Check out the new design

Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad * - Sadržaj prijevodā


Prijevod značenja Sura: El-En'am   Ajet:
هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأۡتِيَهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ أَوۡ يَأۡتِيَ رَبُّكَ أَوۡ يَأۡتِيَ بَعۡضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَۗ يَوۡمَ يَأۡتِي بَعۡضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفۡسًا إِيمَٰنُهَا لَمۡ تَكُنۡ ءَامَنَتۡ مِن قَبۡلُ أَوۡ كَسَبَتۡ فِيٓ إِيمَٰنِهَا خَيۡرٗاۗ قُلِ ٱنتَظِرُوٓاْ إِنَّا مُنتَظِرُونَ
Je, wanangoja isipokuwa kwamba wajiwe na Malaika, au awajie Mola wako Mlezi, au ziwajie baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapowajia baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini kwa nafsi hapo hakutaifaa kitu, ikiwa haikuwa imeamini kabla yake, au imefanya heri katika Imani yake. Sema, "Ngojeni, nasi hakika pia ni wenye kungoja."
Tefsiri na arapskom jeziku:
إِنَّ ٱلَّذِينَ فَرَّقُواْ دِينَهُمۡ وَكَانُواْ شِيَعٗا لَّسۡتَ مِنۡهُمۡ فِي شَيۡءٍۚ إِنَّمَآ أَمۡرُهُمۡ إِلَى ٱللَّهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ
Hakika wale waliofarakisha Dini yao na wakawa makundi makundi, wewe si miongoni mwao katika chochote. Bila ya shaka jambo lao liko kwa Mwenyezi Mungu; kisha atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda.
Tefsiri na arapskom jeziku:
مَن جَآءَ بِٱلۡحَسَنَةِ فَلَهُۥ عَشۡرُ أَمۡثَالِهَاۖ وَمَن جَآءَ بِٱلسَّيِّئَةِ فَلَا يُجۡزَىٰٓ إِلَّا مِثۡلَهَا وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ
Mwenye kuja na jema, basi ana mara kumi mfano wake. Na mwenye kuja na baya, basi hatalipwa isipokuwa mfano wake. Na wao hawatadhulumiwa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ إِنَّنِي هَدَىٰنِي رَبِّيٓ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ دِينٗا قِيَمٗا مِّلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۚ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Sema: Hakika mimi, Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye njia iliyonyooka, dini iliyo sawa kabisa, mila ya Ibrahim aliyekuwa mnyoofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحۡيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Sema: Hakika Swala yangu, na kuchinja kwangu , na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu."
Tefsiri na arapskom jeziku:
لَا شَرِيكَ لَهُۥۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرۡتُ وَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ
Hana mshirika yeyote. Na hayo ndiyo niliyoamrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَبۡغِي رَبّٗا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيۡءٖۚ وَلَا تَكۡسِبُ كُلُّ نَفۡسٍ إِلَّا عَلَيۡهَاۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرۡجِعُكُمۡ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ
Sema: Je nimtafute Mola Mlezi asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ilhali Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu? Na wala haichumi kila nafsi isipokuwa ni juu yake. Na wala hatabeba mbeba mzigo, mzigo wa mwingine. Kisha kwa Mola wenu Mlezi ndiyo marejeo yenu, kisha atawajulisha yale mliyokuwa mkihitalifiana ndani yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَكُمۡ خَلَٰٓئِفَ ٱلۡأَرۡضِ وَرَفَعَ بَعۡضَكُمۡ فَوۡقَ بَعۡضٖ دَرَجَٰتٖ لِّيَبۡلُوَكُمۡ فِي مَآ ءَاتَىٰكُمۡۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورٞ رَّحِيمُۢ
Naye ndiye aliyewafanya kuwa mahalifa katika dunia, na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja mbalimbali ili awajaribu katika hayo aliyowapa. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kufuta dhambi zaidi, Mwenye kurehemu sana.
Tefsiri na arapskom jeziku:
 
Prijevod značenja Sura: El-En'am
Indeks sura Broj stranice
 
Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad - Sadržaj prijevodā

Prevod: Prevodilački centar Ruvvad u saradnji sa Udruženjem za poziv u Rabwi i Udruženjem za pružanje islamskog sadržaja na jezicima.

Zatvaranje