Check out the new design

クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - ルゥワード翻訳事業センター * - 対訳の目次


対訳 章: 家畜章   節:
وَلَا تَقۡرَبُواْ مَالَ ٱلۡيَتِيمِ إِلَّا بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ أَشُدَّهُۥۚ وَأَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ وَٱلۡمِيزَانَ بِٱلۡقِسۡطِۖ لَا نُكَلِّفُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَاۖ وَإِذَا قُلۡتُمۡ فَٱعۡدِلُواْ وَلَوۡ كَانَ ذَا قُرۡبَىٰۖ وَبِعَهۡدِ ٱللَّهِ أَوۡفُواْۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ
Wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kile kilicho kizuri kabisa mpaka afike utu uzima wake. Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu. Hatuibebeshi nafsi isipokuwa kwa uwezo wake. Na mnaposema, basi fanyeni uadilifu hata kama ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu,itimizeni. Hayo amewausia ili mkumbuke.
アラビア語 クルアーン注釈:
وَأَنَّ هَٰذَا صِرَٰطِي مُسۡتَقِيمٗا فَٱتَّبِعُوهُۖ وَلَا تَتَّبِعُواْ ٱلسُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمۡ عَن سَبِيلِهِۦۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ
Na kwamba hakika hii ndiyo Njia yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Wala msifuate njia nyinginezo, zikawatengeni na Njia yake. Haya amewausia ili mmche (Mwenyezi Mungu).
アラビア語 クルアーン注釈:
ثُمَّ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ تَمَامًا عَلَى ٱلَّذِيٓ أَحۡسَنَ وَتَفۡصِيلٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لَّعَلَّهُم بِلِقَآءِ رَبِّهِمۡ يُؤۡمِنُونَ
Tena tulimpa Musa Kitabu kwa kumtimizia (neema) yule aliyefanya uzuri, na kuwa ni maelezo kina ya kila kitu, na uwongofu na rehema, ili waamini katika kukutana na Mola wao Mlezi.
アラビア語 クルアーン注釈:
وَهَٰذَا كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ مُبَارَكٞ فَٱتَّبِعُوهُ وَٱتَّقُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ
Na hiki ni Kitabu tulichokiteremsha, kilichobarikiwa. Basi kifuateni, na mcheni, ili mrehemewe.
アラビア語 クルアーン注釈:
أَن تَقُولُوٓاْ إِنَّمَآ أُنزِلَ ٱلۡكِتَٰبُ عَلَىٰ طَآئِفَتَيۡنِ مِن قَبۡلِنَا وَإِن كُنَّا عَن دِرَاسَتِهِمۡ لَغَٰفِلِينَ
Mkaja kusema, “Hakika waliteremshiwa Kitabu makundi mawili tu kabla yetu, na sisi tulikuwa hatuna habari ya waliyokuwa wakiyasoma.”
アラビア語 クルアーン注釈:
أَوۡ تَقُولُواْ لَوۡ أَنَّآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا ٱلۡكِتَٰبُ لَكُنَّآ أَهۡدَىٰ مِنۡهُمۡۚ فَقَدۡ جَآءَكُم بَيِّنَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞۚ فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَصَدَفَ عَنۡهَاۗ سَنَجۡزِي ٱلَّذِينَ يَصۡدِفُونَ عَنۡ ءَايَٰتِنَا سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ بِمَا كَانُواْ يَصۡدِفُونَ
Au mkasema: "Lau hakika sisi tungeteremshiwa Kitabu hicho, basi tungelikuwa waongofu zaidi kuwaliko wao." Basi hakika imekwisha wajia hoja iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema. Kwa hivyo, ni nani aliye dhalimu mkubwa zaidi kuliko yule anayekadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipa wale wanaojitenga na Ishara zetu adhabu mbaya kabisa kwa sababu ya walivyokuwa wakijitenga.
アラビア語 クルアーン注釈:
 
対訳 章: 家畜章
章名の目次 ページ番号
 
クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - ルゥワード翻訳事業センター - 対訳の目次

ルゥワード翻訳事業センターとラブワ招待協会およびイスラームコンテンツサービス協会の共訳

閉じる