Check out the new design

ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី * - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អ៊ីព្រហ៊ីម   អាយ៉ាត់:
تُؤۡتِيٓ أُكُلَهَا كُلَّ حِينِۭ بِإِذۡنِ رَبِّهَاۗ وَيَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡأَمۡثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ
Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano ili wapate kukumbuka. [25]
[25] Hutoa matunda yake kila wakati aliyo uweka Mwenyezi Mungu yazae kwa mapendekezo ya aliye yaumba. Hivyo hivyo ndio tamshi la Tawhid, Upweke wa Mwenyezi Mungu, ni lenye kuthibiti katika moyo wa Muumini. A'mali yake inapanda kwa Mwenyezi Mungu, na inamfikilia baraka zake na thawabu zake kila wakati. Na Mwenyezi Mungu anawabainishia watu kwa mifano, anashabihisha maana kwa vitu wavijuavyo ili Waumini wawaidhike.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٖ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ ٱجۡتُثَّتۡ مِن فَوۡقِ ٱلۡأَرۡضِ مَا لَهَا مِن قَرَارٖ
Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, ulio ng'olewa juu ya ardhi. Hauna imara. [26]
[26] Neno la uwongo baya mfano wake ni kama mti mbaya ulio ng'olewa, umetupwa juu ya ardhi. Haukusimama imara. Hali kadhaalika neno la uwongo lilio kataliwa halina uthabiti, kwa kuwa halikuungwa mkono na hoja.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
يُثَبِّتُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱلۡقَوۡلِ ٱلثَّابِتِ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِۖ وَيُضِلُّ ٱللَّهُ ٱلظَّٰلِمِينَۚ وَيَفۡعَلُ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُ
Mwenyezi Mungu huwatia imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha ya dunia na katika Akhera. Na Mwenyezi Mungu huwaacha kupotea hao wenye kudhulumu. Na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo. [27]
[27] Mwenyezi Mungu anawathibitisha imara wanao amini juu ya neno la Haki katika uhai wa duniani na Siku ya Kiyama pia. Na Mwenyezi Mungu huwabaidisha nalo neno hilo makafiri kwa kutojitengenezea wenyewe. Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo, akiwathibitisha baadhi na kuwaacha kupotea wenginewe. Hapana wa kumtoa kombo kwa hukumu yake, wala mwenye kuurudisha uamuzi wake!
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
۞ أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ بَدَّلُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ كُفۡرٗا وَأَحَلُّواْ قَوۡمَهُمۡ دَارَ ٱلۡبَوَارِ
Hebu hukuwaona wale walio badilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru, na wakawafikisha watu wao kwenye nyumba ya maangamizo? [28]
[28] Ewe msikilizaji! Hebu huwaangalii hao washirikina ambao, badala ya kushukuru neema ya Mwenyezi Mungu ya kumleta Muhammad na Dini yake, wakaingia kumkataa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wakawasabibisha wafwasi wao kutumbukia katika nyumba ya hilaki kwa upotovu wao.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
جَهَنَّمَ يَصۡلَوۡنَهَاۖ وَبِئۡسَ ٱلۡقَرَارُ
Nayo ni Jahannamu! Wataingia, Maovu yaliyoje makaazi hayo! [29]
[29] Na nyumba hiyo ndiyo Jahannamu wakiteswa kwa uvukuto wake. Na makaazi maovu mno ni Jahannamu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَجَعَلُواْ لِلَّهِ أَندَادٗا لِّيُضِلُّواْ عَن سَبِيلِهِۦۗ قُلۡ تَمَتَّعُواْ فَإِنَّ مَصِيرَكُمۡ إِلَى ٱلنَّارِ
Na walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili wapoteze watu kwenye Njia yake. Sema: Stareheni! Kwani marejeo yenu ni Motoni! [30]
[30] Na wakamfanyia Mwenyezi Mungu Mmoja wa pekee mifano ya masanamu wakiyaabudu, kwa ajili ya kuwa natija ya vitendo vyao iwe kuwapoteza watu wasifuate Njia ya Mwenyezi Mungu! Ewe Nabii! Waambie hao walio potea: Stareheni na matamanio yenu, kwani marejeo yenu ni Motoni!
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قُل لِّعِبَادِيَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُنفِقُواْ مِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ سِرّٗا وَعَلَانِيَةٗ مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ يَوۡمٞ لَّا بَيۡعٞ فِيهِ وَلَا خِلَٰلٌ
Waambie waja wangu walio amini, washike Swala, na watoe katika tulivyo waruzuku, kwa siri na dhaahiri, kabla haijafika Siku isiyo kuwa na biashara wala urafiki. [31]
[31] Ewe Muhammad! Waambie waja wangu walio sadiki, wakaamini, na wakatenda mema: Shikeni Swala, na toeni baadhi ya tuliyo kuruzukuni katika njia za kheri, kwa siri na kwa dhaahiri, kabla ya kufika siku ambayo haifai kitu kupatana kibiashara wala hisani ya urafiki.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجَ بِهِۦ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ رِزۡقٗا لَّكُمۡۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلۡفُلۡكَ لِتَجۡرِيَ فِي ٱلۡبَحۡرِ بِأَمۡرِهِۦۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلۡأَنۡهَٰرَ
Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akateremsha maji kutoka mbinguni. Na kwa hayo akatoa matunda kuwa ni riziki yenu. Na akafanya yakutumikieni majahazi yanayo pita baharini kwa amri yake, na akaifanya mito ikutumikieni. [32]
[32] Ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye zianzisha mbingu na viliomo ndani yake, na ardhi na viliomo ndani yake. Na akateremsha kutoka mawinguni maji ya kumiminika. Na kwa sababu yake akakutoleeni riziki ya matunda, na mazao mengine na miti. Na Yeye akakufanyieni vyombo vya baharini vikufaeni vinakwenda na kupakia riziki zenu, na bidhaa zenu za biashara, kwa idhini yake na kutaka kwake. Na akaifanya mito ya maji matamu ikunufaisheni kwa kunywa nyinyi na kumwagia katika mashamba yenu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ دَآئِبَيۡنِۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ
Na akalifanya jua na mwezi kwa manufaa yenu daima dawamu, na akaufanya usiku na mchana kwa manufaa yenu. [33]
[33] Na akalifanya jua na mwezi yakufaeni daima dawamu, kwa mwangaza na maslaha ya mimea na wanyama. Na akajaalia usiku ukufaeni kwa kupumzika na mchana kwa kufanya kazi.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
 
ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អ៊ីព្រហ៊ីម
សន្ទស្សន៍នៃជំពូក លេខ​ទំព័រ
 
ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

បកប្រែដោយលោកអាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

បិទ