Check out the new design

Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - Centre de traduction Rawwâd * - Lexique des traductions


Traduction des sens Sourate: An Nisâ'   Verset:
لَّا يَسۡتَوِي ٱلۡقَٰعِدُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ غَيۡرُ أُوْلِي ٱلضَّرَرِ وَٱلۡمُجَٰهِدُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡۚ فَضَّلَ ٱللَّهُ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ عَلَى ٱلۡقَٰعِدِينَ دَرَجَةٗۚ وَكُلّٗا وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَفَضَّلَ ٱللَّهُ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ عَلَى ٱلۡقَٰعِدِينَ أَجۡرًا عَظِيمٗا
Hawawi sawa wanaokaa tu miongoni mwa Waumini wasiokuwa na dharura, na wale wanaopigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Mwenyezi Mungu ameboresha kwa daraja wale wanaopigana kwa mali zao na nafsi zao juu ya wale wanaokaa tu. Na kila mmoja wao Mwenyezi Mungu amemuahidi mazuri. Lakini Mwenyezi Mungu amewaboresha kwa ujira mkubwa wale wanaopigana kuliko wale wanaokaa tu.
Les exégèses en arabe:
دَرَجَٰتٖ مِّنۡهُ وَمَغۡفِرَةٗ وَرَحۡمَةٗۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمًا
Hivyo ni vyeo kutoka kwake, na kufutiwa dhambi, na rehema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kufuta dhambi mno, na Mwenye kurehemu sana.
Les exégèses en arabe:
إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ ظَالِمِيٓ أَنفُسِهِمۡ قَالُواْ فِيمَ كُنتُمۡۖ قَالُواْ كُنَّا مُسۡتَضۡعَفِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ قَالُوٓاْ أَلَمۡ تَكُنۡ أَرۡضُ ٱللَّهِ وَٰسِعَةٗ فَتُهَاجِرُواْ فِيهَاۚ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَسَآءَتۡ مَصِيرًا
Hakika, wale ambao Malaika wanawafisha hali ya kuwa wamezidhulumu nafsi zao, watawaambia: Mlikuwa katika nini? Watasema: Tulikuwa tumefanywa kuwa wanyoge katika ardhi. Watawaambia: Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa, mkahamie humo? Basi hao makazi yao ni Jahannam, nayo ni marejeo mabaya kabisa.
Les exégèses en arabe:
إِلَّا ٱلۡمُسۡتَضۡعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلۡوِلۡدَٰنِ لَا يَسۡتَطِيعُونَ حِيلَةٗ وَلَا يَهۡتَدُونَ سَبِيلٗا
Isipokuwa wale waliodhoofishwa miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto wasioweza hila wala hawawezi kufuata sawasawa njia ya kuhama.
Les exégèses en arabe:
فَأُوْلَٰٓئِكَ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَعۡفُوَ عَنۡهُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَفُوًّا غَفُورٗا
Basi hao, huenda Mwenyezi Mungu akawasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kufuta dhambi.
Les exégèses en arabe:
۞ وَمَن يُهَاجِرۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ يَجِدۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُرَٰغَمٗا كَثِيرٗا وَسَعَةٗۚ وَمَن يَخۡرُجۡ مِنۢ بَيۡتِهِۦ مُهَاجِرًا إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ يُدۡرِكۡهُ ٱلۡمَوۡتُ فَقَدۡ وَقَعَ أَجۡرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Na mwenye kuhama katika Njia ya Mwenyezi Mungu, atapata pengi duniani pa kukimbilia, na atapata wasaa. Na mwenye kutoka katika nyumba yake akihamia kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti, basi hakika umekwisha wajibika ujira kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Les exégèses en arabe:
وَإِذَا ضَرَبۡتُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَلَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَقۡصُرُواْ مِنَ ٱلصَّلَوٰةِ إِنۡ خِفۡتُمۡ أَن يَفۡتِنَكُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْۚ إِنَّ ٱلۡكَٰفِرِينَ كَانُواْ لَكُمۡ عَدُوّٗا مُّبِينٗا
Na mnaposafiri katika nchi, basi hakuna ubaya juu yenu mkifupisha katika Swala, iwapo mnachelea kwamba wale waliokufuru watawajaribu. Hakika, makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.
Les exégèses en arabe:
 
Traduction des sens Sourate: An Nisâ'
Lexique des sourates Numéro de la page
 
Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - Centre de traduction Rawwâd - Lexique des traductions

L'équipe du Centre Rouwwâd At-Tarjamah (Les Pionniers de la Traduction) l'a traduite.

Fermeture