Na akakupeni kila mlicho muomba. Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamwezi kuzidhibiti. Hakika mwanaadamu ni dhaalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema. [34]
[34] Na akakutengenezeeni yote mnayo yahitajia katika maisha yenu ambayo anastahiki kuombwa, sawa sawa ikiwa mmemuomba au la. Na mkizihisabu neema alizo kuneemesheni Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti namna zake, seuze idadi yake! Hakika huyo mwenye kukanya ambaye akalipa ukafiri kuwa ni malipo ya neema alizo pewa, basi ni mwingi wa udhalimu na ukafiri!
Na Ibrahim alipo sema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ujaalie mji huu uwe wa amani, na uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu. [35]
[35] Ewe Nabii! Ili watu wako wapate kuzingatia na waache ushirikina wao, wakumbushe kauli ya baba yao Ibrahim baada ya kuijenga Alkaaba. Alisema: Ewe Mola Mlezi! Ujaalie mji huu wenye Alkaaba uwe wa amani, ulindwe na wenye kudhulumu. Na unibaidishe, niwe mbali, mimi na wanangu na ibada ya masanamu.
Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hayo yamewapoteza watu wengi. Basi aliye nifuata mimi huyo ni wangu, na aliye niasi, hakika Wewe ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [36]
[36] Kwani masanamu yamepelekea kupotea watu wengi kwa kuyaabudu. Basi katika dhuriya zangu, wenye kunifuata mimi na wakakuabudu Wewe kwa ikhlasi, basi hao ni watu wa Dini yangu. Na wenye kuniasi kwa kushika ushirikina, basi Wewe ni Muweza wa kuwaongoa, kwani Wewe ni Mwingi wa maghfira na rehema.
Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuriya zangu katika bonde lisilo kuwa na mimea, kwenye Nyumba yako Takatifu, ewe Mola wetu Mlezi, ili washike Swala. Basi zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao, na waruzuku matunda, ili wapata kushukuru. [37]
[37] Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewafanyia maskani baadhi ya dhuriya zangu katika bonde la Makka ambalo halioti mimea, kwenye Nyumba yako uliyo kataza isiingiliwe na kuvunjiwa hishima yake, na ukajaalia sehemu za jirani yake ziwe na amani. Ewe Mola wetu Mlezi! Wakirimu wapate kushika Swala karibu na Nyumba hii. Na zijaalie nyoyo za bora ya watu ziwapende kwa kuizuru Nyumba yako. Na uwaruzuku matunda kwa kuletwa na hao watakao kuja, ili wapate kushukuru neema yako kwa Swala na Dua.
Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe unajua tunayo yaficha na tunayo yatangaza. Na hapana kitu kinacho fichikana kwa Mwenyezi Mungu katika ardhi wala katika mbingu. [38]
[38] Ewe Mola wetu Mlezi! Ni sawa sawa kwako tunayo fanya siri na tunayo fanya dhaahiri. Kwani Wewe unajua maslaha yetu, na unatuonea huruma zaidi kuliko sisi wenyewe. Na hapana lifichikanalo kwako hata likiwa dogo, katika ardhi na katika mbingu. Basi hapana haja sisi ya kukuomba. Lakini juu ya hivyo tunaomba kwa kuonyesha kuwa sisi ni waja wako, twanyenyekea utukufu wako, na tunahitajia uliyo nayo, Wewe!
Alhamdulillahi! Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu aliye nipa juu ya uzee wangu Ismail na Is-haq. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia maombi. [39]
[39] Alhamdulillahi, Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu, aliye nipa juu ya kuwa ni mzee wa miaka mingi, na nimekwisha kata tamaa ya kuzaa, Ismail na kisha Is-haq! Hakika Mwenyezi Mungu anasikia na ananipokelea maombi yangu.
Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kushika Swala, na katika dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu. [40]
[40] Ewe Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nitimize Swala kwa inavyo takikana. Na wawezeshe watimilize kadhaalika wale walio wa kheri katika dhuriya zangu. Ewe Mola wetu Mlezi ipokee dua yangu kwa mapokezi ya kukubaliwa.
Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao. [42]
[42] Ewe Mtume! Wala usidhani kabisa kuwa Mola wako Mlezi ameghafilika na vitendo wafanyavyo wenye kudhulumu, kuupiga vita Uislamu na Waislamu wenyewe. Bali Yeye anaujua ukhalifu wao. Na amekadiria kuakhirisha kuwaadhibu mpaka Siku nzito. Macho yao yatabaki yamekodoka, hawawezi kuyafumba, wala kupepesa kwa kitisho watacho kiona.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
លទ្ធផលស្វែងរក:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".