Check out the new design

Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - Centre de traduction Rawwâd * - Lexique des traductions


Traduction des sens Sourate: An Nisâ'   Verset:
وَمَا لَكُمۡ لَا تُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلۡمُسۡتَضۡعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلۡوِلۡدَٰنِ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَخۡرِجۡنَا مِنۡ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلظَّالِمِ أَهۡلُهَا وَٱجۡعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيّٗا وَٱجۡعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا
Na mna nini hampigani katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na ya wale wanaoonewa miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tufanyie mlinzi kutoka kwako, na tufanyie wa kutunusuru kutoka kwako.
Les exégèses en arabe:
ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱلطَّٰغُوتِ فَقَٰتِلُوٓاْ أَوۡلِيَآءَ ٱلشَّيۡطَٰنِۖ إِنَّ كَيۡدَ ٱلشَّيۡطَٰنِ كَانَ ضَعِيفًا
Wale walioamini wanapigana vita katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wale waliokufuru wanapiana vita katika njia ya Twaghut. Basi piganeni na marafiki wa Shetani. Hakika, hila ya Shetani ni dhaifu.
Les exégèses en arabe:
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ قِيلَ لَهُمۡ كُفُّوٓاْ أَيۡدِيَكُمۡ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقِتَالُ إِذَا فَرِيقٞ مِّنۡهُمۡ يَخۡشَوۡنَ ٱلنَّاسَ كَخَشۡيَةِ ٱللَّهِ أَوۡ أَشَدَّ خَشۡيَةٗۚ وَقَالُواْ رَبَّنَا لِمَ كَتَبۡتَ عَلَيۡنَا ٱلۡقِتَالَ لَوۡلَآ أَخَّرۡتَنَآ إِلَىٰٓ أَجَلٖ قَرِيبٖۗ قُلۡ مَتَٰعُ ٱلدُّنۡيَا قَلِيلٞ وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لِّمَنِ ٱتَّقَىٰ وَلَا تُظۡلَمُونَ فَتِيلًا
Je, hukuwaona wale walioambiwa: ‘Izuieni mikono yenu, na mshike Swala na mtoe Zaka.’ Na pindi walipoamrishwa kupigana, mara kundi moja miongoni mwao likawaogopa watu kama kumwogopa Mwenyezi Mungu, au kwa hofu kubwa zaidi. Na wakasema: ‘Mola wetu Mlezi! Kwa nini umetuamrisha kupigana? Laiti ungetuahirishia kiasi ya muda kidogo hivi!’ Sema: ‘Starehe ya dunia ni ndogo, na Akhera ni bora zaidi kwa mwenye kuchamungu. Wala hamtadhulumiwa hata uzi wa kokwa ya tende.’
Les exégèses en arabe:
أَيۡنَمَا تَكُونُواْ يُدۡرِككُّمُ ٱلۡمَوۡتُ وَلَوۡ كُنتُمۡ فِي بُرُوجٖ مُّشَيَّدَةٖۗ وَإِن تُصِبۡهُمۡ حَسَنَةٞ يَقُولُواْ هَٰذِهِۦ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةٞ يَقُولُواْ هَٰذِهِۦ مِنۡ عِندِكَۚ قُلۡ كُلّٞ مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِۖ فَمَالِ هَٰٓؤُلَآءِ ٱلۡقَوۡمِ لَا يَكَادُونَ يَفۡقَهُونَ حَدِيثٗا
Popote mtakapokuwa, mauti yatawafikia, hata kama mtakuwa katika ngome zilizoimarishwa. Na likiwapata zuri, wanasema: Hili limetoka kwa Mwenyezi Mungu. Na likiwapata ovu, wanasema: Hili limetoka kwako wewe. Sema: Yote hayo yanatokana na Mwenyezi Mungu. Basi wana nini watu hawa hata hawakaribii kufahamu maneno?
Les exégèses en arabe:
مَّآ أَصَابَكَ مِنۡ حَسَنَةٖ فَمِنَ ٱللَّهِۖ وَمَآ أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٖ فَمِن نَّفۡسِكَۚ وَأَرۡسَلۡنَٰكَ لِلنَّاسِ رَسُولٗاۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدٗا
Yaliyokupata katika mazuri, basi ni kutokana na Mwenyezi Mungu. Na yaliyokusibu katika maovu, basi ni kutokana na nafsi yako. Nasi tumekutuma kwa watu uwe ni Mtume. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi.
Les exégèses en arabe:
 
Traduction des sens Sourate: An Nisâ'
Lexique des sourates Numéro de la page
 
Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - Centre de traduction Rawwâd - Lexique des traductions

L'équipe du Centre Rouwwâd At-Tarjamah (Les Pionniers de la Traduction) l'a traduite.

Fermeture