Check out the new design

Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - Centre de traduction Rawwâd * - Lexique des traductions


Traduction des sens Sourate: Al Furqâne   Verset:
أَمۡ تَحۡسَبُ أَنَّ أَكۡثَرَهُمۡ يَسۡمَعُونَ أَوۡ يَعۡقِلُونَۚ إِنۡ هُمۡ إِلَّا كَٱلۡأَنۡعَٰمِ بَلۡ هُمۡ أَضَلُّ سَبِيلًا
Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanaelewa? Hao sio isipokuwa ni kama wanyama tu, bali wao wamepotea zaidi njia.
Les exégèses en arabe:
أَلَمۡ تَرَ إِلَىٰ رَبِّكَ كَيۡفَ مَدَّ ٱلظِّلَّ وَلَوۡ شَآءَ لَجَعَلَهُۥ سَاكِنٗا ثُمَّ جَعَلۡنَا ٱلشَّمۡسَ عَلَيۡهِ دَلِيلٗا
Je, huoni jinsi Mola wako Mlezi anavyokitandaza kivuli. Na angelitaka, angelikifanya kikatulia tu. Kisha tumelifanya jua kuwa ni kiongozi wake.
Les exégèses en arabe:
ثُمَّ قَبَضۡنَٰهُ إِلَيۡنَا قَبۡضٗا يَسِيرٗا
Kisha tunakivutia kwetu kidogo kidogo.
Les exégèses en arabe:
وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ لِبَاسٗا وَٱلنَّوۡمَ سُبَاتٗا وَجَعَلَ ٱلنَّهَارَ نُشُورٗا
Naye ndiye aliyewafanyia usiku kuwa ni vazi, na usingizi kuwa mapumziko, na akawafanyia mchana ni kufufuka.
Les exégèses en arabe:
وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَرۡسَلَ ٱلرِّيَٰحَ بُشۡرَۢا بَيۡنَ يَدَيۡ رَحۡمَتِهِۦۚ وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ طَهُورٗا
Naye ndiye anayezituma pepo kuwa bishara njema kabla ya rehema yake, na tunayateremsha kutoka mbinguni maji safi.
Les exégèses en arabe:
لِّنُحۡـِۧيَ بِهِۦ بَلۡدَةٗ مَّيۡتٗا وَنُسۡقِيَهُۥ مِمَّا خَلَقۡنَآ أَنۡعَٰمٗا وَأَنَاسِيَّ كَثِيرٗا
Ili kwa hayo tuihuishe nchi iliyokufa, na tuwanyweshe wanyama na watu wengi tuliowaumba.
Les exégèses en arabe:
وَلَقَدۡ صَرَّفۡنَٰهُ بَيۡنَهُمۡ لِيَذَّكَّرُواْ فَأَبَىٰٓ أَكۡثَرُ ٱلنَّاسِ إِلَّا كُفُورٗا
Na kwa yakini tumeisarifu kati yao wapate kukumbuka. Lakini wengi wa watu wanakataa isipokuwa kukufuru tu.
Les exégèses en arabe:
وَلَوۡ شِئۡنَا لَبَعَثۡنَا فِي كُلِّ قَرۡيَةٖ نَّذِيرٗا
Na tungelitaka, tungelituma katika kila mji Mwonyaji.
Les exégèses en arabe:
فَلَا تُطِعِ ٱلۡكَٰفِرِينَ وَجَٰهِدۡهُم بِهِۦ جِهَادٗا كَبِيرٗا
Basi usiwatii makafiri. Na pambana nao kwayo kwa Jihadi kubwa.
Les exégèses en arabe:
۞ وَهُوَ ٱلَّذِي مَرَجَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ هَٰذَا عَذۡبٞ فُرَاتٞ وَهَٰذَا مِلۡحٌ أُجَاجٞ وَجَعَلَ بَيۡنَهُمَا بَرۡزَخٗا وَحِجۡرٗا مَّحۡجُورٗا
Naye ndiye aliyezipeleka bahari mbili, hii ni tamu mno, na hii ni ya chumvi chungu. Na akaweka baina yake kinga na kizuizi kizuiacho.
Les exégèses en arabe:
وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ مِنَ ٱلۡمَآءِ بَشَرٗا فَجَعَلَهُۥ نَسَبٗا وَصِهۡرٗاۗ وَكَانَ رَبُّكَ قَدِيرٗا
Naye ndiye aliyemuumba mwanaadamu kutokana na maji, akamjaalia kuwa na nasaba na ushemeji. Na Mola wako Mlezi ni Muweza mno.
Les exégèses en arabe:
وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُهُمۡ وَلَا يَضُرُّهُمۡۗ وَكَانَ ٱلۡكَافِرُ عَلَىٰ رَبِّهِۦ ظَهِيرٗا
Na wanayaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yasiyowafaa wala yasiyowadhuru. Na kafiri daima ni msaidizi wa kumpinga Mola wake Mlezi.
Les exégèses en arabe:
 
Traduction des sens Sourate: Al Furqâne
Lexique des sourates Numéro de la page
 
Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - Centre de traduction Rawwâd - Lexique des traductions

L'équipe du Centre Rouwwâd At-Tarjamah (Les Pionniers de la Traduction) l'a traduite.

Fermeture