Check out the new design

クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - ルゥワード翻訳事業センター * - 対訳の目次


対訳 章: 家畜章   節:
وَلَوۡ جَعَلۡنَٰهُ مَلَكٗا لَّجَعَلۡنَٰهُ رَجُلٗا وَلَلَبَسۡنَا عَلَيۡهِم مَّا يَلۡبِسُونَ
Na kama tungelimfanya Malaika, bila ya shaka tungelimfanya kuwa mwanamume, na tungeliwatilia matatizo yale wanayoyatatiza wao.
アラビア語 クルアーン注釈:
وَلَقَدِ ٱسۡتُهۡزِئَ بِرُسُلٖ مِّن قَبۡلِكَ فَحَاقَ بِٱلَّذِينَ سَخِرُواْ مِنۡهُم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ
Na hakika walifanyiwa mzaha Mitume waliokuwa kabla yako, lakini wale waliowafanyia mzaha yakawafika yale yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.
アラビア語 クルアーン注釈:
قُلۡ سِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ ثُمَّ ٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُكَذِّبِينَ
Sema: Tembeeni katika dunia, kisha mtazame vipi ulikuwa mwisho wa wanaokadhibisha.
アラビア語 クルアーン注釈:
قُل لِّمَن مَّا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ قُل لِّلَّهِۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفۡسِهِ ٱلرَّحۡمَةَۚ لَيَجۡمَعَنَّكُمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ لَا رَيۡبَ فِيهِۚ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ فَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ
Sema: Ni vya nani vilivyo katika mbingu na katika ardhi? Sema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Yeye ameiandika rehemu juu ya nafsi yake. Hakika atawakusanya hadi Siku ya Qiyama isiyokuwa na shaka. Wale waliojihasiri nafsi zao, wao hawaamini.
アラビア語 クルアーン注釈:
۞ وَلَهُۥ مَا سَكَنَ فِي ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ
Na ni vyake vilivyotulia katika usiku na mchana. Naye ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
アラビア語 クルアーン注釈:
قُلۡ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَتَّخِذُ وَلِيّٗا فَاطِرِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَهُوَ يُطۡعِمُ وَلَا يُطۡعَمُۗ قُلۡ إِنِّيٓ أُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ أَوَّلَ مَنۡ أَسۡلَمَۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Sema: Je, nimfanye rafiki mwandani asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mwanzilishi wa mbingu na ardhi, naye ndiye anayelisha wala halishwi? Sema: Hakika Mimi nimeamrishwa kwamba niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina.
アラビア語 クルアーン注釈:
قُلۡ إِنِّيٓ أَخَافُ إِنۡ عَصَيۡتُ رَبِّي عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ
Sema: Hakika Mimi ninahofu nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku kubwa.
アラビア語 クルアーン注釈:
مَّن يُصۡرَفۡ عَنۡهُ يَوۡمَئِذٖ فَقَدۡ رَحِمَهُۥۚ وَذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡمُبِينُ
Mwenye kuepushwa nayo Siku hiyo, basi hakika atakuwa amemrehemu. Na huko ndiko kufuzu kuliko wazi.
アラビア語 クルアーン注釈:
وَإِن يَمۡسَسۡكَ ٱللَّهُ بِضُرّٖ فَلَا كَاشِفَ لَهُۥٓ إِلَّا هُوَۖ وَإِن يَمۡسَسۡكَ بِخَيۡرٖ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ
Na ikiwa Mwenyezi Mungu akikugusa kwa madhara, basi hapana wa kuyaondoa isipokuwa Yeye. Na ikiwa akikugusa kwa heri, basi Yeye ndiye Muweza wa kila kitu.
アラビア語 クルアーン注釈:
وَهُوَ ٱلۡقَاهِرُ فَوۡقَ عِبَادِهِۦۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡخَبِيرُ
Naye ndiye Mwenye nguvu juu ya waja wake, naye ndiye Mwenye hekima, Mwenye habari zote.
アラビア語 クルアーン注釈:
 
対訳 章: 家畜章
章名の目次 ページ番号
 
クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - ルゥワード翻訳事業センター - 対訳の目次

ルゥワード翻訳事業センターとラブワ招待協会およびイスラームコンテンツサービス協会の共訳

閉じる