Check out the new design

Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad * - Sadržaj prijevodā


Prijevod značenja Sura: El-En'am   Ajet:
فَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل رَّبُّكُمۡ ذُو رَحۡمَةٖ وَٰسِعَةٖ وَلَا يُرَدُّ بَأۡسُهُۥ عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ
Na wakikukadhibisha, basi wewe sema: Mola wenu Mlezi ni Mwenye rehema iliyoenea. Wala haizuiwi adhabu yake kwa kaumu wahalifu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
سَيَقُولُ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ لَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَآ أَشۡرَكۡنَا وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمۡنَا مِن شَيۡءٖۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ حَتَّىٰ ذَاقُواْ بَأۡسَنَاۗ قُلۡ هَلۡ عِندَكُم مِّنۡ عِلۡمٖ فَتُخۡرِجُوهُ لَنَآۖ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا تَخۡرُصُونَ
Watasema wale walioshirikisha, "Lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, tusingelishirikisha, wala baba zetu, wala tusingeliharamisha kitu chochote." Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale waliokuwa kabla yao mpaka walipoionja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo elimu yoyote mtutolee hiyo? Nyinyi hamfuati isipokuwa dhana. Wala hamfanyi isipokuwa kukisia tu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ فَلِلَّهِ ٱلۡحُجَّةُ ٱلۡبَٰلِغَةُۖ فَلَوۡ شَآءَ لَهَدَىٰكُمۡ أَجۡمَعِينَ
Sema: Basi Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye hoja ya kukata. Na kama angelitaka, angeliwaongoa nyote.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ هَلُمَّ شُهَدَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ يَشۡهَدُونَ أَنَّ ٱللَّهَ حَرَّمَ هَٰذَاۖ فَإِن شَهِدُواْ فَلَا تَشۡهَدۡ مَعَهُمۡۚ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ وَهُم بِرَبِّهِمۡ يَعۡدِلُونَ
Sema: Waleteni mashahidi wenu ambao wanashuhudia kuwa Mwenyezi Mungu amewaharamisha hawa. Kwa hivyo, wakishuhudia, basi wewe usishuhudie pamoja nao. Wala usifuate matamanio ya wale waliozikadhibisha Ishara zetu, na ambao hawaamini katika Akhera, nao wanamlinganisha Mola wao Mlezi na wengine.
Tefsiri na arapskom jeziku:
۞ قُلۡ تَعَالَوۡاْ أَتۡلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمۡ عَلَيۡكُمۡۖ أَلَّا تُشۡرِكُواْ بِهِۦ شَيۡـٔٗاۖ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنٗاۖ وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَوۡلَٰدَكُم مِّنۡ إِمۡلَٰقٖ نَّحۡنُ نَرۡزُقُكُمۡ وَإِيَّاهُمۡۖ وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلۡفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنۡهَا وَمَا بَطَنَۖ وَلَا تَقۡتُلُواْ ٱلنَّفۡسَ ٱلَّتِي حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ
Sema: Njooni niwasomee yale aliyowaharimishia Mola wenu Mlezi. Kwamba msimshirikishe Yeye na chochote, na wazazi wawili wafanyieni uzuri, wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunawaruzuku nyinyi na wao. Wala msikaribie machafu, yaliyo dhahiri yake, na yaliyofichikana yake. Wala msiiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu aliiharimisha isipokuwa kwa haki. Hayo aliwausia ili myatie akilini.
Tefsiri na arapskom jeziku:
 
Prijevod značenja Sura: El-En'am
Indeks sura Broj stranice
 
Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad - Sadržaj prijevodā

Prevod: Prevodilački centar Ruvvad u saradnji sa Udruženjem za poziv u Rabwi i Udruženjem za pružanje islamskog sadržaja na jezicima.

Zatvaranje