hana mlinzi yeyote wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
 
Prijevod značenja Sura: El-Isra
Indeks sura Broj stranice
 
Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad - Sadržaj prijevodā

Prevod: Prevodilački centar Ruvvad u saradnji sa Udruženjem za poziv u Rabwi i Udruženjem za pružanje islamskog sadržaja na jezicima.

Zatvaranje