Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al idioma swahili- Abdullah Mohamad y Naser Jamis * - Índice de traducciones


Traducción de significados Capítulo: Sura Al-Mumtahana   Versículo:

Surat Al-Mumtahanah

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمۡ أَوۡلِيَآءَ تُلۡقُونَ إِلَيۡهِم بِٱلۡمَوَدَّةِ وَقَدۡ كَفَرُواْ بِمَا جَآءَكُم مِّنَ ٱلۡحَقِّ يُخۡرِجُونَ ٱلرَّسُولَ وَإِيَّاكُمۡ أَن تُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ رَبِّكُمۡ إِن كُنتُمۡ خَرَجۡتُمۡ جِهَٰدٗا فِي سَبِيلِي وَٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِيۚ تُسِرُّونَ إِلَيۡهِم بِٱلۡمَوَدَّةِ وَأَنَا۠ أَعۡلَمُ بِمَآ أَخۡفَيۡتُمۡ وَمَآ أَعۡلَنتُمۡۚ وَمَن يَفۡعَلۡهُ مِنكُمۡ فَقَدۡ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo! Msiwachukue maadui wangu na maadui wenu mkawafanya ni marafiki halisi na vipenzi, mkawa mnaamiliana na wao kwa upendo na mkawapasha habari za Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Waislamu wengine, na hali wao wameikanusha haki iliyowajia ya kumuamini Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Qur’ani iliyoteremshwa kwake. Wanamtoa Mtume na wanawatoa nyinyi, enyi Waumini, kutoka Makkah kwa kuwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu Mola wenu na mnampwekesha. Mkiwa nyinyi, enyi Waumini, mmehama kwa kupigana jihadi katika njia yangu kwa kutafuta radhi yangu kwenu, basi msifanye urafiki na maadui wangu na maadui wenu. Mnawaambia wao kwa siri kuwa mnawapenda, na mimi ninayajua mnayoyaficha na mnayoyadhihirisha. Na yoyote anayefanya hivyo miongoni mwenu, ashakosea njia ya haki na sawa na amepotea njia ya wastani.
Las Exégesis Árabes:
إِن يَثۡقَفُوكُمۡ يَكُونُواْ لَكُمۡ أَعۡدَآءٗ وَيَبۡسُطُوٓاْ إِلَيۡكُمۡ أَيۡدِيَهُمۡ وَأَلۡسِنَتَهُم بِٱلسُّوٓءِ وَوَدُّواْ لَوۡ تَكۡفُرُونَ
Wakiwapatia nafasi nyinyi hao mnaowapenda kwa siri watawapiga vita na watanyosha mikono yao kwenu, wawaue nyinyi na wawateke, na pia ndimi zao, wawatukane nyinyi na wawatusi, na wao walitamani, kwa hali yoyote, lau nyinyi mlikanusha kama wao.
Las Exégesis Árabes:
لَن تَنفَعَكُمۡ أَرۡحَامُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُمۡۚ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يَفۡصِلُ بَيۡنَكُمۡۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ
Hawatawanufaisha nyinyi jamaa zenu wa karibu wala watoto wenu kitu chochote mnapofanya urafiki na wakanushaji kwa ajili yao. Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu Atawatenganisha nyinyi na wao, Awatie Peponi wanaomtii na Awatie Motoni wanaomuasi. Na Mwenyezi Mungu Anayaona mnayoyafanya, hakuna chochote kinachofichamana Kwake cha maneno yenu na matendo yenu.
Las Exégesis Árabes:
قَدۡ كَانَتۡ لَكُمۡ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ فِيٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥٓ إِذۡ قَالُواْ لِقَوۡمِهِمۡ إِنَّا بُرَءَٰٓؤُاْ مِنكُمۡ وَمِمَّا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ كَفَرۡنَا بِكُمۡ وَبَدَا بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكُمُ ٱلۡعَدَٰوَةُ وَٱلۡبَغۡضَآءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَحۡدَهُۥٓ إِلَّا قَوۡلَ إِبۡرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسۡتَغۡفِرَنَّ لَكَ وَمَآ أَمۡلِكُ لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖۖ رَّبَّنَا عَلَيۡكَ تَوَكَّلۡنَا وَإِلَيۡكَ أَنَبۡنَا وَإِلَيۡكَ ٱلۡمَصِيرُ
Kwa hakika mlikuwa na kiigizo kizuri, enyi Waumini, kwa Ibrāhīm na wale waliokuwa pamoja na yeye waliposema kuwaambia wakanushaji Mwenyezi Mungu, «Sisi tumejiepusha na nyinyi na vile mnavyoviabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tumewakanusha nyinyi na tumeukataa ukafiri mlionao, na umejitokeza nje uadui na machukivu ya milele baina yetu sisi na nyinyi madamu bado mko kwenye ukanushaji wenu, mpaka mmuamini Mwenyezi Mungu Peke Yake.» Lakini haliingii kwenye kuigiza tendo la Ibrāhīm la kumuombea msamaha babake, kwa kuwa hilo lilitokea kabla ya Ibrāhīm kufunukiwa kuwa babake ni adui wa Mwenyezi Mungu, na alipofunukiwa kuwa yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu alijiepusha na yeye. Mola wetu! Kwako wewe tumetegemea, na kwako wewe tumerejea kwa kutubia, na kwako wewe ndiko marejeo Siku ya Kiyama.
Las Exégesis Árabes:
رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ وَٱغۡفِرۡ لَنَا رَبَّنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Mola wetu! Usitufanye ni mtihani wa wale waliokukanusha wewe, kwa kutuadhibu au kuwapa nguvu makafiri juu yetu wakatufitini kwa kutuepusha na Dini yetu au wakawa na nguvu juu yetu wakafitinika kwa hilo na hapo waseme, «Lau hawa wangalikuwa kwenye haki haingaliwapata adhabu hii,» na wazidi ukafiri. Na utufinikie dhambi zetu kwa kutusamehe, ewe Mola wetu! Hakika wewe ni Mshindi Asiyekuwa na mwenye kushindana Naye, Mwingi wa hekima katika maneno Yake na matendo Yake.
Las Exégesis Árabes:
لَقَدۡ كَانَ لَكُمۡ فِيهِمۡ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ لِّمَن كَانَ يَرۡجُواْ ٱللَّهَ وَٱلۡيَوۡمَ ٱلۡأٓخِرَۚ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡغَنِيُّ ٱلۡحَمِيدُ
Kwa hakika mlikuwa, enyi Waumini, na kiigizo chema kwa Ibrāhīm, amani imshukie, na wale waliokuwa na yeye, kwa anayetumai kupata kheri kutoka kwa Mwenyezi Mungu duniani na Akhera. Na yoyote anayeyapuuza yale ambayo Mwenyezi Mungu Anamuitia nayo ya kuwaiga Manabii Wake na akafanya urafiki na maadui Wake, basi Mwenyezi Mungu Ndiye Mkwasi wa kutowahitajia waja Wake, Ndiye Mwenye kuhimidiwa kwa dhati Yake na sifa Zake, Ndiye Mwenye kushukuriwa kwa namna zote.
Las Exégesis Árabes:
۞ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَجۡعَلَ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَ ٱلَّذِينَ عَادَيۡتُم مِّنۡهُم مَّوَدَّةٗۚ وَٱللَّهُ قَدِيرٞۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Huenda Mwenyezi Mungu Akaweka baina yenu nyinyi, enyi Waumini, na wale jamaa zenu washirikina, ambao mlikuwa na uadui nao, mapenzi baada ya machukivu na maelewano baada ya ugomvi kwa kuvifanya vifua vyao viukunjukie Uislamu. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake ni Mwingi wa huruma Kwao.
Las Exégesis Árabes:
لَّا يَنۡهَىٰكُمُ ٱللَّهُ عَنِ ٱلَّذِينَ لَمۡ يُقَٰتِلُوكُمۡ فِي ٱلدِّينِ وَلَمۡ يُخۡرِجُوكُم مِّن دِيَٰرِكُمۡ أَن تَبَرُّوهُمۡ وَتُقۡسِطُوٓاْ إِلَيۡهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُقۡسِطِينَ
Mwenyezi Mungu Hawakatazi nyinyi, enyi Waumini, kuwakirimu kwa wema makafiri ambao hawakuwapiga nyinyi vita kwa ajili ya dini wala hawakuwatoa kutoka majumbani mwenu, na kuwafanyia usawa kwa hisani yenu na wema wenu kwao, kwani Mwenyezi Mungu Anawapenda wale wanaofanya uadilifu katika maneno yao na matendo yao.
Las Exégesis Árabes:
إِنَّمَا يَنۡهَىٰكُمُ ٱللَّهُ عَنِ ٱلَّذِينَ قَٰتَلُوكُمۡ فِي ٱلدِّينِ وَأَخۡرَجُوكُم مِّن دِيَٰرِكُمۡ وَظَٰهَرُواْ عَلَىٰٓ إِخۡرَاجِكُمۡ أَن تَوَلَّوۡهُمۡۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمۡ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ
Hakika Mwenyezi Mungu Anawakataza, kuhusu wale waliowapiga vita kwa ajili ya dini na wakawatoa majumbani mwenu na wakawasaidia makafiri kuwatoa nyinyi, kufanya urafiki nao kwa kusaidiana na kupendana. Na yoyote anayewachukua wao kuwa ni wasaidizi dhidi ya Waumini na ni vipenzi, basi wao ndio madhalimu wa nafsi zao, wenye kutoka nje ya mipaka ya Mwenyezi Mungu.»
Las Exégesis Árabes:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا جَآءَكُمُ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ مُهَٰجِرَٰتٖ فَٱمۡتَحِنُوهُنَّۖ ٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِإِيمَٰنِهِنَّۖ فَإِنۡ عَلِمۡتُمُوهُنَّ مُؤۡمِنَٰتٖ فَلَا تَرۡجِعُوهُنَّ إِلَى ٱلۡكُفَّارِۖ لَا هُنَّ حِلّٞ لَّهُمۡ وَلَا هُمۡ يَحِلُّونَ لَهُنَّۖ وَءَاتُوهُم مَّآ أَنفَقُواْۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ أَن تَنكِحُوهُنَّ إِذَآ ءَاتَيۡتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّۚ وَلَا تُمۡسِكُواْ بِعِصَمِ ٱلۡكَوَافِرِ وَسۡـَٔلُواْ مَآ أَنفَقۡتُمۡ وَلۡيَسۡـَٔلُواْ مَآ أَنفَقُواْۚ ذَٰلِكُمۡ حُكۡمُ ٱللَّهِ يَحۡكُمُ بَيۡنَكُمۡۖ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo! Wakiwajia nyinyi wanawake Waumini wakiwa wamehama kutoka nchi ya ukafiri kuja kwenye nchi ya Uislamu, wafanyieni mtihani, ili mjue ukweli wa Imani yao, Mwenyezi Mungu Ndiye Mjuzi zaidi wa Imani yao. Mkiwajua kuwa ni Waumini kulingana na alama na ushahidi uliowafunukia, basi msiwarudishe kwa waume wao makafiri. Kwani wanawake Waumini si halali waolewe na makafiri, na makafiri si halali wawaoe wanawake Waumini. Nawapeni waume wa wale wanawake waliosilimu mahari waliotoa kuwapa hao wanawake. Na si dhambi kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao. Na msishikilie kuendelea na ndoa za wake wenu waliokufuru. Na takeni kwa washirikina mrudishiwe mahari mliotoa kuwapa wanawake wenu walioritadi na wakaungana na hao washirikina. Na wao watake kurudishiwa mahari waliotoa kwa wanawake wao waliosilimu na wakaungana na nyinyi. Hukumu hii iliyotajwa katika aya ni hukumu ya Mwenyezi Mungu Anahukumu baina yenu, basi msiende kinyume nayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, hakuna kitu chochote kinachofichamana Kwake, ni Mwingi wa hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake.
Las Exégesis Árabes:
وَإِن فَاتَكُمۡ شَيۡءٞ مِّنۡ أَزۡوَٰجِكُمۡ إِلَى ٱلۡكُفَّارِ فَعَاقَبۡتُمۡ فَـَٔاتُواْ ٱلَّذِينَ ذَهَبَتۡ أَزۡوَٰجُهُم مِّثۡلَ مَآ أَنفَقُواْۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِيٓ أَنتُم بِهِۦ مُؤۡمِنُونَ
Na pindi baadhi ya wake zenu wanaporitadi na kujiunga na makafiri, na makafiri wasiwape mahari yao miliyotoa kuwapatia, kisha mkapambana na hao makafiri na kupata ushindi juu yao, basi wapeni wale Waislamu, ambao wake zao waliondoka, kitu katika ngawira au kinginecho kama kile cha mahari walichowapa kabla ya hapo. Na muogopeni Mwenyezi Mungu mnayemuamini.
Las Exégesis Árabes:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ إِذَا جَآءَكَ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ يُبَايِعۡنَكَ عَلَىٰٓ أَن لَّا يُشۡرِكۡنَ بِٱللَّهِ شَيۡـٔٗا وَلَا يَسۡرِقۡنَ وَلَا يَزۡنِينَ وَلَا يَقۡتُلۡنَ أَوۡلَٰدَهُنَّ وَلَا يَأۡتِينَ بِبُهۡتَٰنٖ يَفۡتَرِينَهُۥ بَيۡنَ أَيۡدِيهِنَّ وَأَرۡجُلِهِنَّ وَلَا يَعۡصِينَكَ فِي مَعۡرُوفٖ فَبَايِعۡهُنَّ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُنَّ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Ewe Nabii! Wakiwajia nyinyi wanawake wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kuwaahidi kuwa hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu katika kumuabudu, wala hawataiba chochote, wala hawatazini, wala hawataua watoto wao baada ya kuzaliwa au kabla yake, wala hawatawanasibishia waume zao watoto wasiotokana na wao, wala hawataenda kinyume na wewe katika jema unalowaamrisha kwalo, basi waahidi kwa hayo na uwaombee msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe sana dhambi za waja Wake wenye kutubia na ni Mwenye kuwarehemu.
Las Exégesis Árabes:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَوَلَّوۡاْ قَوۡمًا غَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ قَدۡ يَئِسُواْ مِنَ ٱلۡأٓخِرَةِ كَمَا يَئِسَ ٱلۡكُفَّارُ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡقُبُورِ
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake! Msiwafanye wale ambao Mwenyezi Mungu Amewakasirikia kwa ukafiri wao kuwa ni marafiki na vipenzi, kwani hao washakata tamaa kupata thawabu za Mwenyezi Mungu kesho Akhera kama makafiri walio makaburini walivyokata tamaa ya kupata rehema ya Mwenyezi Mungu huko Akhera, watakaposhuhudia ukweli wa mambo na wakajua ujuzi wa yakini kuwa hawatakuwa na fungu lolote huko au kama walivyokata tamaa makafiri kufufuliwa wafu wao- walio makaburini- kwa kuitakidi kwao kuwa hakuna kufufuliwa.
Las Exégesis Árabes:
 
Traducción de significados Capítulo: Sura Al-Mumtahana
Índice de Capítulos Número de página
 
Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al idioma swahili- Abdullah Mohamad y Naser Jamis - Índice de traducciones

Traducción del significado del Noble Corán al suajili por el Dr. Abdalla Mohamed Abubakar y Nassor Khamis

Cerrar