Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 * - 译解目录


含义的翻译 章: 伊斯拉仪   段:
إِلَّا رَحۡمَةٗ مِّن رَّبِّكَۚ إِنَّ فَضۡلَهُۥ كَانَ عَلَيۡكَ كَبِيرٗا
Isipokuwa iwe rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika fadhila yake kwako ni kubwa.
阿拉伯语经注:
قُل لَّئِنِ ٱجۡتَمَعَتِ ٱلۡإِنسُ وَٱلۡجِنُّ عَلَىٰٓ أَن يَأۡتُواْ بِمِثۡلِ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ لَا يَأۡتُونَ بِمِثۡلِهِۦ وَلَوۡ كَانَ بَعۡضُهُمۡ لِبَعۡضٖ ظَهِيرٗا
Sema: Wangelikusanyika watu na majini ili walete mfano wa Qur-ani hii, basi hawawezi kuleta mfano wake, hata kama watasaidiana wao kwa wao.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ صَرَّفۡنَا لِلنَّاسِ فِي هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ مِن كُلِّ مَثَلٖ فَأَبَىٰٓ أَكۡثَرُ ٱلنَّاسِ إِلَّا كُفُورٗا
Na hakika tumewaeleza watu katika Qur-ani hii kwa kila mfano. Lakini wengi wa watu wakakataa isipokuwa kukufuru tu.
阿拉伯语经注:
وَقَالُواْ لَن نُّؤۡمِنَ لَكَ حَتَّىٰ تَفۡجُرَ لَنَا مِنَ ٱلۡأَرۡضِ يَنۢبُوعًا
Na walisema, "Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemichemi katika ardhi hii.
阿拉伯语经注:
أَوۡ تَكُونَ لَكَ جَنَّةٞ مِّن نَّخِيلٖ وَعِنَبٖ فَتُفَجِّرَ ٱلۡأَنۡهَٰرَ خِلَٰلَهَا تَفۡجِيرًا
Au uwe na bustani ya mitende na mizabibu, na utupitishie mito kati yake ikimiminika.
阿拉伯语经注:
أَوۡ تُسۡقِطَ ٱلسَّمَآءَ كَمَا زَعَمۡتَ عَلَيۡنَا كِسَفًا أَوۡ تَأۡتِيَ بِٱللَّهِ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ قَبِيلًا
Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyodai, au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika uso kwa uso.
阿拉伯语经注:
أَوۡ يَكُونَ لَكَ بَيۡتٞ مِّن زُخۡرُفٍ أَوۡ تَرۡقَىٰ فِي ٱلسَّمَآءِ وَلَن نُّؤۡمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيۡنَا كِتَٰبٗا نَّقۡرَؤُهُۥۗ قُلۡ سُبۡحَانَ رَبِّي هَلۡ كُنتُ إِلَّا بَشَرٗا رَّسُولٗا
Au uwe na nyumba iliyopambwa, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako huko mpaka ututeremshie kitabu tukisome. Sema, "Subhana Rabbi (Ametakasika Mola wangu Mlezi)! Kwani mimi ni nani isipokuwa ni mtu tu na Mtume?
阿拉伯语经注:
وَمَا مَنَعَ ٱلنَّاسَ أَن يُؤۡمِنُوٓاْ إِذۡ جَآءَهُمُ ٱلۡهُدَىٰٓ إِلَّآ أَن قَالُوٓاْ أَبَعَثَ ٱللَّهُ بَشَرٗا رَّسُولٗا
Na hakikuwazuilia watu kuamini ulipowajia uongofu isipokuwa ni kwamba walisema, "Je, mwenyezi Mungu alimtuma mtu kuwa ni Mtume?"
阿拉伯语经注:
قُل لَّوۡ كَانَ فِي ٱلۡأَرۡضِ مَلَٰٓئِكَةٞ يَمۡشُونَ مُطۡمَئِنِّينَ لَنَزَّلۡنَا عَلَيۡهِم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ مَلَكٗا رَّسُولٗا
Sema, "Ingelikuwa katika ardhi wapo Malaika wanatembea kwa utulivu wao, basi bila ya shaka tungeliwateremshia Malaika kuwa ni Mtume wao."
阿拉伯语经注:
قُلۡ كَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدَۢا بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡۚ إِنَّهُۥ كَانَ بِعِبَادِهِۦ خَبِيرَۢا بَصِيرٗا
Sema, "Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi baina yangu na nyinyi. Hakika Yeye ana habari zote za waja wake na anawaona vyema."
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 伊斯拉仪
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 - 译解目录

由拉瓦德翻译中心团队与拉布瓦 الدعوة协会和伊斯兰内容服务协会合作翻译。

关闭