Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani * - Daftar isi terjemahan

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Terjemahan makna Surah: Surah Al-Lail   Ayah:

Surat Al-Lail

وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰ
Naapa kwa usiku unapo funika!
Naapa kwa usiku kinapo enea kiza chake!
Tafsir berbahasa Arab:
وَٱلنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ
Na mchana unapo dhihiri!
Na naapa kwa mchana unapo zagaa mwangaza wake!
Tafsir berbahasa Arab:
وَمَا خَلَقَ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ
Na kwa Aliye umba dume na jike!
Na naapa kwa Mjuzi aliye umba viwili viwili, dume na jike, katika kila vinavyo zaliwa!
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّ سَعۡيَكُمۡ لَشَتَّىٰ
Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.
Hakika juhudi zenu bila ya shaka zimekhitalifiana; kwani wapo wenye kubahatika katika juhudi zao, na wako wasio bahatika.
Tafsir berbahasa Arab:
فَأَمَّا مَنۡ أَعۡطَىٰ وَٱتَّقَىٰ
Ama mwenye kutoa na akamchamngu!
Ama mwenye kutoa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na akamkhofu Mola wake Mlezi, na kwa hivyo akaepuka anayo yakataza,
Tafsir berbahasa Arab:
وَصَدَّقَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ
Na akaliwafiki lilio jema!
Na akayakinika kufuata fadhila njema, nayo ni Imani kumuamini Mwenyezi Mungu kwa kumjua,
Tafsir berbahasa Arab:
فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلۡيُسۡرَىٰ
Tutamsahilishia yawe mepesi.
Basi Sisi tutamtengenezea awe katika khulka ya wepesi na raha kwa kumwongoza kwenye njia ya kheri.
Tafsir berbahasa Arab:
وَأَمَّا مَنۢ بَخِلَ وَٱسۡتَغۡنَىٰ
Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake!
Ama mwenye kufanya ubakhili kwa mali yake asitoe haki ya Mwenyezi Mungu iliomo humo, na akawa hana haja na yatokayo kwa Mwenyezi Mungu,
Tafsir berbahasa Arab:
وَكَذَّبَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ
Na akakanusha lilio jema!
Na akakadhibisha khulka nzuri,
Tafsir berbahasa Arab:
فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلۡعُسۡرَىٰ
Tutamsahilishia yawe mazito!
Basi huyo tutamtengenezea khulka ambayo inapelekea uzito na mashaka ya milele.
Tafsir berbahasa Arab:
وَمَا يُغۡنِي عَنۡهُ مَالُهُۥٓ إِذَا تَرَدَّىٰٓ
Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia?
Na kitu gani katika adhabu ambacho hayo mali yake yataweza kumkinga nacho, atapo teketea yeye mwenyewe mzima?
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّ عَلَيۡنَا لَلۡهُدَىٰ
Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu.
Hakika ni juu yetu, Sisi, kwa kufuatana na hikima yetu, ndio tuwabainishie viumbe njia ya uwongofu.
Tafsir berbahasa Arab:
وَإِنَّ لَنَا لَلۡأٓخِرَةَ وَٱلۡأُولَىٰ
Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
Na juu yetu Sisi peke yetu, bila ya shaka, hili jambo la kuendesha yaliomo duniani na Akhera.
Tafsir berbahasa Arab:
فَأَنذَرۡتُكُمۡ نَارٗا تَلَظَّىٰ
Basi nakuonyeni na Moto unao waka!
Ndio maana tukakutieni khofu ya Moto unao waka na kuripuka!
Tafsir berbahasa Arab:
لَا يَصۡلَىٰهَآ إِلَّا ٱلۡأَشۡقَى
Hatauingia ila mwovu kabisa!
Hawauingii kwa kudumu ila kafiri
Tafsir berbahasa Arab:
ٱلَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
Anaye kadhibisha na kupa mgongo.
Aliye ikadhibisha Haki na akazipuuza Ishara za Mola wake Mlezi.
Tafsir berbahasa Arab:
وَسَيُجَنَّبُهَا ٱلۡأَتۡقَى
Na mchamngu ataepushwa nao,
Na atakuwa mbali na huo Moto aliye mwingi wa kujikinga na ukafiri na maasi,
Tafsir berbahasa Arab:
ٱلَّذِي يُؤۡتِي مَالَهُۥ يَتَزَكَّىٰ
Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
Amabye hutoa mali yake wakati wa nafasi ili kujisafisha na uchafu wa ubakhili, na najsi ya uchoyo.
Tafsir berbahasa Arab:
وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُۥ مِن نِّعۡمَةٖ تُجۡزَىٰٓ
Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa.
Na mtoaji huyu si kama anaye mtu yeyote ambaye ndio anamlipa kwa neema aliyo mfanyia zamani,
Tafsir berbahasa Arab:
إِلَّا ٱبۡتِغَآءَ وَجۡهِ رَبِّهِ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
Bali anatoa hicho kwa kutafuta radhi ya Mola wake Mlezi Mtukufu tu.
Tafsir berbahasa Arab:
وَلَسَوۡفَ يَرۡضَىٰ
Naye atakuja ridhika!
Na bila ya shaka atakuja pata kutoka kwa Mola wake Mlezi anacho kitaka kwa njia za ukamilifu kabisa, hata itimie radhi kwake.
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Surah: Surah Al-Lail
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani - Daftar isi terjemahan

Terjemahan Makna Al-Qur`ān Al-Karīm ke Bahasa Sawahili oleh Ali Muhsin Al-Barwani

Tutup