Check out the new design

Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad * - Sadržaj prijevodā


Prijevod značenja Sura: El-Isra   Ajet:
إِلَّا رَحۡمَةٗ مِّن رَّبِّكَۚ إِنَّ فَضۡلَهُۥ كَانَ عَلَيۡكَ كَبِيرٗا
Isipokuwa iwe rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika fadhila yake kwako ni kubwa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُل لَّئِنِ ٱجۡتَمَعَتِ ٱلۡإِنسُ وَٱلۡجِنُّ عَلَىٰٓ أَن يَأۡتُواْ بِمِثۡلِ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ لَا يَأۡتُونَ بِمِثۡلِهِۦ وَلَوۡ كَانَ بَعۡضُهُمۡ لِبَعۡضٖ ظَهِيرٗا
Sema: Wangelikusanyika watu na majini ili walete mfano wa Qur-ani hii, basi hawawezi kuleta mfano wake, hata kama wakisaidiana wao kwa wao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَقَدۡ صَرَّفۡنَا لِلنَّاسِ فِي هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ مِن كُلِّ مَثَلٖ فَأَبَىٰٓ أَكۡثَرُ ٱلنَّاسِ إِلَّا كُفُورٗا
Na hakika tumewaeleza watu katika Qur-ani hii kwa kila mfano. Lakini wengi wa watu wakakataa isipokuwa kukufuru tu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَقَالُواْ لَن نُّؤۡمِنَ لَكَ حَتَّىٰ تَفۡجُرَ لَنَا مِنَ ٱلۡأَرۡضِ يَنۢبُوعًا
Na walisema, "Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchemi katika ardhi hii."
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَوۡ تَكُونَ لَكَ جَنَّةٞ مِّن نَّخِيلٖ وَعِنَبٖ فَتُفَجِّرَ ٱلۡأَنۡهَٰرَ خِلَٰلَهَا تَفۡجِيرًا
Au uwe na bustani ya mitende na mizabibu, na utupitishie mito kati yake ikimiminika.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَوۡ تُسۡقِطَ ٱلسَّمَآءَ كَمَا زَعَمۡتَ عَلَيۡنَا كِسَفًا أَوۡ تَأۡتِيَ بِٱللَّهِ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ قَبِيلًا
Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyodai, au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika uso kwa uso.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَوۡ يَكُونَ لَكَ بَيۡتٞ مِّن زُخۡرُفٍ أَوۡ تَرۡقَىٰ فِي ٱلسَّمَآءِ وَلَن نُّؤۡمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيۡنَا كِتَٰبٗا نَّقۡرَؤُهُۥۗ قُلۡ سُبۡحَانَ رَبِّي هَلۡ كُنتُ إِلَّا بَشَرٗا رَّسُولٗا
Au uwe na nyumba iliyopambwa, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako huko mpaka ututeremshie kitabu tukisome. Sema, "Subhana Rabbi (Ametakasika Mola wangu Mlezi)! Kwani mimi ni nani isipokuwa ni mtu tu na Mtume?
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَمَا مَنَعَ ٱلنَّاسَ أَن يُؤۡمِنُوٓاْ إِذۡ جَآءَهُمُ ٱلۡهُدَىٰٓ إِلَّآ أَن قَالُوٓاْ أَبَعَثَ ٱللَّهُ بَشَرٗا رَّسُولٗا
Na hakikuwazuilia watu kuamini ulipowajia uwongofu isipokuwa ni kwamba walisema, "Je, mwenyezi Mungu alimtuma mtu kuwa ni Mtume?"
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُل لَّوۡ كَانَ فِي ٱلۡأَرۡضِ مَلَٰٓئِكَةٞ يَمۡشُونَ مُطۡمَئِنِّينَ لَنَزَّلۡنَا عَلَيۡهِم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ مَلَكٗا رَّسُولٗا
Sema, "Ingelikuwa katika ardhi wapo Malaika wanatembea kwa utulivu wao, basi bila ya shaka tungeliwateremshia Malaika kuwa ni Mtume wao."
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ كَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدَۢا بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡۚ إِنَّهُۥ كَانَ بِعِبَادِهِۦ خَبِيرَۢا بَصِيرٗا
Sema, "Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi baina yangu na nyinyi. Hakika Yeye ana habari zote za waja wake na anawaona vyema."
Tefsiri na arapskom jeziku:
 
Prijevod značenja Sura: El-Isra
Indeks sura Broj stranice
 
Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad - Sadržaj prijevodā

Prevod: Prevodilački centar Ruvvad u saradnji sa Udruženjem za poziv u Rabwi i Udruženjem za pružanje islamskog sadržaja na jezicima.

Zatvaranje