Check out the new design

クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - ルゥワード翻訳事業センター * - 対訳の目次


対訳 章: 婦人章   節:
لَّا يَسۡتَوِي ٱلۡقَٰعِدُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ غَيۡرُ أُوْلِي ٱلضَّرَرِ وَٱلۡمُجَٰهِدُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡۚ فَضَّلَ ٱللَّهُ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ عَلَى ٱلۡقَٰعِدِينَ دَرَجَةٗۚ وَكُلّٗا وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَفَضَّلَ ٱللَّهُ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ عَلَى ٱلۡقَٰعِدِينَ أَجۡرًا عَظِيمٗا
Hawawi sawa wanaokaa tu miongoni mwa Waumini wasiokuwa na dharura, na wale wanaopigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Mwenyezi Mungu ameboresha kwa daraja wale wanaopigana kwa mali zao na nafsi zao juu ya wale wanaokaa tu. Na kila mmoja wao Mwenyezi Mungu amemuahidi mazuri mno. Lakini Mwenyezi Mungu amewaboresha kwa ujira mkubwa wale wanaopigana kuliko wale wanaokaa tu.
アラビア語 クルアーン注釈:
دَرَجَٰتٖ مِّنۡهُ وَمَغۡفِرَةٗ وَرَحۡمَةٗۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمًا
Hivyo ni vyeo kutoka kwake, na kufutiwa dhambi, na rehema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kufuta dhambi, na Mwenye kurehemu sana.
アラビア語 クルアーン注釈:
إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ ظَالِمِيٓ أَنفُسِهِمۡ قَالُواْ فِيمَ كُنتُمۡۖ قَالُواْ كُنَّا مُسۡتَضۡعَفِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ قَالُوٓاْ أَلَمۡ تَكُنۡ أَرۡضُ ٱللَّهِ وَٰسِعَةٗ فَتُهَاجِرُواْ فِيهَاۚ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَسَآءَتۡ مَصِيرًا
Hakika, wale ambao Malaika wanawafisha hali ya kuwa wamezidhulumu nafsi zao, watawaambia: 'Mlikuwa katika nini?' Watasema: 'Tulikuwa tumefanywa kuwa wanyoge katika ardhi.' Watawaambia: 'Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa, mkahamie humo?' Basi hao makazi yao ni Jahannam, nayo ni marejeo mabaya kabisa.
アラビア語 クルアーン注釈:
إِلَّا ٱلۡمُسۡتَضۡعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلۡوِلۡدَٰنِ لَا يَسۡتَطِيعُونَ حِيلَةٗ وَلَا يَهۡتَدُونَ سَبِيلٗا
Isipokuwa wale waliodhoofishwa miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto wasioweza hila wala hawawezi kufuata sawasawa njia ya kuhama.
アラビア語 クルアーン注釈:
فَأُوْلَٰٓئِكَ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَعۡفُوَ عَنۡهُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَفُوًّا غَفُورٗا
Basi hao, huenda Mwenyezi Mungu akawasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kufuta dhambi.
アラビア語 クルアーン注釈:
۞ وَمَن يُهَاجِرۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ يَجِدۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُرَٰغَمٗا كَثِيرٗا وَسَعَةٗۚ وَمَن يَخۡرُجۡ مِنۢ بَيۡتِهِۦ مُهَاجِرًا إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ يُدۡرِكۡهُ ٱلۡمَوۡتُ فَقَدۡ وَقَعَ أَجۡرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Na mwenye kuhama katika Njia ya Mwenyezi Mungu, atapata pengi duniani pa kukimbilia, na atapata wasaa. Na mwenye kutoka katika nyumba yake akihamia kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti, basi hakika umekwishawajibika ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
アラビア語 クルアーン注釈:
وَإِذَا ضَرَبۡتُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَلَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَقۡصُرُواْ مِنَ ٱلصَّلَوٰةِ إِنۡ خِفۡتُمۡ أَن يَفۡتِنَكُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْۚ إِنَّ ٱلۡكَٰفِرِينَ كَانُواْ لَكُمۡ عَدُوّٗا مُّبِينٗا
Na mnaposafiri katika nchi, basi hakuna ubaya juu yenu mkifupisha katika Swala, iwapo mnachelea kwamba wale waliokufuru watawajaribu. Hakika, makafiri ni maadui zenu walio wazi.
アラビア語 クルアーン注釈:
 
対訳 章: 婦人章
章名の目次 ページ番号
 
クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - ルゥワード翻訳事業センター - 対訳の目次

ルゥワード翻訳事業センターとラブワ招待協会およびイスラームコンテンツサービス協会の共訳

閉じる